Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa nini makombora ya urani iliyorutubishwa hutumiwa na yana madhara gani?
Urusi imeionya Uingereza kutosambaza makombora ya urani yaani uranium iliyorutubishwa kama silaha kwa vifaru inavyotuma Ukraine, ikisema kuwa yana "jumuisha nyuklia".
Madini ya Urani yaliyorutubishwa hufanya silaha kuwa na nguvu zaidi, lakini kuna wasiwasi kwamba silaha hizi ni tishio kwa watu wanaoishi katika maeneo ambayo hutumiwa.
Urani ‘Uranium’ iliyorutubishwa ni nini?
Urani iliyorutubishwa ni uranium ya asili ambayo imeondolewa makali sana - lakini sio yote - ya nyenzo zake za mionzi.
Ni uchafu au dutu unaotokana na mchakato wa kurutubisha madini ya uranium kwa matumizi ya vinu vya nyuklia na silaha za nyuklia.
Kwa nini baadhi ya silaha hutumia urani iliyorutubishwa?
Kwa kuwa uranium ni metali nene sana, urani iliyorutubishwa inaweza kutumika kuimarisha silaha za vifaru.
Inaweza pia kuwekwa kwenye ncha za risasi, na makombora ya mortar ili kupenya kwenye silaha za kawaida za kivita.
Makombora ya urani yaliyorutubishwa huwa na athari na hivyo kuongeza uwezo wao wa ulinzi dhidi ya silaha, na huwaka inapogusana.
Silaha za urani iliyorutubishwa imetumika wapi?
Kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Uingereza, makombora ya urani iliyorutubishwa yalitengenezwa na Marekani na Uingereza katika miaka ya 1970.
Zilitumika kwa mara ya kwanza katika Vita vya Ghuba mwaka wa 1991, kisha Kosovo mwaka wa 1999 na katika Vita vya Iraq mwaka 2003.
Ni silaha gani za urani iliyorutubishwa zinatumwa Ukraine?
Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema inapatia wanajeshi wa Ukraine makombora ya uranium iliyorutubishwa kutumika pamoja na vifaru 14 vya Challenger 2 inazotuma Kyiv.
Makombora haya yatawaruhusu wahudumu wa vifaru wa Ukraine kufyatua shabaha za adui kutoka umbali mrefu zaidi, na hivyo kupunguza uwezekano wao wa kujibu kwa kurusha silaha.
Afisa wa Ikulu ya Marekani ameliambia shirika la habari la AP kwamba Urusi pia ina akiba ya silaha za uranium zilizorutubishwa, ingawa haijafahamika iwapo ilizitumia nchini Ukraine.
"Makombora ya urani yaliyorutubishwa hayazingatiwi kuwa silaha za nyuklia," anasema Dk Marina Miron, wa Chuo cha Kings London.
"Hazikusudiwi kuwatia watu sumu. Zinatumika kwa sababu ya uwezo wao wa kukabiliana na uharibifu wa makombora."
Silaha za urani zilizorutubishwa zina hatari gani?
Uranium iliyorutubishwa ina mionzi kidogo.
"Tunahofia kwamba makombora ya urani yaliyorutubishwa, yakianguka chini, yatachafua kwa kuacha dutu", aeleza Dk Miron. "Ndio maana Marekani na washirika wake wa NATO walileta utata walipozitumia huko Kosovo."
Mnamo mwaka 2007, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliamuru mapitio ya athari za kiafya za silaha hizo, na mashirika ya kimataifa yamefanya mapitio mengine kadhaa.
Kamati ya Kisayansi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Athari za Mionzi ya Atomiki (UNSCEAR) imehitimisha kuwa kuathiriwa na uranium iliyorutubishwa hakusababishi sumu kubwa.
Hata hivyo, Shirika la Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) linasema kunaweza kuwa na hatari ya mionzi kwa watu wanaojihusisha moja kwa moja na vipande vya makombora ya urani iliyorutubishwa.
Utafiti uliochapishwa katika jarida la Uchafuzi wa Mazingira mnamo 2019 unapendekeza kunaweza kuwa na uhusiano kati ya utumiaji wa silaha za urani iliyorutubishwa na kasoro za kuzaliwa huko Nasiriyah, Iraqi.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Upokonyaji Silaha pia ina wasiwasi kuwa "katika mazingira ya baada ya vita, kuwepo kwa mabaki ya urani iliyorutubishwa kunaweza kuongeza wasiwasi wa wakazi wa eneo hilo".
Katika ripoti iliyochapishwa mwaka wa 2022, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) lilionyesha wasiwasi wake kuhusu uwezekano wa matumizi ya urani iliyorutubishwa nchini Ukraine, kwani inaweza kusababisha "kuwashwa kwa ngozi, kushindwa kwa figo kufanya kazi na kuongeza hatari ya saratani".
"Sumu ya kemikali ya urani iliyorutubishwa inaonekana kama tatizo kubwa kuliko athari zinazowezekana za mionzi yake.
Hilo linaweza kuongeza wasiwasi wa watu wa eneo hilo."
Je, silaha za urani iliyorutubishwa ni halali?
Wizara ya Ulinzi ya Uingereza inasisitiza kwamba makombora ya urani iliyorutubishwa inayotuma Ukraine hayajapigwa marufuku na makubaliano yoyote ya kimataifa.
Inadai kuwa chini ya Kifungu cha 36 cha Itifaki ya Kwanza ya 1977 ya nyongeza ya Mikataba ya Geneva ya 1949, makombora ya urani yaliyorutubishwa ya Uingereza "yana uwezo wa kutumika halali katika vita vya kimataifa vyenye kuhusisha silaha".
Rais Vladmir Putin ameonya kwamba iwapo Uingereza itapeleka makombora ya urani yaliyorutubishwa Ukraine, "Urusi itabidi ichukue hatua ipasavyo, kwani nchi za Magharibi tayari zimeanza kwa pamoja kutumia silaha zenye kujumuisha vipengele vya nyuklia".
Wizara ya Ulinzi ilijibu katika taarifa: "Jeshi la Uingereza limekuwa likitumia uranium iliyorutubishwa katika makombora yake kwa ajili ya kuzuia silaha kushambuliwa kwa miongo kadhaa. Urusi inajua hili, lakini inajaribu kupotosha kwa makusudi."
Hata hivyo, Bw. Miron anaamini kuwa kutuma makombora ya uranium yaliyorutubishwa kunaweza kuleta madhara kwa Ukraine na washirika wake:
"Matumizi ya makombora haya yanaiwezesha Urusi kutumia silaha zake za nyuklia na kutishia kutumia mojawapo ya vipengele vyake," anaeleza.