Tunajua kuna tatizo la kutumika kwa watoto walemavu kwenye shughuli za ombaomba’-Tanzania yajibu ufichuzi wa BBC

Serikali ya Tanzania imekiri kuwepo kwa baadhi ya watu wanaofanya biashara haramu ya ulanguzi wa binadamu kwa kuwasafirisha watoto wenye ulemavu na kisha kuwatumikisha kwenye shughuli mbalimbali ikiwemo 'ombaomba'.

Hata hivyo Serikali inaendelea na juhudi za kutoa elimu, kuwatambua walemavu na kuongeza ulinzi katika mipaka ili kuhakikisha biashara hiyo inakomeshwa.

Alexander Lupilya ndiye Mkuu wa Utafiti na Takwimu katika Sekretarieti ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu Tanzania