Ukraine na Urusi: Fahamu ‘' eneo hatari zaidi kwa mataifa ya Ulaya’’

Chanzo cha picha, Getty Images
Ni ukanda wa ardhi ulioko kati ya Lithuania na Poland na kutokana na mvutano unaoongezeka kati ya Moscow na Magharibi, baadhi ya wafafanuzi wameeleza eneo hilo kuwa ‘’mahali hatari sana kwa Ulaya’’.
Ni ukanda wa Suwalki, upanuzi wa takriban kilomita 70 kwa urefu unaounganisha Belarus, mshirika mkuu wa Moscow, na Kaliningrad, eneo la Urusi lililowekwa Ulaya.
Hivi karibuni ukanda huo ulikuwa na mvutano mkubwa baada ya vikwazo ambavyo Umoja wa Ulaya (EU) iliweka katika kukabiliana na uvamizi wa Ukraine, Urusi kupigwa marufuku kusafirisha baadhi ya bidhaa zake kwenda Kaliningrad kupitia humo.
Sasa baadhi ya wachambuzi wanaonya kwamba eneo hilo linaweza kuwa moja ya shabaha za kwanza za Rais wa Urusi Vladimir Putin ikiwa ataamua kuzidisha vita vya Ukraine hadi makabiliano ya wazi na NATO.
‘’Kwa hakika hii ni (a) hali ya hatari. Kwa sababu ingezuia NATO kufikia mataifa ya Baltic na hivyo kuruhusu Urusi kujiunga na mataifa hayo pia,’’ mtaalam huyo anaongeza.
Ni kwa sababu ya urahisi wa kiasi ambao Urusi inaweza kukamata ukanda wa Suwalki na kwamba kwa muda mrefu imekuwa ikichukulia kuwa eneo dhaifu kwa NATO.
Eneo hilo, ambalo ni kama halijakaliwa na watu linalojumuisha hasa mabwawa, barabara kuu mbili na njia moja ya reli, inawakilisha umbali mfupi zaidi kati ya Kaliningrad na Belarus.
Kufuatia kuanguka kwa Umoja wa Kisovyeti, Shirikisho la Urusi lilishikilia Kaliningrad.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Lakini eneo hilo lenye wanajeshi wengi sasa lilikuwa upande wa pili wa Lithuania na Poland, likiwa limetengwa na Urusi na mshirika wake Belarus.
Licha ya majaribio ya mara kwa mara ya Urusi katika miaka ya 1990 kupata eneo ambalo lingeruhusu uwepo wa kijeshi unaoendelea kati ya Belarusi na Kaliningrad, juhudi zote zilishindwa.
Ilikuwa ni mwaka wa 2003 tu, wakati Poland na Lithuania zilipokuwa zikijadiliana juu ya kujiunga na Umoja wa Ulaya, ambapo Urusi ilifikia mkataba wa jumla zaidi ambao uliruhusu usafiri wa abiria na bidhaa kupitia ukanda kati ya Lithuania na Poland.
Umuhimu wa kimkakati hapo awali, hatari ya ukanda, ulipewa jina la jiji la Kipolishi la Suwalki, na kukaribia kutotambuliwa.
Lakini wakati majimbo ya Baltic ya Lithuania, Estonia na Latvia yalipojiunga na NATO, ukanda huo ulichukua umuhimu mkubwa wa kimkakati.
Eneo lake lilimaanisha kuwa Kaliningrad ilizungukwa na mataifa ya NATO.
Lakini pia, ukanda uliunda kizuizi kwa muungano wa kijeshi, na kuwa chanzo cha kuwepo kwa udhaifu - kwa shirika.
‘’Ukanda kati ya Kaliningrad na Belarus kwa hakika ni kikwazo, sio tu kwa masharti madhubuti ya kijeshi, lakini pia katika suala la vifaa kwa msaada wa NATO kwa vikosi vya Estonia, Latvia na Lithuania,’’ Profesa Kenton anaiambia BBC Mundo.
‘’Kwa sababu ikiwa Warusi wangefunga ukanda huo wa kijeshi, na pia kuweka kizuizi cha majini kwenye Baltic, basi NATO ingeachwa katika hali ngumu sana ya jinsi ya kusambaza hata vifaa vya msingi, chakula na mafuta kwa majimbo matatu ya Baltic.’’ anaongeza.
Msimamo wa kimkakati wa ukanda huo, na uwezekano wa Urusi kuliteka eneo hilo, ulizidi kuwa muhimu zaidi baada ya Moscow kutwaa eneo la Crimea mwaka 2014.
Na wachambuzi wengi waliona uwezekano huo kuwa karibu zaidi baada ya Urusi kuivamia Ukraine mwezi Februari mwaka huu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Eneo lenye wanajeshi wengi
Kwa uhakika, kwa NATO, eneo hilo lilikua muhimu vya kutosha kuweka jopo kazi linaloongozwa na Marekani huko Orzysz, Poland, karibu na mpaka wa Lithuania.
Na tangu 2014 hali ya kijeshi katika eneo hilo imeongezeka kwa kasi na silaha imeongezeka sana kwa pande zote mbili.
Mvutano katika eneo hilo ulifikia viwango vipya mnamo Juni wakati Lithuania ilipiga marufuku usafirishaji wa chuma na metali zingine zenye chuma kupitia ukanda wa Suwalki kutokana na vikwazo vilivyowekwa na EU juu ya uvamizi wa Ukraine.
