Tetesi za soka Ulaya Jumatatu: Modric njia panda Madrid na Uarabuni

Luka Modric

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Kiungo mkongwe wa Croatia Luka Modric, 39, bado hajapokea ofa ya mkataba mpya kutoka kwa Real Madrid na anaweza kuhamia klabu moja nchini Qatar. (Marca)

Arsenal wako tayari kulipa pauni milioni 17 (euro milioni 20) kumnunua mlinda mlango wa Espanyol Joan Garcia baada ya vilabu vya Serie A na Bundesliga kumnunua Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 23. (El Nacional)

Everton wamezungumza na wawakilishi wa kiungo wa kati wa Freiburg na Ujerumani Merlin Rohl mwenye umri wa miaka 22 kuhusu uwezekano wa kuhama. (Kicker)

Merlin Rohl

Chanzo cha picha, Getty Images

Real Madrid wamemtambua winga wa AC Milan na Ureno Rafael Leao, 25, kama mmoja kati ya watu watatu wanaoweza kuchukua nafasi iwapo wataamua msimu huu wa joto ni wakati wa kumuuza kiungo wa kimataifa wa Brazil Vinicius Jr. (Fichajes)

Arsenal na Liverpool wako tayari kuwa miongoni mwa timu kuu zinazojaribu kumsajili kiungo wa kati wa Crystal Palace na Uingereza Eberechi Eze, 26, msimu huu wa joto. (Caughtoffside)

Mkufunzi wa Newcastle Eddie Howe ni shabiki mkubwa wa mlinda lango wa Southampton Aaron Ramsdale na anafikiria kukifikia kipengele cha pauni milioni 25 kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 26. (Football Insider)

Aaron Ramsdale

Chanzo cha picha, Getty Images

Bournemouth itadai pauni milioni 40 kumnunua mlinzi wa kushoto wa Hungary Milos Kerkez, 21, ambaye yuko kwenye rada ya Liverpool, pamoja na mlinzi wa Fulham wenye thamani ya pauni milioni 50 na Mmarekani Antonee Robinson, 27. (Mirror)

West Ham wanapanga kufanyia marekebisho makubwa kikosi chao majira ya kiangazi, huku hadi wachezaji 10 waandamizi wakitarajiwa kuondoka London Stadium. (Football Insider)

Brighton na Bournemouth wote wanamfuatilia kiungo wa kati wa Bristol Rovers Kofi Shaw, 18. (Mail)

Newcastle wamefanya mawasiliano ya moja kwa moja na wakala wa mshambuliaji wa Fiorentina Moise Kean kuhusu uhamisho wa majira ya kiangazi, huku mshambuliaji huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 25 pia akizivutia Arsenal, Tottenham, AC Milan, Napoli na Barcelona. (Calciomercato)

Kean

Chanzo cha picha, Getty Images

Mkufunzi wa Real Madrid Carlo Ancelotti bado yuko tayari kwa wazo la kuwa kocha wa Brazil katika siku zijazo, lakini tu wakati muda wake huko Bernabeu utakapokamilika. (Relevo)

Kocha wa zamani wa Manchester United Erik ten Hag alionekana Roma kabla ya mechi ya Roma ya Serie A dhidi ya Juventus. Vilabu vyote viwili vinatazamia kuwa na meneja mpya katika majira ya joto. (Radio Mana Sport Roma)