Jinsi mwanamke alivyomuingiza kimagendo mtoto mchanga Uingereza

Newborn baby in travel seat

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Sanchia Berg
    • Nafasi, News correspondent
    • Author, Tara Mewawalla
    • Nafasi, BBC News
  • Muda wa kusoma: Dakika 5

Mwaka jana majira ya kiangazi, mwanamke mmoja alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Gatwick alipowasili tu kutoka Nigeria akiwa na mtoto mchanga wa kike.

Mwanamke huyo alikuwa akiishi West Yorkshire na mume wake na watoto, na kabla ya kuondoka Uingereza kuelekea Afrika alikuwa amemwambia daktari wake kuwa ni mjamzito.

Lakini imebainika kuwa hakusema ukweli.

Mwanamke huyo aliporejea mwezi mmoja baadaye akiwa na mtoto huyo, alikamatwa kwa tuhuma za ulanguzi wa binadamu.

Kesi hiyo, ya pili ambayo BBC imefuatiliwa katika Mahakama ya Familia katika miezi ya hivi karibuni, inafichua kile ambacho wataalam wanasema ni mwelekeo unaotia wasiwasi wa watoto wachanga kuletwa Uingereza kinyume cha sheria - baadhi kutoka kwa kile kinachoitwa "viwanda vya watoto" nchini Nigeria.

'Watoto wangu hufichwa kila wakati'

Mwanamke huyo, ambaye tunamwita Susan, ni Mnigeria, lakini amekuwa akiishi Uingereza tangu Juni 2023, pamoja na mume wake na watoto.

Susan alidai kuwa alikuwa mjamzito. Lakini uchunguzi na vipimo vya damu vilionyesha kuwa hiyo haikuwa kweli. Badala yake, uchunguzu ulibaini kuwa Susan alikuwa na uvimbe, ambao madaktari walihofia kuwa unaweza kuwa wa saratani. Lakini alikataa matibabu.

Susan alisisitiza kwamba mimba zake za awali hazikuonekana kwenye vipimo, akimwambia mwajiri wake kuwa, "watoto wangu hufichwa kila mara". Pia alidai kuwa alibeba ujauzito wa hadi miezi 30 kabla ya kujifungua watoto wake wengine.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Susan alikuwa amezuru Nigeria mwanzoni mwa Juni 2024, akisema kuwa alitaka kujifungulia mtoto wake huko, lakini baadaye akawasiliana na hospitali yake nchini huko Uingereza, kusema kuwa amejifungua.

Madaktari walikuwa na wasiwasi na kuwasiliana na huduma za watoto.

Aliporudi Uingereza na mtoto wa kike - ambaye tunamwita Eleanor - Susan alizuiliwa na kukamatwa na Polisi wa Sussex.

Alipewa dhamana na jeshi la polisi linaloendesha kesi hiyo likithibitisha kuwa hakuna uchunguzi wa kina ulifanywa kuhusiana na hilo.

Baada ya kukamatwa, Susan, mume wake, na Eleanor walifanyiwa vipimo vya chembechembe za vinasaba (DNA). Na hapo ndipo mtoto Eleanor alipelekwa katika nyumba za ulezi.

"Matokeo yatakapothibitihsa poonyesha kuwa mimi ni mama yake Eleanor, nataka arejeshwe mara moja," Susan alisema.

Lakini vipimo vilionyesha mtoto huyo hakuwa na uhusiano wa uzazi na Susan au mumewe. Susan alitaka vipipo kurejelewa mara ya pili - ambao ulitoa matokeo sawa, na hapo ndipo alibadilisha maelezo yake.

Alisema kuwa alifanyiwa IVF (kubebewa ujauzito) kabla ya kuhamia Uingereza mnamo 2023 lakini yeye na mume wake walichangia yai na manii, alisema, na ndiyo sababu vipimo vya DNA vilikuwa hasi.

Susan aliwasilisha barua kutoka kwa hospitali ya Nigeria, iliyotiwa saini na mkurugenzi wa matibabu, akisema alijifungua huko, pamoja na hati kutoka kwa kliniki nyingine kuhusu matibabu ya IVF ili kuthibitisha madai yake.

Pia alitoa picha na video ambazo alisema zilimuonyesha akiwa katika chumba cha kujifungua cha hospitali ya Nigeria. Hakuna sura inayoonekana kwenye picha hizo na moja ilionyesha mwanamke aliyekuwa uchi akiwa kondo katikati ya miguu yake, huku kitovu kikiwa bado kimefungwa.

