Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vita vya Ukraine: Masaibu ya wanavijiji wanaokimbia maeneo ya mpakani
Wakati ndege za Urusi zilipoanza kushambulia kijiji chake cha mpakani kaskazini mwa Ukraine, Nina Skorkina alikataa kuondoka.
Lakini polisi waliamua kumhamisha ajuza huyo mwenye umri wa miaka 87, huku kukiwa na milipuko pande zote.
Katika siku za hivi majuzi, wazee wengine pia wamebebwa kwenye blanketi na kuvushwa daraja ambalo tayari limeharibiwa na mashambulio ya ndege.
Wakati Vladimir Putin anasherehekea kupata mhula mwingine wa miaka sita madarakani , mashambulizi ya mpakani yameongezeka kwa kasi.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema karibu mabomu 200 yamearushwa kwenye eneo la Sumy kaskazini mashariki mwa Ukraine mwezi huu pekee.
Anaishutumu Urusi kwa kujaribu kuchoma moto vijiji vya mpakani.
Polisi na wafanyikazi wa dharura sasa wameokoa mamia ya watu kutoka eneo la mpaka la Sumy, wakiwapeleka ndani zaidi ya Ukraine na kuwaweka salama.
Wengi ni kutoka kwa vijiji karibu na Velyka Pysarivka.
Nilisaidiwa na basi la shule la manjano wiki hii, Nina Makarenko anasema kuwa nyumba ambayo alilazimika kuondoka ilikuwa imeharibika.
"Walivunja nyumba zetu. Hakuna kitu kilichosalia," alisema.
Mashavu yake yalikuwa yameng'aa kwa blusher na midomo yake ilipakwa rangi, lakini Nina alichokuja nacho ni nguo chache na jamu ya kujitengenezea nyumbani.
Kabla ya vita, alikuwa akivuka kwenda Urusi mara kwa mara kwenda kufanya ununuzi. Sasa vikosi vya Urusi vinashambulia nyumba yake.
"Inatisha. Wanashambulia usiku na mchana."
Basi hilo linawapeleka waliohamishwa hadi mji mdogo wa Okhtyrka, ambapo mamlaka za eneo hilo zimegeuza shule ya chekechea na shule kuwa makazi ya muda.
Mlipuko uliofuata ni wa hasira dhidi ya Vladimir Putin - ambaye alianzisha vita hivi na ambaye sasa ametangazwa rasmi kuwa rais wa Urusi kwa muhula wa tano.
"Putin ni adui yetu! Anasema ataiangamiza Ukraine!" Tetiana anasema kwa shauku akidhihaki kuchaguliwa tena kwa kiongozi huyo wa Urusi. "Alijiteua mwenyewe!"
"Tulimfanyia nini? Lakini angalia watu wangapi wameuawa hapa, wangapi wameteswa. Ni watu wangapi wamepoteza mikono na miguu. Na kwa nini?"
Tetiana anapozungumza, mama yake mzee analia kando yake. Pande zote, karibu kila mtu ndani ya chumba analia.
Wanakijiji wengi wameacha eneo la mpaka wa Sumy tangu msimu wa joto uliopita kwani limekuwa hatari zaidi.
Sasa, haiwezekani kukaa. Picha zilizorekodiwa na polisi wa uokoaji zinaonyesha nyumba zikiwa zimeharibika kabisa
Sababu moja ambayo huenda imesababisha kuchacha kwa mashambulizi ni kuongezeka kwa mashambulizi ya Ukraine huko Belgorod, jiji kubwa zaidi la Urusi karibu na mpaka.
Vladimir Putin ameapa kujibu, akipuuza ukweli kwamba makombora ya Kirusi yamekuwa yakipiga nyumba na miundombinu ya umma nchini Ukraine bila kusita kwa miaka miwili.
Meya wa Okhtyrka ana nadharia nyingine ya kuongezeka kwa mashambulizi.
"Ninaelewa kwamba adui anataka kuunda aina fulani ya eneo ambapo vifaa vya kijeshi haviwezi kuingia na ambapo watu hawawezi kusonga kwa makundi makubwa," Pavlo Kuzmenko anasema.
Kwa sasa yuko katika maktaba ya mji kwa sababu ofisi zake mwenyewe zilikuwa zimeharibiwa na shambulio la kombora la Urusi.
"Katika mpaka wetu wote, adui anaunda hatua kwa hatua eneo ambalo Waukraine hawataweza kukanyaga," meya anaamini.
Kuna sababu nyingine ya kuongezeka kwa mabomu.
Kabla tu ya Vladimir Putin kurejea Kremlin, kundi la wapiganaji wa Urusi walitangaza uvamizi kutoka Ukraine - Kwenda kwa nchi yao wenyewe.
Wakiwa wanajiita "vikosi vya ukombozi" walitaka kuonyesha kuwa Bw Putin alikuwa amepoteza udhibiti wa mpaka wake. Hapo ndipo wanakijiji wanasema mashambulizi ya anga ya kijeshi kwenye Velyka Pysarivka yalianza.
Sio tu mapigano ambayo familia zinakimbia huko Sumy.
Eneo la kaskazini ndilo pekee linalovuka mpaka nchini humo kutoka Urusi, na kuifanya kuwa njia kuu ya Waukraine kutoroka.
Kila siku, makumi ya watu kutoka maeneo ambayo Urusi imedai kinyume cha sheria kama yake huvumilia safari ngumu kufikia eneo linalodhibitiwa na Ukraine.
Kremlin inasema watu wengi katika mikoa iliyokaliwa walijitokeza kumpigia kura Putin mwezi huu.
Lakini hiyo sio picha iliyotolewa na wale wanaofikia Sumy.
Wiki hii, Zoya Vypyraylo na mumewe Mykhailo walisafiri kwa muda wa siku tatu kutoka kijiji kilichoko kusini mwa mkoa wa Kherson ambao sasa umejaa askari wa Urusi.
"Kuna wengi huko, wako ndani ya nyumba. Wako mashambani. Magari yao yanatembea kotekote. Ilikuwa ya kutisha sana," Zoya alieleza, alipofika kituo cha mapokezi