‘Nimetoa maagizo yote muhimu kwa makabidhiano ya mamlaka’ - Uhuru Kenyatta

Chanzo cha picha, State House Kenya
Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza kujitolea kwake kusimamia makabidhiano ya amani ya mamlaka kwa utawala ujao.
Katika hotuba yake iliyopeperushwa kwenye runinga Jumatatu jioni, Uhuru alisema kwa kutii kiapo alichotoa alipochukua madaraka cha kuzingatia sheria na kuheshimu maamuzi ya michakato ya mahakama, ataheshimu uamuzi wa Mahakama ya Juu zaidi wa kuidhinisha uchaguzi wa William Ruto kama Rais mteule.
"Ninajitolea kutekeleza maagizo ya mahakama hii kwa mahakama hii," Uhuru alisema.
"Ni nia yangu kusimamia makabidhiano ya amani kwa utawala ujao na maagizo yote muhimu ya kuwezesha mchakato huu tayari yametolewa," aliongeza.
Mkuu huyo wa nchi hakumpongeza Ruto lakini aliwapongeza Wakenya kwa kudumisha amani wakati wote wa mchakato wa uchaguzi na wakati matokeo yalipopingwa mahakamani.

Heshima kwa rais anayeondoka
Rais mteule ameweka wazi maono yake ya Kenya ya kidemokrasia ambayo haina vitisho."
Hii inaashiria mwisho wa siasa za udanganyifu, usaliti na ujanja," amesema."
Tunataka siasa za Kenya za siku zijazo - kila kiongozi lazima ahukumiwe kwa kile anachosema na kile anachosema ndicho anachofanya."
Bw Ruto anahisi kuwa yeye na wafuasi wake wakati fulani wamenyanyaswa.
"Tunataka kuwa na nchi inayozingatia utawala wa sheria - mfumo wa haki ya jinai utawekwa kwa ajili ya kupata wahalifu na uhalifu - hautatumika tena kwa sababu za kisiasa ... dhidi ya wale ambao wana maoni kinyume na yetu.
"Pia amesema kuwa Bw Kenyatta atatendewa vyema."Tutaheshimu rais wetu katika kustaafu kwake ... sisi ni watu wa heshima, sisi sio wadogo na hatuna wivu.
Amefanya kazi nzuri na atakuwa na nafasi yake katika historia ya Kenya.
Hakuna mtu anayepaswa kushikilia chochote dhidi ya rais. wa Kenya.
"Naye Bw Odinga ataheshimiwa, ameongeza.
Kuunganisha taifa
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Rais mteule wa Kenya William Ruto amejaribu kukomesha mgawanyiko nchini Kenya na kutengeneza njia ya umoja akisema demokrasia haipaswi kuwa "biashara ya kiharamia".
Alinyoosha mkono wa urafiki kwa wapinzani wake wa kisiasa, akisema waliowapigia kura washindani wake wote wanaitakia Kenya kilicho bora na kwamba amejitolea kutimiza hilo."Sisi si maadui, sisi ni Wakenya.
Tuungane kuifanya Kenya kuwa taifa ambalo kila mtu atajivunia kuliita nyumbani kwake."Pia alisema atatawala kwa ajili ya watu wote, bila kujali "hali zao za kijamii, dini, kabila na jinsia".
William Ruto amesifu utendakazi wa tume ya uchaguzi (IEBC) akizungumzia maafisa ambao wamepoteza maisha na wamekuwa wakitishwa “na kila aina ya majaribio ya kupotosha matakwa ya wananchi”.
Lakini pia amesema wale waliowasilisha ombi kwa Mahakama ya Juu kupinga matokeo ya Agosti 9 akisema ni haki yao ya kikatiba.
"Ilikuwa ni halali kabisa kwa walalamishi kwenda mbele ya Mahakama ya Juu ili maswali yao yajibiwe."
















