Urusi na Ukraine: Silaha nzito za kisasa za magharibi zaizuia Urusi kupiga hatua Donbas

Silaha za mataifa ya magharibi zaanza kuzaa matunda Ukraine

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Silaha za mataifa ya magharibi zaanza kuzaa matunda Ukraine

Wanajeshi waliopo katika mstari wa mbele katika eneo la mashariki mwa Ukraine wanasema kwamba silaha nzito kutoka kwa mataifa ya magharibi zimezuia mashambulizi ya Urusi ya mara kwa mara . lakini je huu ni utulivu wa muda mfupi au ishara kwamba wimbi la mzozo huo linabadilika?

Moshi ulipenya katika anga karibu na mlima kaskazini mwa eneo la Bakhmut , mji wa kilimo uliotorokwa kutokana na mashambulizi ya Urusi ya wiki kadhaa.

''Haya sio Maisha kwetu. Hakuna eneo lililopo salama. Natamani maisha yangu yangeisha'', alisema Anna Ivanova bibi mwenye umri wa miaka 86, akizama kwa usaidizi wa fimbo yake kuondoa magugu kutoka katika bustani yake , huku ndege mbili za kivita za Ukraine zikipaa chini chini angani.

Dakika kumi baadaye , msururu wa milipuko mitano ama hata zaidi ilishuhudiwa katika shamba la alizeti .

Bakhmut

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wakaazi wanatembea mbele ya nyumba ilioharibiwa na makombora , huku Urusi ikiivamia Ukraine katika eneo la Bakhmut tarehe 13 mwezi Juni.

Mji wa Bakhmut umekabiliwa na mashambulizi kwa wiki kadhaa sasa. Kwa mtu yeyote anayeendesha gari karibu na eneo la mstari wa mbele la mashambulizi mashariki mwa Donbas – kutoka mji ulioharibiwa wa Slovyansk kaskazini , hadi katika vijiji vya wakulima vilivyotorokwa karibu na Donetsk kusini – inaonekana mashambulizi ya Urusi yamekuwa yakiendelea.

Lakini kona moja ya shamba moja la ngano nje ya mji wa Donetsk, kamanda wa kitengo cha silaha nzito za Ukraine ambaye alitaka kujulikana tu kwa jina lake la kwanza , Dmitro alikana.

''Hawashambulii kama ilivyokuwa awali. Kiwango cha mashambulizi ya Urusi kimeshuka maradufu. Pengine hata zaidi na pengine hata kwa thuluthi mbili'', alisema kando ya gari moja kubwa la rangi ya kijani.

.

Gari hilo - kipande cha silaha kinachojiendesha chenye pipa kubwa linaloelekeza kusini kuelekea eneo linaloshikiliwa na Urusi - ni Kaisari aliyetengenezwa na Ufaransa, mojawapo ya idadi inayoongezeka ya silaha za kisasa za Magharibi ambazo sasa zinaweza kuonekana zikisonga kwenye njia za nchi kote Donbas. Dmitro, na wengine wengi hapa, wanaamini wanasaidia kubadilisha hali dhidi ya Urusi.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kwa mlipuko unaoweza kuharibu maskio , Kaisari alifyatua kombora la kwanza kati ya matatu kwa kile Dmitro alisema kilikuwa kitengo cha askari wa miguu wa Urusi na vipande kadhaa vya mizinga umbali wa kilomita 27 (maili 16).

"Sisi sasa tuna usahihi wa kulenga shabaha . Na tunaweza kuwashambulia kutoka mbali zaidi," alisema, kwa grin. Ndani ya dakika moja, kikosi cha vifaru kilikuwa kimerusha makombora mengine mawili, na gari lilikuwa tayari likisogea, kwa kasi, kabla ya mizinga ya Urusi kupata nafasi ya kulifuatilia na kutekeleza mashambulizi.

Katika wiki za hivi karibuni raia na wanajeshi wa Ukraine wametazama, mara nyingi kwa furaha, huku kanda za ndege zisizo na rubani na video zingine zilizopakiwa kwenye mtandao zikionekana kuonyesha mfululizo wa milipuko mikubwa katika eneo linaloshikiliwa na Urusi.

Inaripotiwa kote kwamba haya ni maghala makubwa ya silaha yaliyofichwa , lakini sasa yanaweza kufikiwa na silaha mpya za Magharibi zilizowasili, zikiwemo zile za Himars kutoka marekani na Polish Krab howwitzers.

