Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kombe la Dunia la Wanawake: Rekodi 4 ambazo wanawake wamewazidi wanaume kwenye Kombe la Dunia la soka
Ingawa michuano hii kwa wanawake ilianza hivi majuzi - kwa mara ya kwanza ilifanyika mwaka wa 1991 nchini China - michuano ya kombe la dunia la soka kwa wanawake imekuwa matukio ya kimataifa.
Na kupitia mashindano hayo, wachezaji wa soka wanafikia rekodi na mafanikio ambayo yamesalia kuandikwa katika vitabu vya historia vya mchezo huu.
Utawala wa Marekani - ikiwa na kutwaa mataji manne ya ulimwengu-, kiwango cha kushangaza cha timu za Asia (Japan ilikuwa bingwa wa dunia na mshindi wa pili, China ilishika nafasi ya pili mnamo 1999) na ufanisi wa Ulaya ukiongozwa na nchi za Nordic na England zimekuwa sehemu za kushangaza za mashindano haya.
Bila shaka, ulinganisho - ambao kila mara unachukiza - kati ya michuano hii ya wanwake na ile ya kombe la dunia la soka ya wanaume hauepukiki, lakini kwa namna ya kipekee mashindano ya wanawake yamekuwa ya kishujaa na makubwa ya aina yake ukilinganisha na ya wanaume, na mashujaa kama Marta, Nadine Angerer au Formiga wamevunja rekodi za wanaume.
BBC tunakuletea rekodi zinazoshikiliwa na wanawake katika mashindano ya dunia ya soka.
1. Mabao 17 ya Kombe la Dunia
Marta Viera Silva ni Mbrazil. Kwa wanwake yeye ni gwiji wa soka.
Na ni kwa sababu kadhaa: Mosi alichaguliwa kwa miaka sita kama mchezaji bora wa mpira wa miguu duniani kwa upande wa wanawake, ndiye mfungaji bora wa muda wote wa timu yake na ameshiriki katika Kombe la Dunia mara tano.
Lakini pengine kwa kile kitakachobakia milele katika vitabu vya historia ya soka ni kwamba amefunga mabao 17 katika Kombe la Dunia, rekodi ambayo hakuna mwanasoka mwingine yoyote, mwanamume au mwanamke, ameifikia.
Marta, ambaye ni mzaliwa wa Dois Riachos -mji ulioko mashariki mwa Brazil-, anawapita magwiji kama Mjerumani Miroslav Klose, ambaye alifunga mabao 16 katika Fainali nne za Kombe la Dunia alizoshiriki.
Linapokuja suala la soka nchini mwake, pia anampita Ronaldo Nazario de Lima, pengine mchezaji bora wa Brazil katika historia nyuma ya Pele, ambaye alifanikiwa kufunga mabao 15 katika michuano minne ya Kombe la Dunia ambayo alishiriki.
Alama nyingine ambayo Mbrazil huyo amaeiweka ni ile ya kuwa mwanasoka wa kwanza kufunga katika michuano mitano tofauti ya Kombe la Dunia, rekodi ambayo ilifikiwa na Cristiano Ronaldo katika michuano iliyopita, Qatar 2022.
Marta anatarajiwa kuwa sehemu ya timu itakayoshiriki Kombe la Dunia huko Australia na New Zealand ambapo ataweza kuongeza zaidi rekodi hii, ambayo itakuwa vigumu kwa wenzake wa kiume kufikia.
2. Michuano saba ya dunia ya Formiga
Labda jina la Miraildes Maciel Mota si maarufu sana... lakini tukitaja Formiga, jina la utani, tunajua kwamba tunamzungumzia mchezaji anayepamba kurasa za takwimu duniani.
Mbrazil huyo, ambaye ana umri wa miaka 45 na bado anachezea Sao Paulo katika ligi ya daraja la kwanza, ana rekodi kadhaa kwa sifa zake: yeye ndiye mchezaji mzee zaidi kufunga katika Kombe la Dunia (alikuwa na umri wa miaka 37 alipofanya hivyo) na ndiye mwenye umri mkubwa zaidi kushiriki Kombe la Dunia (miaka 41 nchini Ufaransa 2019).
Lakini hiyo ni katika michuano ya Kombe la Dunia kwa wanawake tu, kwa sababu Formiga inabeba rekodi nyingine ya ajabu kwenye mabega yake: amecheza katika michuano saba ya Kombe la Dunia , ambayo hakuna mchezaji wa soka kwenye sayari amefanikiwa kufikia hadi sasa.
Alicheza michuano ya Sweden 1995, Marekani 1999 na 2003, China 2007, Ujerumani 2011, Canada 2015 na Ufaransa mwaka 2019.
Mbali na yeye wanawake hawa wamecheza michuano mitano ya dunia; Mjerumani Birgit Prinz na Mmarekani Kristine Lilly.
Lakini, Lilly anashikilia rekodi nyingine ya Kombe la Dunia: amecheza jumla ya mechi 30. Anafuatiwa na Formiga mwenye mechi 27 na Mjerumani Lothar Matheus mwenye 25.
Katika mashindano ya wanaume Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, Lothar Matheus, Antonio Carbajal, Rafa Márquez na Andrés Guardado wamecheza fainali tano za Kombe la Dunia.
Ingawa Formiga hayumo kwenye kikosi kitakachocheza Kombe la Dunia huko Australia na New Zealand, ukweli ni kwamba rekodi yake tayari imewekwa kwa herufi za dhahabu kwenye sayari ya mpira.
3. Ushindi mkubwa zaidi (13-0)
Asubuhi ya Juni 11, 2019, wachezaji wa timu ya taifa ya Thailand walikuwa na wakati mgumu: wanaingi kucheza michuano yao ya pili ya Kombe la Dunia katika historia yao na mpinzani wake wa kwanza katika mashindano hayo ya pili alikuwa Marekani ambaye ni taifa gwiji kwa soka la wanawake.
Kitu ambacho Thais labda hawakuwahi kufikiria ni jinsi mechi hiyo ingeisha: walichapwa 13-0, ushindi mkubwa zaidi katika historia ya mashindano ya kombe la dunia.
Lakini, zaidi ya yote, tofauti kubwa zaidi ya mabao katika michuano yote ya dunia .
Mabao yalifungwa na Alex Morgan mabao 5, Samantha Mewis na Rosel Lavelle mabao mawili kila mmoja. Megan Rapinoe , Lindsey Horan, Mallory Pugh na Carli Lloyd kila mmoja alifunga bao moja kukamilisha matokeo ya mwisho.
Ushindi huo tayari umevunja rekodi nyingine iliyokuwa ikishikiliwa na wanawake: ya mabao 11-0 ambayo Ujerumani ilikuwa imeichapa Argentina katika Kombe la Dunia la mwaka 2007 nchini China.
Rekodi hizo zinaipita ile iliyowekwa na wanaume ambayo ni ushindi wa 10-1 ambao Hungary iliupata dhidi ya El Salvador katika Kombe la Dunia la mwaka 1982 huko Hispania au ule wa 9-0 ambayo Yugoslavia iliichapa Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) huko Ujerumani mnamo 1974.
4. Ubingwa bila kuruhusu bao
Kitu cha kawaida kwenye soka kuwa timu ina ukuta mzuri, na ulinzi bora ni ushambuliaji mzuri. Lakini hakuna kocha au mchezaji anayeweza kukwepa jaribu la kujigamba kuwa aliweza kufanikiwa kushinda mashindano bila kuruhusu bao.
Katika historia ya mashindano ya dunia ya wanaume, hakuna timu ambayo imefanikiwa kutwaa ubingwa bil kuruhusu bao.
Angalau Ufaransa mnamo 1998, Italia mnamo 2006 na Uhispania mnamo 2010, zilikuwa na rekodi nzuri ya kuruhusu mabao machache, timu zao ziliruhusu mabao mawili pekee wakati wa michuano ya Kombe la Dunia walioishia kutwaa kombe hilo.
Hata hivyo, kwa wanawake kuna timu ambayo imetawazwa bingwa wa soka duniani bila kuruhusu bao hata moja: Ujerumani, katika michuano ya nchini China mwaka 2007.
Kipa wa timu hiyo, Nadine Angerer, alikuwa na mengi ya kufanya, ambaye kwa kushangaza alikuwa kipa wa akiba, alianza kucheza kwa sababu siku chache kabla ya mashindano kuanza, kipa aliyekuwa namna moja aliumuia.
Angerer alifanikiwa kuweka rekodi ya kutopoteza mechi na kuruhusu bao iliyowekwa na Ujerumani na hata aliokoa mkwaju wa penalti kutoka kwa Marta kwenye fainali, ambayo iliisha kwa Teutons kushinda taji.