Kwanini Urusi inashangilia mapinduzi ya Burkina Faso

Katika mapinduzi ya hivi karibuni nchini Burkina Faso vijana walionekana wakipeperusha bendera za Urusi katika mitaa ya mji mkuu, Ouagadougou - kitu ambacho lazima kilifurahisha mioyo ya watawala wa Kremlin.

Ingawa ilikuwa ni idadi ndogo ya vijana, kitendo hiki kiliibua tetesi kwamba huenda kulikuwa na uhusika kiasi fulani wa Urusi katika matukio yaliyomfanya Kapteni Ibrahim Traoré anyakue madaraka katika nchi iliyokumbwa na ongezeko la ghasia za makundi ya jihadi.

Yevgeny Prigozhin, ambaye ni mshirika wa karibu zaidi wa rais wa Urusi Vladimir Putin na muasisi wa Kundi la Wagner - ambalo ni shirika la mamluki linaloendelesha harakati zake katika mataifa kadhaa ya Afrika - alimpongeza kiongozi kijana wa kijeshi na kumuelezea kama " kijana ambaye kweli anastahili na kijana jasiri wa taifa lake".

"Watu wa Burkina Faso walikuwa chini ya wakoloni, waliowaibia watu pamoja na kuwachezea michezo yao, wakawapatia mafunzo na kuyaunga mkono magenge ya majambazi na kusababisha majonzo makubwa kwa wananchi ."

Hapa alikuwa akimaanisha koloni la zamani la Burkina Faso Ufaransa - na wale walioafiki mapinduzi katika taifa hilo la magharibi mwa Afrika hawakupeperusha tu bendera ya Urusi bali pia walishambulia taasisi za kifaransa, ukiwemo ubalozi wake.

Ghasia hizo zilisababisha wimbi la mshituko kote katika kanda hiyo ya Afrika magharibi, na kwa mara nyingine nchi nyingi kati ya zile zilizokuwa makoloni ya Ufaransa zikaonyesha hisia za chuki dhidi ya Ufaransa.

kwa karibu muongo mmoja Ufaransa imekuwa ikijaribu kuyasaidia majeshi katika kanda ya Sahel - ukanda wa ardhi ambayo ni nusu kame kusini mwa Jangwa la Sahara linalojumuisha nchi ya Burkina Faso - kukabiliana na wanamgambo wa jihadi, ambao baadhi yao wana uhusiano na al-Qaedaau kikundi cha Islamic State.

Lakini hivi karibuni imejiondoa katika nchi jirani ya Mali, ambayo pia ni koloni lake la zamani, kufuatia kuvunjika kwa mahusiano na wanajeshi wa junta huko ambao wamekuwa wakishutumiwa kwa kuelekea Urusi kwa ajili ya kupata msaada wa kupigana na wanamgambo.

Sergei Markov, mshauri wa zamani wa Kremlin, amekuwa mkweli katika tathmini zake : "Watu wetu walimsaidia kiongozi mpya [wa Burkina Faso]. "Nchi nyingine ya Afrika itahama kutoka katika ushirikiano na Ufaransa na kuwa mshirika wa Urusi."

Kwa mshambuzi wa siasa za kieneo Dr Samuel Ramani, huu ni mwanzo wa Urusi wa kuachana na mtindo wake wa kawaida wa kuitikia kushughulikia ukosefu wa usalama katika kanda.

" Katika mapinduzi yaliyopita Urusi ilijaribu kujionyesha kama iliyonufaika kibahati na mabadiliko ya utawala ," anasema Dr Ramanai kutoka taasisi ya Royal United Services Institute (Rusi), kituo cha wataalamu wa ulinzi na usalama, na mwandishi wa kitabu cha Urusi katika Afrika ( Russia in Africa).

"Mara hii Urusi inahusika zaidi kayika kuunga mkono mapinduzi, na hilo limesababisha kuongezeka kwa tetesi kwamba Urusi imehusika katika kazi ya kuyaratibu mapinduzi."

Hatua hii kwa Kikundi cha Wagner, ingawa Urusi imekuwa ikikana mara kwamara kwamba mamluki wana uhusiano wowote na taifa na hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa kuhusika kwa Urusi.

