Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Chelsea yamfuta kazi kocha wake Thomas Tuchel
Chelsea imemtimua meneja Thomas Tuchel kufuatia kichapo cha Jumanne usiku katika Ligi ya Mabingwa dhidi ya Dinamo Zagreb.
Kocha huyo wa zamani wa Borussia Dortmund na Paris St-Germain mwenye umri wa miaka 49 anaondoka Stamford Bridge baada ya miezi 20.
Mmiliki Todd Boehly amewaweka wakufunzi wa Tuchel kazini kwa muda hadi mtu mwingine atakapopatikana.
Tuchel aliteuliwa Januari 26, 2021, kuchukua nafasi ya Frank Lampard, na kuiongoza klabu hiyo kutwaa taji lao la pili la Ligi ya Mabingwa miezi minne tu baadaye.
Aliendelea kuongeza Uefa Super Cup na Fifa Club World Cup baadaye mwaka huo.
Taarifa kutoka kwa Chelsea inasema:
"Kwa niaba ya kila mtu katika Chelsea FC, Klabu ingependa kuweka rekodi ya shukurani zake kwa Thomas na wafanyakazi wake kwa juhudi zao zote wakati wakiwa na Klabu. Thomas atakuwa na nafasi katika historia ya Chelsea baada ya kushinda Ligi ya Mabingwa, Kombe la Super Cup na Kombe la Dunia la Klabu wakati wake hapa.
“Wakati kundi jipya la umiliki likifikisha siku 100 tangu kutwaa Klabu, na huku likiendelea na kazi kubwa ya kuipeleka klabu mbele, wamiliki wapya wanaamini ni wakati mwafaka wa kufanya mabadiliko haya,” inasema taarifa hiyo.
Chelsea imesema haitakuwa na maoni zaidi kuhusu suala hilo hadi uteuzi mpya wa kocha mkuu utakapofanywa.
Jinsi kiwango cha mchezo wa Chelsea kilishuka
Tuchel alianza vyema Chelsea, akishinda mechi nyingi walizocheza.
Lakini kiwango kilikuwa kimeshuka sana, huku klabu ikishinda mechi saba pekee kati ya 16 zilizopita za Ligi Kuu, kama takwimu hizi za Opta zinavyoonyesha.
Asilimia yake ya ushindi ilikuwa imeshuka kutoka zaidi ya 67% hadi 44% hivi majuzi.
Thomas Tuchel ni wazi hakuwa na furaha baada ya kushindwa kwa Mabingwa wa 1-0 na Dinamo Zagreb jana usiku. Alisema Blues walikuwa "wanakosa kila kitu" na kwamba "alikuwa na hasira juu yake mwenyewe".
"Tunahitaji kuwa bora zaidi. Hatujamaliza, hatuna furaha lakini nilifikiri tuko kwenye njia nzuri. Nashangazwa na uchezaji huu," aliongeza. Kweli, Chelsea pia wanakosa meneja.