Ushindi wa Trump unamaanisha nini kwa Ukraine, Mashariki ya Kati na China

Muda wa kusoma: Dakika 5

Kurudi kwa Donald Trump ikulu kunatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika sera za mambo ya Nje za Marekani katika maeneo mengi nyeti, huku vita na wasiwasi vikiwa vinaikumbua dunia.

Wakati wa kampeni yake, Trump alitoa ahadi za kisera, mara nyingi bila maelezo maalumu, kwa kuzingatia kanuni za kutoingilia kati na kulinda biashara au kama anavyoiweka "Marekani Kwanza".

Ushindi wake unaashiria uwezekano wa kuchafuliwa kwa sera za kigeni za Marekani kwa miaka mingi wakati huu wa migogoro mbalimbali inayoendelea duniani.

Unaweza kusoma

Urusi, Ukraine na Nato

Wakati wa kampeni, Trump alisema mara kwa mara kwamba anaweza kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine "kwa siku moja". Alipoulizwa jinsi gani, alisema kwa kusimamia mpango huo, lakini hakutoa maelezo zaidi.

Utafiti ulioandikwa na wakuu wawili wa zamani wa usalama wa taifa wa Trump mwezi Mei ulisema Marekani inapaswa kuendeleza usambazaji wake wa silaha kwa Ukraine, lakini kuweka msaada huo uwe na masharti ya Kyiv kuingia katika mazungumzo ya amani na Urusi.

Ili kuishawishi Urusi, nchi za Magharibi ziliahidi kuchelewesha kuingia kwa Ukraine katika NATO. Washauri wa zamani walisema Ukraine haipaswi kukata tamaa ya kupata eneo lake lote lililodkutoka kwa uvamizi wa Urusi, lakini inapaswa kujadiliana kwa kuzingatia mstari wa mbele wa sasa.

Wapinzani wa Trump wa chama cha Democratic, wanaomtuhumu kwa kujihusisha na Rais wa Urusi Vladimir Putin, wanasema mbinu yake ni sawa na kujisalimisha kwa Ukraine na itahatarisha Ulaya yote.

Amesema mara kwa mara kipaumbele chake ni kumaliza vita na kumaliza uchakavu wa rasilimali za Marekani.

Haijulikani wazi jinsi utafiti huo wa washauri wa zamani unavyowakilisha mawazo ya Trump mwenyewe, lakini kuna uwezekano wa kutupa mwongozo wa aina ya ushauri atakaoupata.

Nato sasa ina nchi wanachama 32 na Trump kwa muda mrefu amekuwa mkosoaji wa muungano huo.

Ikiwa kweli ataiondoa Marekani kutoka Nato, ambayo itaaashiria mabadiliko makubwa zaidi katika uhusiano wa ulinzi wa Atlantiki katika karibu karne moja, bado ni suala la mjadala.

Baadhi ya washirika wake wanapendekeza kwamba msimamo wake mkali ni mbinu ya mazungumzo ya kuwafanya wanachama kufikia miongozo ya matumizi ya ulinzi ya muungano.

Lakini ukweli ni kwamba viongozi wa Nato watakuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu ushindi wake unamaanisha nini kwa mustakabali wa muungano huo na jinsi athari yake ya kuzuia inachukuliwa na viongozi wenye uhasama.

Mashariki ya Kati

Sawa na Ukraine, Trump ameahidi kuleta "amani" Mashariki ya Kati, akimaanisha kuwa atamaliza vita vya Israel na Hamas huko Gaza na vita vya Israel na Hezbollah nchini Lebanon, lakini hajasema ni kwa namna gani.

Amekuwa akisema mara kwa mara kwamba, kama angekuwa madarakani badala ya Joe Biden, Hamas isingeishambulia Israel kwa sababu ya sera yake ya "shinikizo la juu" dhidi ya Iran, ambayo inafadhili kundi hilo.

Kuna uwezekano Trump amejaribu kurejea kwenye sera hiyo, ambayo ilishuhudia utawala wake ukiiondoa Marekani katika mkataba wa nyuklia wa Iran, kuweka vikwazo zaidi dhidi ya Iran na kumuua Jenerali Qasem Soleimani, kamanda wa kijeshi mwenye nguvu zaidi wa Iran.

Katika Ikulu ya White House, Trump alipitisha sera kali zinazoiunga mkono Israel, akiitaja Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel na kuhamisha ubalozi wa Marekani huko kutoka Tel Aviv, hatua ambayo ilitia nguvu kanisa la kiinjili la Kikristo la Trump, kundi kuu la wapiga kura wa Republican.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alimtaja Trump kuwa "rafiki bora zaidi ambaye Israel imewahi kuwa naye katika Ikulu ya White House".

Lakini wakosoaji wanasema sera yake ilikuwa na athari ya kudhoofisha ukanda huo.

Wapalestina walisusia utawala wa Trump, kwa sababu ya Washington kutelekeza madai yao kwa Jerusalem, mji ambao ni kitovu cha kihistoria cha maisha ya kitaifa na kidini kwa Wapalestina.

Walitengwa zaidi wakati Trump alipoanzisha kile kinachojulikana kama "Makubaliano ya Abraham", ambayo yalishuhudia makubaliano ya kihistoria ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Israeli na nchi kadhaa za Kiarabu na Kiislamu.

Wapalestina waliachwa katika moja ya maeneo yaliyotengwa zaidi katika historia yao na mamlaka pekee ambayo inaweza kutumia nguvu kwa pande zote mbili katika mzozo, ikizidi kudhoofisha uwezo wao kwani waliona ni kujilinda vijijini.

Trump alitoa kauli kadhaa wakati wa kampeni akisema anataka vita vya Gaza viishe.

Amekuwa na uhusiano mgumu, wakati mwingine ambao haufanyi kazi vizuri na Netanyahu, lakini kwa hakika ana uwezo wa kumpa shinikizo.

Pia ana historia ya uhusiano mkubwa na viongozi katika nchi muhimu za Kiarabu ambazo zina mawasiliano na Hamas.

Trump atalazimika kuamua jinsi ya kuendeleza mchakato wa kidiplomasia uliokwama ulioanzishwa na utawala wa Biden ili kufikia usitishaji wa mapigano Gaza ili kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas.

China na biashara

Mtazamo wa Marekani kwa China ni eneo lake muhimu zaidi la kimkakati la sera ya kigeni na ambalo lina athari kubwa zaidi kwa usalama na biashara ya kimataifa.

Alipokuwa ofisini, Trump aliitaja China kuwa "mshindani wa kimkakati" na akaweka ushuru kwa baadhi ya bidhaa za China zinazoingia Marekani. Hii iliibua ushuru wa 'nipige nikupige' na Beijing kwa bidhaa za Marekani.

Kulikuwa na juhudi za kumaliza mzozo wa kibiashara, lakini janga la Covid lilifuta uwezekano huu, na uhusiano ukazidi kuwa mbaya zaidi kwani rais wa zamani aliita Covid "virusi vya China".

Wakati utawala wa Biden ulidai kuchukua njia ya kuwajibika zaidi kwa sera ya China, kwa kweli, iliweka ushuru mwingi wa enzi ya Trump kwa bidhaa za kuagiza kutoka nje.

Unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Lizzy Masinga na Seif Abdalla