Muda mfupi baada ya kuchukua mamlaka, Kapteni Traoré aliwema bayana kuwa anataka kufanya kazi na washirika wapya wa kimataifa katika kuyarudisha nyuma makundi ya wanamgambo ambayo yamekuwa yakiendesha harakati zake katika nchi hiyo tangu mwaka 2015. Wengi waliamini kuwa alimaanisha Warusi.

Lakini huku juhudi zake zikielekezwa katika kuwashinda Jihadi, anasema pia yuko tayari kufanya kazi na Marekani au nchi yoyote ambayo ina utashi wa kusaidia kuboresha usalama wa nchi.

Marekani huandaa mazoezi makubwa ya kijeshi ya kila mwaka ya ya kupambana na ugaidi kwa ajili ya nchi za Afrika Magharibi - ingawa mwaka huu Mali na Burkina Faso kwa pamoja hawakuhudhuria katika mazoezi hayo yanayofahamika kama Operation Flintlock.

"Ninadhani kwamba Burkina Faso inataka kuepuka mtego ambao Mali ilijingiza ndani yake," anasema Dr Ramani, na kuongeza kuwa wanamgambo wa Junta wa Mali walikuwa nachuki sana kwa mataifa ya Ulaya na marekani tangu walipochukua mamlaka katika mwaka 2020.

"Kwa sasa wametekwa na taifa la Urusi na wanalitegemea kabisa," anasema " Warusi wanapoingia katika michezo hii ya maigizo hawawezi kuwatoa nje. Kitu kama hiki kilifanyika katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati (CAR)."

Kundi la Wagnerlimekuwa likiendesha harakati zake katika CAR tangu mwaka 2018 na harakati zake zimekuwa zikishutumiwa kwa kukiuka haki za binadamu, kutekeleza mauaji, kuimarisha kutoweka kwa watu na ubakaji.

Kuyawajibisha makundi kama Wagner ni jambo gumu, anasema Dr Sorcha MacLeod, profesa msaidizi katika Chuo kikua cha Copenhagen na mwenyekiti wa kikundi kazi cha Umoja wa Mataifa kuhusu matumizi ya Mamluki.

"Wakati unapokuwa na mamluki hawa, halafu nchi inaweza kuhusika katika mzozo wa silaha, bila kuwa upande rasmi unaokubali kuhusika katika mzozo. "Na halafu kukanusha kwao kunakubalika...bila shaka hilo lina athari kubwa inapokuja katika jukumu na uwajibikaji."

Juu ya hilo uwepo wao halisi unaweza kusababisha kutofikiwa kwa mafanikio, anasema. "Wakati aina hizi za wahusika zinapoingizwa katika mzozo wa kijeshi, mzozo huwa wa muda mrefu, na kuna hatari ya uhalifu wa kivita. "Uhalisia ni kwamba mashirika haya hayana motisha ya kumaliza mzozo. Wanatiwa hamasa na pesa"

Marekani inakubali, ikisema kuwa mamluki wa Urusi wanachota raslimali asili katika CAR, Mali kwa ajili ya kufadhili vita vya Moscow katika Ukraine. Katika mameno makali wiki iliyopita, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa alisema ni gharama kubwa kwa Afrika kulipa.

"Badala ya kuwa mshirika wa wazi na kuboresha usalama, Wagner inakuwa katika hali ya mteja mkali ambaye anatoa huduma za usalama katika dhahabu, almasi,mbao, na vyanzo vya raslimali asili - hii ni sehemu ya muundo wa biashara ya kikundi cha Wagner," Linda Thomas-Greenfield aliuambia mkutano wa Baraza la Uslama la Umoja wa Mataifa.

"Tunafahamu faida hizi mbaya zinatumiwa kufadhili mashine za vita za Urusi katika Afrika, Mashariki ya Kati na Ukraine." Hii inaweza kuelezea ni kwanini kapteni Traoré anasita kuweka matumaini yake yote kwa utegemezi wa Urusi.

"Ninadhani kwamba Traoré aajaribu kucheza karata zake na kuonyesha kuwa anaweza kujaribu kufanya kazi na pande zote ," anasema Dr Ramani. "Lakini bila shaka ushirikiano wowte na Urusi utakuwa kifo cha uhusiano na Ufaransa na Magharibi kwa ujumla. Wamarekani na Wafaransa hawatakuwepo pamoja na Warusi.