"Sikiliza ukimya huo," alisema Yuri Bereza, jamaa mwenye ndevu mwenye umri wa miaka 52 anayeongoza kitengo cha kujitolea kilichopewa jukumu la kutetea Sloyansk. Kwa zaidi ya saa moja hakuna mlipuko hata mmoja uliosikika.

"Hiyo yote ni kwa sababu ya silaha ulizotupa - kwa sababu ya usahihi wake," alisema Bereza. "Hapo awali, Urusi ilikuwa na mapipa 50 ya bunduki kwa kila tuliyokuwa nayo. Sasa ni zaidi kama tano kwa moja. Faida yao sasa ni ndogo."

Lakini Bereza, kama Dmitro, alisisitiza kuwa Ukraine ilihitaji zaidi silaha za Magharibi ili kutekeleza mashambulizi yenye ufanisi. Yuri Bereza, ni kamanda wa kujitolea wa kitengo kinachotetea Eneo la Slovyansk, mashariki mwa Ukraine

.
Maelezo ya picha, Yuri bereza anasema kwamba silahaza za magharibi zimewezesha wanajeshi wa Ukraine kuweza kukabili uwezo wa Urusi Kijeshi.

"Hawawezi kutushinda , hatuwezi kuwashinda hapa. Tunahitahi silaha zaidi , hususan, vifaru na ndege. Bila hivyo vitu wengi watapoteza Maisha yao. Hivyo ndivyo Urusi inavyopigana. Hawajali kuhusu Maisha ya binadamu," said Bereza.

‘’Ukweli ni kwamba tunahitaji mara tatu ya silaha ambazo zimetumwa na matifa ya magharibi na haraka sana’’, alithibitisha Dmitro.

Lakini ukosefu wa silaha sio jambo pekee linaloweza kuzuia azma ya Ukraine ya kukomboa eneo lililotekwa. Licha ya kupungua kwa mashambulizi ya mabomu ya Urusi, vikosi vya Kremlin vinaendelea kusogea karibu na mji wa kimkakati wa Bakhmut, na kuzua wasiwasi miongoni mwa vikosi vya Ukraine kuhusu ukosefu wa ukosefu wa silaha na mafunzo.

"Hapa kuna ujanja rahisi," alisema mtu mmoja, akiwa amelala kwenye njia ya uchafu na kuelekeza bunduki yake, akiwa amezungukwa na askari arobaini wa Ukraine waliokuwa makini.

"Inua mguu wako hivi," alisema mtu huyo, askari wa miavuli wa zamani wa Uingereza, ambaye alikuwa sehemu ya kikundi cha kibinafsi kinachotoa msaada kwa brigedi ya Kiukreni ambayo ilikuwa imewasili hivi karibuni kuimarisha wanajeshi walio mstari wa mbele.

Waukraine wote walikuwa watu wa kujitolea, na walikuwa na miezi michache tu ya mafunzo ya kimsingi. Makamanda wao walikuwa wamefikia makubaliano yasiyo rasmi na wakufunzi wa Magharibi, kwa kozi ya siku tano.

"Bila shaka, inatisha. Sijaona vita hapo awali," kamanda wa kitengo hicho mwenye umri wa miaka 22, wakili, ambaye aliomba tusitumie jina lake.

"Kinachotia wasiwasi ni ukweli kwamba watu hawa…wanakosa ujuzi wa kimsingi wa kijeshi ambao nchi za Magharibi zimezoea," alisema mkufunzi mwingine, Rob, mwanajeshi wa zamani wa Marekani.

Kundi la wapiganaji wa Mozart waliojitolea
Maelezo ya picha, Kundi la wapiganaji wa Mozart waliojitolea

Mashirika ya kibinafsi yanafanya kazi kwa uhuru mashariki mwa Ukraine, pamoja na kundi la Mozart

Kwa sasa, serikali za Magharibi zimekataa kutuma maafisa, au wanakandarasi, nchini Ukraine kusaidia katika kuajiri wanajeshi na juhudi za mafunzo. Mashirika machache ya kibinafsi yanafanya kazi hapa, kwa kujitegemea.

Alisisitiza kuwa kundi lake la Mozart lilikuwa na mawasiliano "sifuri" na, au kuungwa mkono na serikali ya Marekani, lakini aliyakosoa mataifa ya Magharibi kwa "kufifia" na "kutoona macho" kukataa kujihusisha moja kwa moja zaidi.

"Ni ujinga. Lakini watu hawa wamepoteza watu wengi kiasi kwamba hawana [walimu wa kutosha wa Kiukreni]," alisema. "Mataifa ya Magharibi yanahitaji kupanga hilo sasa."