Msanii Eric Omondi: Asilimia 5 katika muswada wa fedha itauwa sekta ya waundaji maudhui

Nchini Kenya, wabunge wamerekebisha mapendekezo ya nyongeza ya baadhi ya kodi tata, huku muswada huo ukipita bungeni baada ya kusomwa kwa mara ya pili siku ya Alhamisi na sasa unasubiriwa kusomwa kwa mara ya tatu na kupitishwa au kupingwa.

Nchini Kenya, wabunge wamerekebisha mapendekezo ya nyongeza ya baadhi ya kodi tata, huku muswada huo ukipita bungeni baada ya kusomwa kwa mara ya pili siku ya Alhamisi na sasa unasubiriwa kusomwa kwa mara ya tatu na kupitishwa au kupingwa. Baadhi ya marekebisho ya kodi ni katika mapato yanayotokana na mitandao, ambapo kodi hiyo sasa ikupunguzwa kutoka asilimia 15% iliyopendekezwa hadi asilimia 5%. Lakini wasanii wa kutengeneza maudhui mitandaoni wamelichukuliaje suala hilo? Mwandishi wa BBC Roncliffe Odit amezungumza na mcheshi Eric Omondi kuhusu hili.

Lakini wasanii wa kutengeneza maudhui mitandaoni wamelichukuliaje suala hilo? Mwandishi wa BBC Roncliffe Odit amezungumza na mcheshi Eric Omondi kuhusu hili.