Je, harufu pekee inatosha kujua chakula kilichoharibika?

Chanzo cha picha, Getty Image
Vijidudu katika chakula vinaweza kusababisha ugonjwa hata kama hakuna harufu. Lakini watu wengi hawana uhakika jinsi ya kujua ikiwa harufu ni nzuri au mbaya.
Ni kweli kwamba baadhi ya vijidudu hutoa harufu mbaya. Harufu mbaya hutokea wakati vijidudu vinapokuwa kwa haraka, hutumia kaboni na vitu vingine kama chanzo cha nishati. Lakini vijidudu aina ya listeria na salmonella, ambao husababisha magonjwa ya chakula, ni vigumu kugundua kwa kunusa tu.
Hatari pia ni ndogo ikiwa bakteria wa aina hiyo wako katika kiwango cha chini katika chakula. Zaidi ya hayo, ikiwa harufu yoyote ya bakteria ni ndogo kuliko harufu ya chakula, kuna uwezekano mdogo wa kusababisha matatizo ya afya hata ikiwa wako katika chakula.
Kutokana na matumizi ya viungo vya chakula, wakati mwingine ni vigumu kugundua bakteria kwa harufu. Bakteria wa salmonella wanaoweza kusababisha ugonjwa, pia wanaweza kupatikana katika maji machafu.

Chanzo cha picha, Getty Image
Chakula kinaweza kugunduliwa kuwa kimeharibika, ikiwa kimeachwa muda mrefu bila kuhifadhiwa vizuri na kupelekea bakteria kukila. Kipimo cha kunusa ni muhimu katika kupunguza upotevu wa chakula kwa kutambua chakula kilichoharibika na sio kutupa chakula kizima.
Hata hivyo, baadhi ya vyakula, harufu mbaya haisababishwi na kuwepo kwa bakteria katika chakula. Pia, sababu za baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na chakula kuharibika bado hazijajulikana. Ingawa inajulikana kuwa katika kuwa bakteria wengine husababisha ugonjwa, bado kuna mengi ambayo hatujui.
Hata hivyo, hali inaboreka katika suala hili ikilinganishwa na siku za nyuma. Wanasayansi wanapata vifaa ambavyo ni sahihi zaidi kuliko pua zetu ili kugundua bakteria wanaokuwa kwenye chakula.
Vilevile, badala ya kutumia pua kunusa wakati chakula unachokula kikionekana kuwa kibaya, ni bora kukihifadhi eneo linalofaa na kuchukua muda unaohitajika kukipika.















