Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vita vya Ukraine: Urusi yapiga makombora kila upande nchini Ukraine
Wanajeshi wa Urusi walifanya shambulizi kubwa la roketi katika miji yote ya Ukraine Jumatatu asubuhi.
Kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu, shambulizi lilifanywa katikati mwa Kyiv.
Milipuko yenye nguvu ilivuma huko Lvov, Ternopil, Ivano-Frankivsk, Zhytomyr, Dnipro, Kharkiv, Konotop, Odessa, Kremenchug na miji mingine.
Shambulio hilo lilifanywa wakati ikielekea saa za asubuhi.
Kuna ripoti za raia waliokufa na kujeruhiwa. Waangalizi wengi wana uhakika kwamba mashamulizi ya leo ni kitendo cha kulipiza kisasi kwa kulipua daraja la Crimea.
Siku ya Jumapili, Rais wa Urusi Vladimir Putin alidai kuhusika na kuhujumu daraja la huduma maalumu za Ukraine.
Huko Kyiv, roketi ziligonga vitu katika wilaya za kati za jiji - Shevchenkovsky na Solomensky. Moja ya roketi ililipuka karibu na mnara wa Hrushevsky kwenye Mtaa wa Volodymyrska, nyingine karibu na daraja jipya la waenda kwa miguu juu ya Volodymyrsky Spusk.
Kufikia saa 10 alfajiri, watu wanane waliuawa na 24 walijeruhiwa, alisema mshauri wa Waziri wa Mambo ya Ndani Rostislav Smirnov.
Alisema kuwa zaidi ya magari 15 yaliharibiwa kutokana na shambulio la Kyiv.
Meya wa Kyiv, Vitali Klitschko, alisema kuwa mashambulizi kadhaa zilifanywa kwenye vifaa muhimu vya miundombinu. Picha za video zinaonesha kuwepo kwa mlipuko mmoja karibu na uwanja wa michezo.
Safari za treni za Kyiv zimesimamishwa kwenye njia zote, vituo vinafanya kazi kama makazi ya waathirika wa bomu. Waokoaji wanafanya kazi katikati mwa jiji.
Shambulio kote Ukraine
Milipuko pia ilitokea katika miji mingine mingi ya Ukraine. Mkuu wa utawala wa mkoa, Valentin Reznichenko, alitangaza shambulio kubwa la kombora katika mkoa wa Dnieper na Dnepropetrovsk. Kuna waliokufa na waliojeruhiwa.
Katika mkoa wa Lviv, shambulio kwenye miundombinu ya nishati lilirekodiwa. Habari hiyo ilithibitishwa na mkuu wa Lviv OVA Maksim Kozitsky.
Waandishi wa BBC wanaripoti milipuko mikubwa na huko Lviv. Shambulio la kombora pia lilipiga kwenye miundombinu ya nishati ya mkoa wa Zhytomyr.
Wakuu wa tawala za kijeshi za mkoa walithibitisha milipuko pia huko Kharkiv, wilaya ya Kremenchug ya mkoa wa Poltava na katika wilaya ya Kropivnitsky ya mkoa wa Kirovohrad.
Kulikuwa na ripoti kuhusu kazi ya ulinzi wa anga katika mikoa ya Khmelnytsky na Terpopol. "Siku ya 229 ya vita kamili. Siku ya 229 wanajaribu kutuangamiza na kutufuta kutoka kwa uso wa dunia. Alisema Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.
"Kuna kombora lililopigwa. Kwa bahati mbaya, kuna wafu na waliojeruhiwa. Ninawaomba: msiondoke. Jilinde mwenyewe na familia yako. Aliandika kwenye mtandao wa Telegram.