Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je, kisiwa hiki kidogo cha Mauritius ni kituo cha siri cha ujasusi?
Arnaud Poulay hakutaka kuondoka katika kisiwa kidogo cha Bahari ya Hindi cha Agalega, lakini mwaka huu alipakia begi lake na kuondoka, akiwa amevunjwa moyo na kile alichokiona kama kuifanya nyumba yake kuwa ya kijeshi.
Hadi hivi karibuni ni watu 350 tu waliishi Agalega, wakivua samaki na kufanya kilimo cha nazi. Chakula kingine kililetwa mara nne kwa mwaka na meli kutoka mji mkuu wa Mauritius, uliopo kilomita 1,100 (maili 680) kuelekea kusini. Ndege ndogo ilikuwa nadra kutumika isipokuwa kwa dharura za kimatibabu.
Lakini mwaka 2015, taifa dogo la Mauritius ambalo kisiwa cha Agalega ni sehemu yake lilitia saini makubaliano ya kuiwezesha India kujenga barabara kubwa ya mita 3,000 na kivuko cha baharini kama sehemu ya ushirikiano wa nchi hizo mbili katika suala la usalama wa baharini.
Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa Agalega wanahofia kuwa hali hii inaweza kusababisha uwepo mkubwa wa jeshi.
Bwana Poulay, mwenye umri wa miaka 44 na mwanamuziki wa reggae, aliongoza kampeni dhidi ya mradi huo.
"Ninapenda kisiwa changu na kisiwa changu kinanipenda," anasema. "Lakini wakati kituo cha kijeshi kilipozinduliwa, nilijua kuwa nilipaswa kuondoka."
Agalega - visiwa viwili vidogo vinavyofunika kilomita za mraba 25, kusini-magharibi mwa Bahari ya Hindi - itakuwa eneo bora kwa India kufuatilia trafiki ya baharini. Na kulinganisha picha za satelaiti kutoka 2019 na zingine zilizochukuliwa Julai mwaka huu inaonyesha ni kiasi gani kimebadilika.
Zulia la miti ya mitende limetengeneza njia ya barabara, ambayo inaenea kando ya mgongo wa kisiwa cha kaskazini kati ya vijiji viwili vikuu - La Fourche kaskazini na Vingt-Cinq kusini zaidi.
Majengo mawili ya mita 60 yanaweza kuonekana kando ya lami, angalau moja mojawapo likiwa ni jengo la ofisi ya ndege ya P-8I ya India, kulingana na Samuel Bashfield, msomi katika chuo kikuu cha taifa cha Australia.
P-8I ni ndege aina ya Boeing 737 iliyobadilishwa kuwinda na uwezekano wa kushambulia submarines, na kufuatilia mawasiliano ya baharini. Wasafiri wa kisiwa hicho tayari wamepiga picha ndege hiyo kwenye uwanja wa ndege.
"Wakati picha mpya za satelaiti zikipatikana, tutaelewa vyema jukumu la Agegaga katika mawasiliano ya Bahari ya Hindi," anasema.
Taasisi ya Kimataifa ya Mafunzo ya Kimkakati inakitaja kituo hicho kama "kituo cha uchunguzi" na inasema kuwa kuna uwezekano wa kuwa na mfumo wa ufuatiliaji wa rada za pwani sawa na vifaa vilivyojengwa na India mahali pengine nchini Mauritius.
Serikali ya India ilikataa kujibu maswali kuhusu Agalega, na kuifanya BBC kutafuta taarifa zake za awali kwenye tovuti yake.
Katika moja ya taarifa hizi, Waziri Mkuu Narendra Modi alisema India na Mauritius ni "washirika wa asili" katika usalama wa baharini, wanakabiliwa na changamoto za jadi na zisizo za jadi katika eneo la Bahari ya Hindi.