"Hilo lina muacha njia panda Traoré - je aegemea upande wa Urusi? au ajiondoe, au ajitie katika hatari ya kutokuwa na uungaji mkono wa nje." Bado kuna hasira iliyoongeshwa na vijana Waburkinabe kwamba kukabiliana na tisho la jihadi lazima kiwe kipaumbele cha kiongozi mpya wa junta.

Kiongozi mmoja wa kikanda alisema wiki iliyopita kwamba Burkina Faso imekuwa "ikikaribia kuanguka'' kwasababu ya uukosefu wa usalama. Hatahivyo kuna maswali kuhusu ni kwa vipi wapiganaji wa Wagner watakuwa na ufanisi nchiniBurkina Faso.

Marekani inakubali, ikisema kuwa mamluki wa Urusi wanachota raslimali asili katika CAR, Mali kwa ajili ya kufadhili vita vya Moscow katika Ukraine. Katika mameno makali wiki iliyopita, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa alisema ni gharama kubwa kwa Afrika kulipa.

"Badala ya kuwa mshirika wa wazi na kuboresha usalama, Wagner inakuwa katika hali ya mteja mkali ambaye anatoa huduma za usalama katika dhahabu, almasi,mbao, na vyanzo vya raslimali asili - hii ni sehemu ya muundo wa biashara ya kikundi cha Wagner," Linda Thomas-Greenfield aliuambia mkutano wa Baraza la Uslama la Umoja wa Mataifa.

"Tunafahamu faida hizi mbaya zinatumiwa kufadhili mashine za vita za Urusi katika Afrika, Mashariki ya Kati na Ukraine."

Hii inaweza kuelezea ni kwanini kapteni Traoré anasita kuweka matumaini yake yote kwa utegemezi wa Urusi.

"Ninadhani kwamba Traoré aajaribu kucheza karata zake na kuonyesha kuwa anaweza kujaribu kufanya kazi na pande zote ," anasema Dr Ramani.

"Lakini bila shaka ushirikiano wowote na Urusi utakuwa kifo cha uhusiano na Ufaransa na Magharibi kwa ujumla. Wamarekani na Wafaransa hawatakuwepo pamoja na Warusi.

"Hilo lina muacha njia panda Traoré - je aegemea upande wa Urusi? au ajiondoe, au ajitie katika hatari ya kutokuwa na uungaji mkono wa nje." Bado kuna hasira iliyoongeshwa na vijana Waburkinabe kwamba kukabiliana na tisho la jihadi lazima kiwe kipaumbele cha kiongozi mpya wa junta.

Kiongozi mmoja wa kikanda alisema wiki iliyopita kwamba Burkina Faso imekuwa "ikikaribia kuanguka'' kwasababu ya uukosefu wa usalama. Hatahivyo kuna maswali kuhusu ni kwa vipi wapiganaji wa Wagner watakuwa na ufanisi nchiniBurkina Faso.

Ramani inayoonyesha maeneo yaliko makundi ya jihad katika jimbo la Sahel

Ingawa harakati za kikundi hicho zimekuwa zikiendela katika nchi ya Mali kwa chini ya mwaka mmoja, dalili za mwanzo hazionekani kuwa nzuri kwani mashambulizi ya jihadi yanaongezeka na wapiganaji hao wamekuwa wakishutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu.

Nchi inajirejeshea eneo lake kama kitovu cha mzozo wa Sahel, ikirekodi idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na mashambambulio ya wanamgambo hadi sasa katika mwaka 2022.

Zaidi ya hayo, mwaka 2022 ni mwaka unaotarajiwa kuwa mwaka wa vifo zaidi kwa nchi zote mbili Burkina Faso na Mali tangu uasi uanze.

"Wagner ni wazuri katika kuanzisha vurugu. Lakini kama kikosi cha mapigano wanahangaika, hususan katika ameneo mapya hatari ,"anasema Dr Ramani. Bado anaamini kwamba junta katika jimbo la Sahel wanaweza kuamua kufanya kazi na mamluki wa Urusi kutokana na kushinda kwa Ufaransa kuzuwia kusambaa kwa ghasia.

Zaidi ya hayo Urusi ni mshirika wa kigeni ambaye hana masharti mengi. "Urusi inaonekana kama mshirika ambaye haingilii masuala ya haki za binadamu na demokrasia," anasema Dr Ramani.

"Wala haijaribu kukulazimisha kufuata mtindo wake wa maisha - na hilo linaonekana kupendwa sana kwani itakuw ani udikteta na uporaji."