Leeds magistrate & Family Court

Chanzo cha picha, Alamy

Kuna mtu aliyejifungua - lakini sio Susan

Mahakama ya kifamilia mjini Leeds ilimtuma Henrietta Coker kufanya uchunguzi .

Bi Coker, ambaye hutoa ripoti za kitaalamu kwa mahakama za familia katika kesi kama hizi, ana tajriba ya takriban miaka 30 kama mfanyakazi wa kijamii. Alipata mafunzo nchini Uingereza, na amekuwa mstari wa mbele wa ulinzi wa watoto huko London, kabla ya kuhamia Afrika.

Bi Coker alitembelea kituo cha matibabu ambapo Susan alidai kuwfanyiwa IVF. Hakukuwa na rekodi ya Susan kutibiwa hilo - wafanyakazi walimwambia barua hiyo ilikuwa ya kughushi.

Alipotembelea mahali ambapo Susan alidai kujifungulia mwanawe alipata ghorofa iliyochakaa, yenye vyumba vitatu vya kulala, na kuta "zilizobadilika" na mazulia "chafu".

Katika jengo hilo Bi Coker alikutana na "wasichana watatu matineja walioketi kwenye chumba cha mapokezi wakiwa wamevaa sare za wauguzi".

Alipoomba kusema na msimamizi wao "akaelekezwa jikoni ambapo alimuona msichana akila wali".

Kutoka hapo Bi Coker alifuatilia na kumpata daktari aliyemuandikia Susan barua ya kusema kuwa alijifungulia katika hospitali hiyo. Alipoulizwa alisema , "Naam, kuna mtu aliyejifungua".

Bi Coker alimuonyesha picha ya Susan, lakini haikuwa yeye, daktari huyo alisema.

"Suala la watu kutoa taarifa za uongo wakitumia majina ya watu wengine ni jambo la kawaida katika eneo hilo la dunia," alimwambia Bi Coker, akiashiria kuwa Susan huenda "amenunua mtoto".

Henrietta Coker ana tajiriba ya miaka kadhaa kama mhudumu wa kijamii

Chanzo cha picha, Supplied

Maelezo ya picha, Henrietta Coker ana tajiriba ya miaka kadhaa kama mhudumu wa kijamii

Visa vya watoto "kuibwa" vimeshamiri sana Afrika magharibi, Bi Coker baadaye aaliifahamisha mahakama. Kuna takriba makazi 200 ya "watoto" ambayo yamefungwa na mamlka za Nigeria katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, alisema.

Baadhi yalikuwa na wasichana wadogo ambao walikuwa wametekwa nyara, kubakwa na kulazimishwa kujifungua mara kwa mara.

"Wakati mwingine wasichana hawa huachiwa huru," Bi Coker alisema, "nyakati nyingine hufa wakati wa kujifungua, au kuuawa na kuzikwa katika makaburi ya umma."

Haijulikani mtoto Eleanor alitolewa wapi? - ingawa daktari alimwambia Bi Coker kuwa anaamini kwamba alitolewa kwa hiari.

Bi Coker hakuweza kubaini wazazi halisi wa Eleanor ni akina nani.

Alitoa ushahidi kwa Mahakama ya Familia huko Leeds mwezi Machi mwaka huu, pamoja na Susan, mume wake, mwajiri wake na daktari mkuu wa uzazi.

Katika kikao cha awali hakimu aliomba simu ya Susan ichunguzwe. Wachunguzi walipata jumbe ambazo Susan alikuwa amemtumia mtu fulani zimehifadhiwa katika anwani yake ya simu kama "Mum oft [sic] Lagos Baby".

Pregnant woman, Lagos, Nigeria

Chanzo cha picha, Getty Images

Takriban wiki nne kabla ya tarehe ambayo Susan alidai kujifungua aliandika ujumbe mfupi wa maandishi uliosomeka:

"Habari za mchana mama, sijaona vitu vya hospitali"

Siku hiyo hiyo, Mum Oft Lagos Baby alijibu:

"Dawa ya kujifungua ni 3.4 m

"Bili ya hospitali 170k."

Kwa kuchukulia kuwa pesa hizo ni Naira ya Nigeria, zitakuwa katika eneo la £1,700 na £85 mtawalia, hakimu wa Mahakama ya Familia, Rekoda William Tyler KC alisema.

Ikiwa hela hizo ni za sarafu ya Nigeria, basi ni £1,700 hadi £85 mtawalio, mratibu wa jaji wa mahakama ya William Tyler KC alisema.