Nchi hizo mbili zimekuwa na uhusiano wa karibu wa ulinzi tangu miaka ya 1970. Mshauri wa usalama wa taifa wa nchi hiyo, mkuu wake wa walinzi wa pwani na mkuu wa kikosi cha helikopta cha polisi wote ni raia wa India na maafisa katika shirika la ujasusi la nje la India, jeshi la majini na jeshi la anga.
Pande zote mbili zitataka kituo hicho kuonekana "kama moja vituo ambavyo ni zaidi ya kujenga uwezo kuliko matumizi yoyote ya kijeshi", anasema Profesa Harsh Pant, wa taasisi ya India katika taasisi ya King's London.
Hata hivyo, si siri kwamba India na washirika wake wa Magharibi wana wasiwasi juu ya kuongezeka kwa uwepo wa China katika Bahari ya Hindi.
Wakati si kawaida kwa nchi kubwa kuanzisha kituo cha kijeshi katika eneo la mshirika mdogo, kazi ya ujenzi wa Agalega imesumbua baadhi ya wakazi wa kisiwa.
Maeneo kadhaa, ikiwa ni pamoja na baadhi ya fukwe za kisiwa hicho, tayari yamefungwa, wakazi wa kisiwa hicho wanasema. Pia kuna uvumi unaoendelea kwamba kijiji cha La Fourche kitamezwa na miundombinu ya India ambayo inaendelea kuongezeka karibu nacho, na kwamba familia 10 zinazoishi huko zitalazimishwa kuhama.
"Litakuwa eneo lililozuiliwa kabisa kwa ajili ya Wahindi," anasema Laval Soopramanien, rais wa chama cha marafiki wa Agalega.
Anahofia kwamba "Agalega itakuwa hadithi ya visiwa vya Chagos" - wasiwasi ulioungwa mkono na Billy Henri, anasema mwanamke mwenye umri wa miaka 26, aliyefukuzwa kutoka visiwa vya Chagos.
"Mama yangu [alipoteza] kisiwa chake," anasema Henri. "Baba yangu atakuwa wa pili."
Wakazi kadhaa wa Agalega wanatoka katika familia zilizokumbwa na ufurushwaji kutoka visiwa vya Chagos, kilomita 2,000 mashariki, baada ya serikali ya Uingereza kuvitangaza mwaka 1965 kuwa eneo la Uingereza na kutoa ruhusa kwa Marekani kujenga kituo cha mawasiliano katika kisiwa hicho kikubwa zaidi, Diego Garcia. Hatua kwa hatua kikawa ngome kamili ya kijeshi.
Billy Henri anahofia kuwa serikali ya Mauritius, ambayo inamiliki ardhi yote katika eneo la Agalega na ndio mwajiri pekee, inajaribu kuweka masharti magumu kiasi kwamba kila mtu ataondoka.
Anataja matatizo ya huduma za afya na elimu, uwekezaji mdogo katika uchumi wa ndani, ukosefu wa fursa za ajira, na marufuku kwa watu wa ndani kufungua biashara zao wenyewe.
Msemaji wa serikali ya Mauritius ameiambia BBC kwamba hakuna mtu atakayeagizwa kuondoka, na kwamba watu wa eneo hilo walizuiwa tu kuingia uwanja wa ndege na bandarini - miundombinu ambayo alisema itasaidia nchi hiyo kudhibiti uharamia, usafirishaji wa madawa ya kulevya na uvuvi usiodhibitiwa.
Mauritius pia inakanusha madai kwamba Agalega ni mwenyeji wa kambi ya kijeshi, akisema kuwa polisi wa taifa hilo bado wanadhibiti kikamilifu. Hata hivyo, inakubali kwamba India itasaidia katika "uhifadhi na uendeshaji" wa vifaa vipya, ambavyo vilijengwa kwa gharama za India.