Mnamo Julai, Lithuania iliondoa marufuku hiyo, lakini uamuzi wa awali ulichochea hasira ya Moscow, ambayo ilitishia kujibu kizuizi hicho na kulaani vikwazo hivyo kuwa haramu na visivyokubalika.
Mkuu wa baraza la usalama la Urusi, Nikolai Patrushev, alitishia ‘’athari mbaya kwa idadi ya watu wa Lithuania’’.
Utekaji mwingine wa Urusi?
Kizuizi cha Kilithuania kilifufua hofu ya kuingizwa kwa Urusi kwa ukanda wa Suwalki.
Lakini si wataalamu wote wanaoamini kwamba Moscow iko tayari kuchukua hatua hiyo wakati majeshi yake yanapohusika katika uvamizi wa Ukraine.
‘’Nadhani haiwezekani sana,’’ anasema Profesa Stephen Hall.
‘’Urusi inaweka uwezo wake mwingi (wa kijeshi) nchini Ukraine, ambapo haijafanya kazi ya kipekee’’.
Ni vita vya ugomvi. Inapiga hatua, lakini itaendelea kuwa ngumu zaidi na zaidi kupata uimarishaji na kufanya uamuzi mgumu wa kuimarisha Donbas kujaribu kuwaondoa Waukraine au kuondoka (miji mingine) wazi kwa mashambulizi ya kukabiliana’’.

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini zaidi ya hayo, ikiwa majeshi ya Urusi yangekamata ukanda huo, ambao ni eneo la NATO, hiyo ingesababisha makabiliano ya mara moja kati ya Urusi na wanachama wa muungano huo.
Kwa sababu hatua yoyote ya Urusi katika eneo la Poland au Lithuania ingesababisha matumizi ya Kifungu cha 5 kinachosema kwamba shambulio dhidi ya mwanachama wa NATO linawakilisha shambulio kwa mataifa yote washirika.
Kama Stepehn Hall anavyosema, Urusi ‘’haiwezi kumudu kuendeleza vita ambavyo vitaleta NATO karibu na uwezo wake kamili.’’
Lakini je, Washington, London na wanachama wengine wa muungano huo wangekuwa tayari kuingilia kati makabiliano na Urusi kuhusu eneo lisilo na watu wengi?
Mkurugenzi mwenza wa Kituo cha Masuala ya Vita katika Chuo Kikuu cha Reading, Kenton White, haamini kwamba wanachama wote wa NATO wako tayari kufanya hivyo
‘’Itakuwa vigumu sana kwa Warusi, hata kwa msaada wa Belarus, (kuchukua ukanda huo) kwa sababu NATO imekuwa ikituma wanajeshi zaidi katika eneo hilo, lakini kama hali hiyo ingetokea, kungekuwa na baadhi ya nchi za NATO ambazo huenda wasiwe tayari kukabiliana na vikosi vya Urusi moja kwa moja, bila kujali Kifungu cha 5.’’
‘’Nafikiria nchi kama Ujerumani, Ubelgiji, labda Denmark, huenda zisiwe tayari kuhusika katika hali kama hiyo.’’
Ni lazima ikumbukwe kwamba huko Kaliningrad, Urusi imeanzisha uwepo wa kijeshi wa kutisha ambao unajumuisha meli zake za Baltic, makumi ya maelfu ya wanajeshi na kumekuwa na ripoti kwamba imepeleka silaha za nyuklia katika eneo la karibu watu milioni.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kama Kenton White anavyoelezea, Kifungu cha 5 cha NATO hakisemi kwamba wanachama lazima watoe nguvu za kijeshi, na zaidi, ‘’kuna hisia kali miongoni mwa baadhi ya wanachama wa NATO kwamba makabiliano ya kijeshi ni kitu ambacho wanataka kuepuka kwa gharama yoyote.’’
Kuimarishwa kwa Finland na Uswidi ukweli ni kwamba, kama profesa katika Chuo Kikuu cha Reading anasema, ukanda huo kwa sasa ni ‘’mahali pa hatari sana kwa watu wa Ulaya na kwa hakika ni tishio kwa NATO.’’
Na kwa matarajio ya NATO kujiunga na Uswidi na Finland kumeongeza mvutano kati ya Urusi na Magharibi.
Kujumuishwa kwa nchi hizo mbili za Skandinavia kutageuza Bahari ya Baltic kuwa kile ambacho baadhi ya wachambuzi wanakiita ‘’ziwa la NATO’’.
Na hii inaweza labda kutoa motisha kubwa zaidi kwa Moscow kujenga ‘’daraja’’ kati ya Belarusi na Kaliningrad.
Lakini wataalam wanasema kuwa Sweden na Finland zikiwa wanachama wa NATO, ukanda wa Suwalki hautakuwa tena sehemu dhaifu katika muungano huo wa kijeshi.
Pamoja na Finland kutakuwa na njia ya moja kwa moja kuelekea mataifa ya Baltic, ambayo haipatikani kwa sasa. Kwa hiyo ukanda huo hautakuwa tena tishio kubwa kwa utendakazi wa NATO’’.
‘’Kwa hakika tunapaswa kuwa na wasiwasi juu ya nia ya muda mrefu ya Putin kuelekea NATO na ukanda huo unaweza kuwa mahali pazuri.’’
Lakini kujiunga kwa Finland na Uswidi kutapunguza hofu juu ya eneo hilo na kuweka usawa wa eneo hilo kwa faida ya NATO,’’ mtaalam huyo anasema.












