Rais mteule wa Kenya William Ruto aahidi kuliunganisha taifa

Chanzo cha picha, WILLIAM RUTO/TWITTER
Rais mteule wa Kenya, ambaye ushindi wake umeidhinishwa na mahakama, ameahidi kuunganisha nchi hiyo na kuwahakikishia wanaotofautiana naye kuwa hawatadhulumiwa.
William Ruto pia amesema hajazungumza na rais anayeondoka, Uhuru Kenyatta, kwa miezi kadhaa, lakini sasa atampigia simu kujadili mabadiliko hayo.
Viongozi hao wawili walitofautiana miaka mitano iliyopita na Bw. Kenyatta alimuunga mkono aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga.
William Ruto amesema hana hasira kwamba Rais Kenyatta alichagua kumuunga mkono mpinzani wake. Alimhakikishia kiongozi huyo anayeondoka kwamba atapewa hadhi na heshima akistaafu, kama atakavyokuwa Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga atakapoondoka kwenye jukwaa la kisiasa.
Rais mteule amekuwa na uhusiano mbaya na Bw Kenyatta, ambaye alimuunga mkono katika mihula yake miwili ya uongozi.
"Hakuna mtu atakayetukanwa, kudhulumiwa au kufunguliwa mashtaka kwa kuwa na maoni kinyume na yetu," alisema Bw. Ruto. Akisisitiza kuwa ndivyo yeye na viongozi waliomuunga mkono wamekuwa wakipitia.
Alikaribisha uamuzi wa Mahakama ya Juu zaidi wa kuidhinisha ushindi wake na kusema unaleta tamati mchakato wa muda mrefu wa uchaguzi .

Demokrasia nchini
Rais mteule ameweka wazi maono yake ya Kenya ya kidemokrasia ambayo haina vitisho.
"Hii inaashiria mwisho wa siasa za udanganyifu, usaliti na ujanja," amesema.
"Tunataka siasa za Kenya za siku zijazo - kila kiongozi lazima ahukumiwe kwa kile anachosema na kile anachosema ndicho anachofanya."
Bw Ruto anahisi kuwa yeye na wafuasi wake wakati fulani wamenyanyaswa.
"Tunataka kuwa na nchi inayozingatia utawala wa sheria - mfumo wa haki ya jinai utawekwa kwa ajili ya kupata wahalifu na uhalifu - hautatumika tena kwa sababu za kisiasa ... dhidi ya wale ambao wana maoni kinyume na yetu."
Pia amesema kuwa Bw Kenyatta atatendewa vyema.
"Tutaheshimu rais wetu katika kustaafu kwake ... sisi ni watu wa heshima, sisi sio wadogo na hatuna wivu. Amefanya kazi nzuri na atakuwa na nafasi yake katika historia ya Kenya. Hakuna mtu anayepaswa kushikilia chochote dhidi ya rais. wa Kenya."
Naye Bw Odinga ataheshimiwa, ameongeza.
'Nawanyooshea mkono wa urafiki wapinzani wangu' - Ruto
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Rais mteule wa Kenya William Ruto amejaribu kukomesha mgawanyiko nchini Kenya na kutengeneza njia ya umoja akisema demokrasia haipaswi kuwa "biashara ya kiharamia".
Alinyoosha mkono wa urafiki kwa wapinzani wake wa kisiasa, akisema waliowapigia kura washindani wake wote wanaitakia Kenya kilicho bora na kwamba amejitolea kutimiza hilo.
"Sisi si maadui, sisi ni Wakenya.
Tuungane kuifanya Kenya kuwa taifa ambalo kila mtu atajivunia kuliita nyumbani kwake."
Pia alisema atatawala kwa ajili ya watu wote, bila kujali "hali zao za kijamii, dini, kabila na jinsia".
William Ruto amesifu utendakazi wa tume ya uchaguzi (IEBC) akizungumzia maafisa ambao wamepoteza maisha na wamekuwa wakitishwa “na kila aina ya majaribio ya kupotosha matakwa ya wananchi”.
Lakini pia amesema wale waliowasilisha ombi kwa Mahakama ya Juu kupinga matokeo ya Agosti 9 akisema ni haki yao ya kikatiba.
"Ilikuwa ni halali kabisa kwa walalamishi kwenda mbele ya Mahakama ya Juu ili maswali yao yajibiwe."
‘Tutafanya kazi kwa bidii, hatutawaangusha’

Chanzo cha picha, William Ruto/Twitter
"Tuliombewa ushindi, watu wengi waliomba, watu wengi walifunga na tunashukuru kweli na hatutakuangusha, tutafanya kazi kwa bidii na hatutakuangusha.
Pia aliwashukuru washirika wake wa kisiasa.“Wengi mmepelekwa mahakamani, wengi mmenyanyaswa... kosa lenu lilikuwa ni kuwa rafiki yangu."Lakini tuliamini katika Kenya bora, Kenya iliyo huru zaidi ya kidemokrasia."
Rais mteule wa Kenya amesema anakaribisha uamuzi wa Mahakama ya Juu zaidi wa kudumisha ushindi wake wa uchaguzi kwa "unyenyekevu wa hali ya juu" na kuwasifu majaji kwa "kutopendelea upande wowote" na "uzalendo".
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari alisema kuwa uamuzi wao unaashiria mwisho wa uchaguzi wa Kenya: "Uchaguzi wetu wa muda mrefu, wenye mashaka na wa muda mrefu umefikia kikomo.
"Pia alisema ushindi wake ulikuwa chanzo cha msukumo kwa vijana wa Kenya."Nadhani kuchaguliwa kwangu kunafungua uwezekano kwa watoto wetu wote bila kujali asili zao".