Wakazi kadhaa wa Agalega wanatoka katika familia zilizokumbwa na ufurushwaji kutoka visiwa vya Chagos, kilomita 2,000 mashariki, baada ya serikali ya Uingereza kuvitangaza mwaka 1965 kuwa eneo la Uingereza na kutoa ruhusa kwa Marekani kujenga kituo cha mawasiliano katika kisiwa hicho kikubwa zaidi, Diego Garcia. Hatua kwa hatua kikawa ngome kamili ya kijeshi.
Billy Henri anahofia kuwa serikali ya Mauritius, ambayo inamiliki ardhi yote katika eneo la Agalega na ndio mwajiri pekee, inajaribu kuweka masharti magumu kiasi kwamba kila mtu ataondoka.
Anataja matatizo ya huduma za afya na elimu, uwekezaji mdogo katika uchumi wa ndani, ukosefu wa fursa za ajira, na marufuku kwa watu wa ndani kufungua biashara zao wenyewe.
Msemaji wa serikali ya Mauritius ameiambia BBC kwamba hakuna mtu atakayeombwa kuondoka, na kwamba watu wa eneo hilo walizuiwa tu kuingia uwanja wa ndege na bandarini - vifaa ambavyo alisema vitasaidia nchi hiyo kudhibiti uharamia, usafirishaji wa madawa ya kulevya na uvuvi usiodhibitiwa.
Mauritius pia inakanusha madai kwamba Agalega ni mwenyeji wa kambi ya kijeshi, akisema kuwa polisi wa taifa hilo bado wanadhibiti kikamilifu. Hata hivyo, inakubali kwamba India itasaidia katika "uhifadhi na uendeshaji" wa vifaa vipya, ambavyo vilijengwa kwa gharama za India.
Serikali za Mauritius na India zinasema maboresho ya usafiri wa baharini na angani yalilenga kuwanufaisha wakazi wa kisiwa hicho na kusaidia kuwaondoa katika umaskini. Lakini wenyeji wanasema hili halijatokea: bado kuna feri nne tu kwenye kisiwa kikuu cha Mauritius kila mwaka, na hakuna ndege za abiria.
Waagalegan wanasema wamezuiwa kutibiwa katika hospitali mpya iliyojengwa na India, ingawa taarifa ya serikali ya Mauritius ilitoa majengo yake kwa ajili ya utoaji huduma za mashine za X-ray na vifaa vya matibabu ya meno.
Billy Henri anasema kuwa mvulana aliyeungua kwa mafuta ya ya kupikia, ambaye alihitaji msaada zaidi, alikataliwa kuingia kwenye hospitali hiyo mwezi Oktoba.
"Ni kwa Wahindi tu!" anasema.
Badala yake mtoto huyo aliyejeruhiwa alisafiri pamoja na wazazi wake hadi katika kisiwa kikuu cha Mauritius.
Laval Soopramanien anasema kuwa mtoto huyo bado yuko hospitalini na kwamba familia hiyo itasalia katika kisiwa hicho hadi boti ijayo itakapoondoka kuelekea Agalega.
Serikali ya Mauritius haikujibu, ilipotakiwa kutoa maoni juu ya hatma ya kijana huyo kwa kuchomwa moto. Serikali ya India imekataa kutoa maoni yake.
Katika hotuba yake ya hivi karibuni kwa bunge la Mauritius, Waziri Mkuu Pravind Jugnauth alisema maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Agalega ni ya juu kuliko wakati wowote katika ajenda ya serikali yake.
"Mpango mkuu" uliandaliwa ili kuboresha afya na elimu, uhusiano wa usafiri na vifaa vya burudani kwa wakazi wa kisiwa hicho, na kuendeleza sekta ya uvuvi na unyonyaji wa bidhaa za nazi, alisema.
Lakini kutoaminiana kunachochewa na ukweli kwamba sio India wala Mauritius ambayo imechapisha maelezo ya makubaliano ya 2015, kwa hivyo mipango yao ya siku zijazo haijulikani.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi