Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Napoli mbioni kumsajili Garnacho

Muda wa kusoma: Dakika 3

Napoli inamuwania Alejandro Garnacho, Aston Villa yakataa ombi la West Ham la kumsajili Jhon Duran, Manchester United wako mbioni kumsajili Patrick Dorgu kutoka Lecce na kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti anatarajiwa kuondoka majira ya joto.

Napoli wana matumaini ya kufikia mkataba wa pauni milioni 50 kumsaini winga wa Manchester United na Argentina Alejandro Garnacho, 20. (Corriere dello Sport, kwa Kiitaliano)

Ombi la West Ham la kumsajili Jhon Duran kwa pauni milioni 57 limekataliwa na Aston Villa, ambao wameamua kutomuuza mshambuliaji huyo wa Colombia mwenye thamani ya pauni milioni 80 katika kipindi hiki cha uhamisho wa wachezaji. (Telegraph - usajili unahitajika)

Manchester United wanajadiliana na beki wa Lecce Patrick Dorgu, kwa lengo la kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark mwenye umri wa miaka 20 kuziba pengo katika kikosi cha Ruben Amorim. (Athletic -usajili inahitajika)

United pia imemfuatilia beki wa Wolves na Algeria Rayan Ait-Nouri, 23, na beki wa wa Crystal Palace na England Tyrick Mitchell, 25, kwa kuhofia kumkosa mlinzi wa Paris-St Germain na Ureno Nuno Mendes, 22, katika uhamisho wa wachezaji Januari hii. (ESPN)

Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo majira ya kiangazi, huku kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso akipigiwa upatu kuchukua nafasi ya Muitaliano huyo. (Ondacero - kwa Kihispania)

Liverpool wanakabiliwa na mgogoro mpya wa kandarasi, huku beki wa Ufaransa Ibrahima Konate, 25, akiwa bado hajatia saini mkataba mpya na klabu hiyo licha ya kumepewa ofa mpya. (Telegraph - usajili unahitajika)

Kiungo wa Manchester City na England Jack Grealish, 29, ananyatiwa na Inter Milan na Borussia Dortmund, huku mustakabali wake Etihad ukizidi kutofahamika. (Sun)

Tottenham wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Ipswich Town Muingereza Liam Delap, 21, mwezi huu lakini huenda wakakabiliana na ushindani kutoka kwa Chelsea. (Team Talk)

Liverpool haina nia ya kupokea dau la kumuuza kiungo wa kati wa England c wa hini ya umri wa miaka 21 Harvey Elliott, 21, mwezi Januari au katika ahamisho wa majira ya kiangazi, licha ya kukosa kuchezea kikosi cha kwanza. (Football Insider)

Beki wa Hungary Milos Kerkez atasalia Bournemouth licha ya kuwaniwa na klabu ya Manchester United, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 huenda akahama wakati wa usajili wa majira ya kiangazi. (Florian Plettenberg, Sky Germany)

AC Milan wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Denmark wa Manchester United Rasmus Hojlund, 21, na mshambuliaji wao wa kimataifa wa Uholanzi Joshua Zirkzee, 23. (ESPN)

Juventus wamefanya mazungumzo na klabu ya Udinese kuhusu uhamisho wa beki wa Denmark Thomas Kristensen, 23, ambaye pia analengwa na Tottenham na Leicester City. (Mail)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi