Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
BBC Africa Eye: Ufichuzi wa watoto wa Kitanzania wanaopelekwa Kenya kuwa ombaomba mitaani
Uchunguzi wa BBC Africa Eye umefichua mtandao wa magendo ya binadamu unaosafirisha watoto walemavu kutoka Tanzania hadi Kenya. Wengi huchukuliwa kutoka kwa wazazi wao kwa ahadi ya maisha bora. Lakini badala yake, watoto wanalazimika kuomba-omba mitaani – mara nyingi kwa miaka mingi – huku watekaji wao wakichukua faida yote. Africa Eye ilimsaidia mwathirika mmoja kutoroka. Njeri Mwangi anaripoti kutoka Nairobi.