Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Ijumaa: Man United kumnunua Karim Adeyemi kutoka Borussia Dortmund
Manchester United wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Ujerumani Karim Adeyemi, 23. (Bild - kwa Kijerumani, Subscription Required).
Chelsea wanaandaa dau la Euro 150m (£132m) kumnunua mshambuliaji wa Argentina Julian Alvarez, 25, kutoka Atletico Madrid msimu ujao. (Fichajes - In Spanish).
Kiungo wa kati wa Brazil na Wolves Joao Gomes, 24, pia anaangaliwa na Manchester United katika jitihada zao za kuimarisha nafasi yao ya nambari sita. (Mail - Subscription Required)
Liverpool na Tottenham wanamtazama mshambuliaji wa Bournemouth na Ghana Antoine Semenyo, 25, ili kuimarisha mashambulizi yao. (TeamTalks)
Kiungo wa kati wa Uingereza James Garner, 24, anasema "hajasikia lolote" na hakujakuwa na mazungumzo na Everton kuhusu kuongeza mkataba wake, ambao unamalizika msimu ujao wa joto. (FourFourTwo)
Newcastle United wanamtaka kiungo wa kati wa AZ Alkmaar Mholanzi Kees Smit, 19, ambaye pia anafuatiliwa na Barcelona, Bayern Munich, Borussia Dortmund na Real Madrid. (Mail - Subscription Required)
West Ham wamefufua nia yao ya kumnunua mlinzi wa Toulouse Charlie Cresswell, 23, ambaye amekuwa akichezea timu ya vijana ya Uingereza ya Under-21. (Sportsport)
Brentford, Everton na Leeds wanamwinda Daizen Maeda, 28 wa Celtic, huku mshambuliaji huyo wa Japan akitamani kuhama Januari kutoka Scotland. (TeamTalks)
Roma wanataka kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee kwa mkopo kutoka Manchester United mwezi Januari lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Everton, West Ham, Juventus na PSV Eindhoven. (Mirror)
Manchester United wamemtambua mlinda lango wa Malmo raia wa Uswidi Melker Ellborg, 22, kama mbadala wa Mbelgiji Senne Lammens, 23. (Sun).
Beki wa Manchester United Muingereza Harry Amass, 18, anatazamiwa kuendelea kwa mkopo Sheffield Wednesday zaidi ya dirisha la uhamisho la Januari. (Express),
Wolfsburg wameweka nia ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa West Ham na Ujerumani Niclas Fullkrug, 32, na beki wa kati wa Brentford na Norway Kristoffer Ajer. (Sky Sport News)
Kocha wa Brazil Carlo Ancelotti amekanusha kuwa alimwambia mshambuliaji wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 19, Endrick, ambaye anakaribia kujiunga na Lyon kwa mkopo, kwamba alilazimika kuihama klabu hiyo ya Uhispania ili kupata nafasi ya kukipiga katika kikosi chake kwa ajili ya Kombe la Dunia la 2026. (AS - In Spanish)
Beki wa Ecuador Willian Pacho, 24, ametia saini mkataba wa nyongeza na Paris St-Germain ambao utaendelea hadi 2030. (RMC Sport - In French).