Uchaguzi Kenya: Ni upi msingi wa pingamizi la Odinga mahakamani?

Mgombea aliyeshindwa katika uchaguzi wa urais Raila Odinga na mgombea mwenza , Martha Karua

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mgombea aliyeshindwa katika uchaguzi wa urais Raila Odinga na mgombea mwenza, Martha Karua

Raila Odinga mgombea wa urais aliyeshindwa katika uchaguzi wa hivi karibuni nchini Kenya, amewasilisha pingamizi la kisheria dhidi ya matokeo, ambayo William Ruto alitangazwa kuwa mshindi.

Tumekuwa tukiangalia vipengele vya kesi vya kisheria vilivyowasilishwa na Bw Odinga.

Je mkuu wa tume ya uchaguzi alifanya jambo lisilofaa?

Sehemu muhimu ya kesi ya Raila Odinga inahusiana na nafasi ya Mwenyekiti wa Tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC), Wafula Chebukati.

AFP

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Maswali ya mlalamikaji yalihoji kuhusu vitendo vya mkuu wa tume ya uchaguzi Bw Wafula Chebukati

Sehemu muhimu ya kesi ya Raila Odinga kuhusu uchaguzi wa Kenya ni juu ya nafasi ya Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi na mipaka (IEBC), Wafula Chebukati.

Bw Odinga anasema kuwa asingepaswa kumtangaza William Ruto kama mshindi bila makubaliano na wengi wa makamishna wa tume , na hivyo “kutovuka ” majukumu yao ya kikazi.

Tunafahumu kuwa makamishna wanne kati ya saba hawakuunga mkono tangazo la matokeo ya uchaguzi wa urais.

Lakini kuna ufafanuzi tofauti wa mamlaka aliyonayo Bw Chebukati.

Baadhi ya wataalamu wanaamini kuwa chini ya tatiba ya Kenya, yeye pekee ndiye anayepewa mamlaka ya kutangaza matokeo ya uchaguzi wa urais, akifanya kazi kama msimamizi wa kura ya urais.

Pia wanaelezea ukweli kwamba anawajibika kisheria kufanya hivyo katika kipindi cha siku saba kuanzia tarehe ulipofanyika uchaguzi.

Hatahivyo, maoni mengine ya kisheria yanadai chini ya sheria ya IEBC ya 2011 IEBC, Bw Chebukati anaweza tu kutangaza kile ambacho kamishna “amejumlisha na kuthibitisha.”

Bw Odinga anadai hili halikutokea kwasababu ya kutoafikiana miongoni mwa makamishna.

Hiki ndicho Mahakama ya juu zaidi ya Kenya itatakiwa kutatua.

Je Bw Odinga yuko sahihi kuhusu utofauti wa idadi ya wapiga kura waliojitokeza kupiga kura?

Malalamiko ya kisheria ya Odinga pia yanasema idadi rasmi ya watu waliopiga kura ilitofautiana na asilimia iliyotolewa na maafisa wa uchaguzi ya idadi ya jumla ya wapiga kura waliojitokeza kupiga kura.

Wakenya wakiwa katika msururu wa kupia kura katika siku ya uchaguzi
Maelezo ya picha, Wakenya wakiwa katika msururu wa kupia kura katika siku ya uchaguzi
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Bw Chebukati awali alitangaza kujitokeza kwa 65.4% ya wapiga kura.

Bw Odinga anasema idadi hii ingemaanisha kuwa wapiga kura milioni 14.5 lazima wangepiga kura, kwa kuzingatia idadi ya jumla ya wapiga kura waliosajiriwa kupiga kura.

 Idadi rasmi ya mwisho ya kura halali ilikuwa ni milioni 14.2 (na hata kama ungeongeza kura zilizoharibika, ungepata kura takriban milioni 14.3 zilizopigwa). Kwahivyo timu ya mawakili wa Bw Odinga inadai kwamba "tume imeshindwa kuelezea kura zaidi ya 250,000 zilizopigwa katika uchaguzi wakiondolewa wapiga kura waliopiga kura kwenye karatasi ziko wapi ."

 Maelezo ya Odinga kwa kifupi ni sahihi. Hatahivyo anatumia numba (65.4%) kwamba Bw Chebukati muda mfupi baadaye alirekebisha na kuweka 64.6% - idadi ambayo ni sahihi inaoyoonyesha idadi kamili ya watu waliopiga kura.

 Kwhiyo Bw Odinga anaweza kudai kwamba kamishna awali alifanya makosa, lakini hili lilirekebishwa haraka na Bw Chebukati siku hiyo hiyo.

Idadi ya mwisho rasmi ya wapiga kura wali, baada ya idadi ya kura zote kupigwa na kuhakikiwa, ilikuwa ni 64.8% ya wapiga kura.

Je kulikuwa na utofauti wa kura katika ngazi ya mwanzo?

Katika siku ya uchaguzi, wapiga kura hawakuwa wanamchagua rais mpya tu. Walikuwa wanawachagua magavana, maseneta, wabunge na wawakilishi wa wanawake na wajumbe wa mabunge ya kaunti.

 Bw Odinga anasema kulikuwa na utofauti ausioelezeka katika jumla ya idadi ya kura zilizopigwa kwa ajili ya viti tofauti katika maeneo sawa.

 Kwa mfano, katika Kaunti ya Kirinyaga kati kati mwa Kenya, anasema watu 23,000 zaidi walipiga kura za rais kuliko kura za gavana, kulingana na idadi iliyofichuliwa na vyombo vya habari ambayo haijathibitishwa.

 Katika baadhi ya maeno, mawakili wa Bw Odinga wanadai kuwa kura za rais zilikuwa chache kuliko zile za viti vingine, jambo wanalosema "haliwezi kutokea katika mazingira ya kawaida."

 Utofauti wa idadi ya kura zilizogaribika unaweza kutokana na baadhi ya utofauti. Pia, wafungwa wanaruhusiwa kupiga kura ya kumchagua rais pekee – na sio wagombea wa viti vingine – lakini hilo lisingeleta tofauti kubwa.

 Inaweza kugeuka kuwa utofati usio muhimu, lakini kwa hatua hii haiwezekano kutambua haya kwasababu hakuna data zote kutoka katika tume ya uchaguzi