Mtanzania atengeneza mfumo wa kusafisha maji taka yanayozalishwa nyumbani kwake
Mtanzania atengeneza mfumo wa kusafisha maji taka yanayozalishwa nyumbani kwake
Kijana wa Kitanzania Jimson Julius ametengeneza mfumo wa kusafisha maji taka yote yanayozalishwa kwenye nyumba yake kutokana na shughuli mbalimbali ikiwemo haja ndogo na kuyatumia tena kwa shughuli za kilimo kwenye bustani zake
Mfumo huo ambao unajumuisha mpangilio maalumu wa mawe, changarawe, mkaa, mchanga udongo na mizizi ya mimea unamuwezesha kufanya kilimo kwa mwaka mzima
Mwandishi wa BBC @eagansalla_gifted_sounds alikutana naye na kuandaa taarifa hii



