BBC Africa Eye: Kenya yaukamata mtandao wa wezi wa watoto

Kenya

Polisi nchini Kenya imesema kuwa imebaini mtandao unaohusika na wizi wa watoto katika jiji la Nairobi nchini Kenya.

Sakata hii imebainika baada ya kipindi cha uchunguzi cha BBC Africa Eye kupeperushwa hewani ambacho kilionesha uhalifu unaotendeka katika maeneo mbalimbali na hospitali za umma.

Maafisa watatu wa matibabu wa hospitali za umma wamekamatwa na polisi na imedokeza kuwa bado kuna wengi ambao wanatafutwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Inspekta Generali wa polisi Hillary Mutyambai, ilisema uchunguzi na taarifa kutoka kwa washirika umeonesha maafisa waandamizi wa matibabu wanahusika kwa kiasi kikubwa na wizi wa watoto.

Mamlaka imehaidi kuboresha ulinzi wa watoto.

Katika mkutano na waandishi wa habari serikali iliweka wazi kuwa wahusika wa biashara hiyo haramu - wauzaji na wanaonunua - watafikishwa katika mikono ya kisheria.

Waziri wa kazi na masuala ya jamii, Simon Chelugui, alisema uchunguzi wa uhalifu huo unaendelea.

Alisema ni muhimu kuboresha huduma ya usalama kwa watoto, serikali haiwezi kuvumilia vitendo hivi vya kinyama.

Maelezo ya video, Uchunguzi wa BBC wabaini watoto wanaotoka katika mazingira magumu Kenya wanauzwa

BBC Africa Eye iliingia kwenye safu ya mitandao haramu, ikishuhudia watoto wakiibiwa kutoka kwa mama wasio na makazi na kuuzwa mitaani kwa kima cha dola za Kimarekani 450.

Mtoto wa kiume anaweza kuuzwa kwa dola 3000 za kimarekani. Lakini biashara hii ya kusikitisha haishii hapo.

Pia uumebainika ushahidi wa watoto waliozaliwa wakiuzwa katika kliniki haramu, na watoto waliotelekezwa wakiuzwa na wafanyikazi wa afya katika hospitali ya Mama Lucy Kibaki jijini Nairobi. Usimamizi wa hospitali haukujibu madai hay