Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Arsenal wanapanga kuweka dau la £70m kumnunua Sesko
Arsenal wanafikiria kumnunua Benjamin Sesko Januari, Dele Alli yuko tayari kurejea Italia, AC Milan inamtaka Kyle Walker.
Arsenal wanapanga kuweka dau la £70m kumnunua mshambuliaji wa RB Leipzig Benjamin Sesko mwenye umri wa miaka 21 kwenye dirisha la uhamisho la mwezi huu wa Januari, au kujadiliana mkataba wa mkopo wa muda mfupi. (The Sun)
Barcelona pia wana nia ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Slovenia, ingawa vikwazo dhidi yao vya kifedha vitakuwa kizuizi. (Mirror)
Winga wa zamani wa Uingereza Dele Alli, 28, anatazamiwa kusaini mkataba siku ya Jumapili kuichezea klabu ya Cesc Fabregas ya Serie A ya Como hadi Juni 2026 - kukiwa na chaguo la kuongeza mkataba huo kwa msimu ujao zaidi. (Fabrizio Romano)
Zlatan Ibrahimovic, ambaye ni mshauri mwandamizi wa wamiliki wa AC Milan, amethibitisha nia ya klabu hiyo kutaka kumsajili beki wa kulia wa Manchester City na Uingereza Kyle Walker, 34. (Mail, via DAZN)
Wakati huo huo, mkurugenzi wa Juventus Cristiano Giuntoli amesema klabu hiyo ya Italia haijapokea ofa kutoka City ya kumtaka beki wao Andrea Cambiaso, 24. (Goal, via DAZN).
Beki wa kushoto wa Ureno Nuno Mendes, 22, ambaye amekuwa akihusishwa na Manchester United, huenda akasalia na Paris St-Germain. (L'Equipe - in French)
United wanamfikiria beki wa Wolves wa Algeria Rayan Ait-Nouri, 23, kama mbadala wa Mendes. (Independent)
Wakati huohuo, mlinzi wa Uholanzi wa Mashetani Wekundu Tyrell Malacia, 25, huenda akaihama klabu hiyo kwa mkopo katika dirisha la uhamisho la Januari. (Voetball International - in Dutch)
West Ham na Bournemouth ni miongoni mwa vilabu vinavyosubiri habari kuhusu iwapo mshambuliaji wa Brighton Evan Ferguson, 20, atapatikana kwa mkopo mwezi huu. (Express)
Kiungo wa kati Manu Silva, 23, aliyeachwa nje ya kikosi cha Vitoria kwa mchezo wao wa Jumamosi – anafuatiliwa na Wolves. (Wolverhampton Express & Star)
Klabu ya Italia Genoa imefanya makubaliano ya awali kumsajili winga mwenye umri wa miaka 28 Maxwel Cornet, ambaye amekuwa kwa mkopo Southampton kutoka West Ham. (Fabrizio Romano)
Arsenal, Chelsea na Bayern Munich ni miongoni mwa vilabu vinavyotaka kumsajili beki wa kati wa Sporting Ousmane Diomande, 21. (Caught Offside)
Deportivo La Coruna huenda ikalazimika kumuuza winga Yeremay Hernandez, 22, ingawa Deportivo inasemekana kuwa wamekataa ofa ya awali ya Chelsea kwa vile wanataka kima cha kiasi na karibu na kipengele cha kuachiliwa kwa mchezaji huyo cha pauni milioni 17. (Caught Offside)