Uimara wa England na Hispania kuelekea fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake

Jumapili hii Uingereza na Uhispania zitacheza katika mechi ambayo haijawahi kutokea, kwenye Uwanja wa Australia mjini Sydney katika fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake. Ni mara ya kwanza kwa timu zote mbili kufika fainali ya Kombe la Dunia.

Uhispania ilifika fainali baada kuifunga timu ya Sweden mabao 2-1. England ikiishinda Australia 3-1 siku ya Jumatano.

Waingereza, wakiongozwa na meneja wa Uholanzi, Sarina Wiegman walifanikiwa kutinga hatua ya makundi kwa ushindi dhidi ya China (6-1), Haiti (1-0) na Denmark (1-0). Katika hatua ya 16 na robo fainali walipata upinzani mkubwa dhidi ya Nigeria na Colombia.

Kwa upande mwingine, Uhispania imekuwa moja ya timu zenye msimamo mzuri katika mashindano hayo. Imepoteza mchezo mmoja tu, dhidi ya Japan. Katika mechi ya mwisho ya hatua ya makundi.

Je, Uhispania inaweza kuwashinda mabingwa wa Ulaya na kutawazwa mabingwa wa dunia kwa mara ya kwanza?

England

Ubora wao unatokana na wachezaji wake. England ya wanawake ilikuwa mabingwa wa kombe la Ulaya 2020, waliifunga Ujerumani kwenye fainali. Hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa na ubora wa wachezaji wanaotamba katika Ligi Kuu ya Wanawake nchini Uingereza na ligi nyingine barani Ulaya.

Kwa mfano, Keira Walsh, anachezea FC Barcelona, inahesabiwa kuwa moja ya timu bora zaidi barani Ulaya. Mshambuliaji mchanga wa Brighton, Katie Robinson na mchezaji Lauren James. Hawa wote ni wachezaji wazuri.

Aidha, James, ambaye hakuwepo kwenye michezo miwili baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kucheza rafu kwenye mechi dhidi ya Nigeria, atakuwepo kwenye fainali. England ilipata ushindi katika mech zote za makundi.

Sarina Wiegman

Sarina Wiegman wa Uholanzi ameshinda karibu kila mechi kama kocha katika ngazi ya timu ya taifa. Kazi yake ya kwanza ni katika nchi yake Uholanzi. Alipata ushindi dhidi ya Denmark katika fainali ya Ulaya 2017, mojawapo ya mataji bora zaidi katika soka la nchi yake.

Miaka miwili baadaye, Wiegman alikaribia kushinda Kombe la Dunia la Wanawake - 2019 huko Ufaransa, lakini alishindwa na Marekani kwenye fainali. Kisha akaajiriwa kama meneja wa England na hapo akafika tena kileleni na kushinda Kombe la Ulaya - 2022.

Moja ya uwezo wake ni kusoma mchezo kama ilivyotokea wakati wa robo fainali ya Ulaya 2022 dhidi ya Hispania. Wiegman aliamua kubadili mfumo wake wa 4-3-3, akaweka ule wa hatari zaidi uliokuwa na walinzi watatu pekee 3-4-3.

Hatimaye alifanikiwa kwenda nusu fainali.

Uhispania

Ubora wa wachezaji wa timu ya soka ya Uhispania ni mkubwa vilevile, viungo Alexia Putella na Aitana Bonmatí ni wachezaji vijana ambao ni mabingwa wa dunia katika ngazi ya chini ya miaka 17 na 20. Lakini zaidi ni ustadi wao, wa kutokata tamaa.

Licha ya kipigo cha mabao 5-0 dhidi ya Japan katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi, Hispania imeonyesha nia yake ni kutwaa ubingwa bila kujali ni timu gani imewekwa mbele yao.

Kisha ikacheza na Uholanzi katika mchezo huo mgumu, ilikuwa bila bila hadi dakika 90. Walifanikiwa kuweka mambo sawa kwa bao la, Salma Paralluelo wakati wa dakika za nyongeza. Dhidi ya Sweden, historia ilijirudia, sare ikajirudia ya bilabila wakati dakika zimesalia chache. Lakini tena, Paralluelo aliweka mambo sawa.

Salma Paralluelo

Hakuna kitu ambacho kocha anataka zaidi ya mshambuliaji wake kufunga mabao. Na Uhispania, hivi sasa, ina mmoja wa wachezaji kwenye safu ya kufunga. Salma Paralluelo na Jumapili hii anaweza kutawazwa kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya soka la wanawake kushinda kombe la dunia la U-17, U-20 na wakubwa.

Binti huyu mchanga, mwenye miaka 19, amekuwa na mvuto mkubwa katika Kombe la Dunia ambalo hufanyika Australia na New Zealand. Na labda talanta hiyo itaipa Uhispania taji la kwanza la ulimwengu.