Je, miamba hii minne kugonga dunia?

    • Author, Yemisi Adegoke
    • Nafasi, BBC World Service
  • Muda wa kusoma: Dakika 5

Mara nyingi tunafikiria kuhusu miamba ama sayari ndogo za anga za mbali tunapoangalia filamu za sayansi au tunaposikia habari kuhusu uwezekano wa miamba hii kugonga Dunia. Lakini duniani kote, mashirika na vituo vingi vya uchunguzi hufuatilia miamba hii kwa sababu mbalimbali.

Miamba hii ni mabaki kutokana na kuundwa kwa mfumo wa jua, takriban miaka bilioni 4.6 iliyopita. Kuna zaidi ya miamba milioni moja inayojulikana, mingi ikiwa kwenye ukanda mkuu wa miamba, unaozunguka Jua kati ya Mars na Jupita.

Hata hivyo, baadhi ya miamba hii inalikaribia dunia na inaweza kutusaidia kuelewa asili ya uhai, anafafanua Monica Grady, Profesa Mstaafu wa Sayansi ya Sayari na Anga katika Chuo Kikuu cha Open nchini Uingereza. "Baadhi ya miamba hii ina vitu vinavyoweza kuwa viambato muhimu vya uhai," anasema. "Nadharia moja ni kwamba uhai ulianza duniani kwa sababu tu miamba hii iliileta viambato vya uhai."

Ingawa miamba mingi haina madhara na hupita bila taabu, nyingine ina umuhimu. Agata Ruzek, mtafiti katika Shule ya Fizikia na Astronomia ya Chuo Kikuu cha Edinburgh nchini Uingereza, anasema, "Kuna ongezeko la maslahi katika vitu vinavyoikaribia dunia.

Inafuatiliwa kwa karibu hadi njia zao zitakapojulikana vizuri vya kutosha kuzuia, na wakati mwingine hata kutabiri, uwezekano wa kugongana. Katika umbali mkubwa kutoka dunia, tunatafuta vitu vyenye muundo usio wa kawaida."

Linapokuja suala la ukubwa, miamba mikubwa haileti wasiwasi sana. "Tunajua hasa ilipo na inakwenda wapi," Ruzek anaeleza. "Tuna uelewa mzuri sana wa sheria zinazosimamia mwendo wake, na tunasoma visa visivyo vya kawaida ili kuielewa vizuri." Anaongeza kuwa, "Miamba midogo ambayo haijagunduliwa inaweza kuleta wasiwasi mkubwa, hadi njia zao zitakapojulikana."

Hapa chini kuna miamba mitatu muhimu inayofuatiliwa kwa sasa na wanasayansi, pamoja na mwamba mmoja muhimu sana ambao NASA umezindua misheni ya kuuchunguza.

1. Apophis

NASA ilisema kwamba miamba ya Apophis si tishio kwa dunia kwenye karne ijayo. Apophis imepewa jina la mungu wa kale wa Misri wa machafuko na uharibifu na iligunduliwa mwaka 2004. Nafasi ya kugonga dunia ilionekana kuwa ndogo kwa miamba hii, lakini baadaye NASA ilitangaza kuwa "ina uhakika hakuna hatari ya miamba hii kugonga dunia kwa angalau miaka 100 ijayo."

"Sasa tunajua kwamba itapita salama karibu na dunia mnamo Aprili 13, 2029," anasema Ruzek. Aliongeza: "Imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu tangu igunduliwe, na itakaribia sana dunia, kwa umbali sawa na ule wa satelaiti za geostationary. Tunaamini kwamba kukaribia kwake dunia kunaweza kufanya umbo la mimba hiyo kubadilika."

Kwa mujibu wa NASA, mvuto wa dunia pia utazalisha nguvu ya mvuto ambayo itabadilisha mzungumzo wa Apophis kuzunguka Jua na inaweza kusababisha maporomoko madogo ya ardhi kwenye miamba. Ina kipenyo cha wastani cha mita 340 takriban urefu wa viwanja vitatu vya mpira na itapita takriban kilomita 32,000 kutoka kwenye uso wa dunia. Hiyo ni karibu vya kutosha kuonekana kwa macho.

2. Asteroidi 2024 YR4

Ikiwq na ukubwa wa kati ya mita 53 na 67, takriban ukubwa wa jengo la orofa 15, kama inavyosema NASA, mimba ya 2024 YR4, iligunduliwa mwaka 2024 na hivi karibuni ilizua vichwa vya habari duniani kote ilipoonekana kuwa na uwezekano mdogo wa kugongana na dunia mwaka 2032.

Watafiti hata walikadiria nafasi ya kugonga dunia kuwa 1 kati ya 32, lakini baadaye NASA ilikanusha hilo. "Moja ya changamoto za kuangalia miamba inayoelekea kugongana na dunia ni kubaini athari zianzoweza kutokea," anasema Monica Grady. "Tunahitaji kuendelea kufuatilia mwelekeo wake," aliongeza.

Bado kuna uwezekano wa asilimia 3.8 kwamba 2024 YR4 itagongana na Mwezi, lakini NASA inaongeza kuwa hata kama athari itatokea, haitabadilisha mzunguko wa dunia.

3- ديديموس وديمورفوس

3. Didymos na Dimorphos

Didymos, ambayo inamaanisha pacha kwa Kigiriki, ni sayari ndogo, na Dimorphos ni mwezi mdogo unaoizunguka. Hakuna hata mmoja kata ya hii miamba inayochukuliwa kuwa tishio kwa dunia, lakini wanapita karibu nayo.

Mwaka 2022, walikuwa shabaha ya Jaribio la Uelekezaji wa Asteroidi Pacha (DART) la NASA, ambalo lilijumuisha kutuma uchunguzi kugongana na Dimorphos, na kuharibika katika mchakato huo. Lengo lilikuwa kujaribu uwezo wa kugeuza salama miamba ya anga ambayo inaweza kutishia dunia.

Dimorphos na Didymos ziliainishwa kwa uangalifu. Hakuna hata moja iliyokuwa kwenye njia ambayo ingeingiliana na dunia kabla ya jaribio, na mabadiliko yoyote madogo katika uhusiano wao wa mzunguko yangeongeza hatari.

"Chombo cha kuchunguza miamba hii kilivyotumwa kiligongana na mwezi mdogo Dimorphos, ikibadilisha obiti yake kuzunguka Didymos katika jaribio la kwanza la vitendo la ulinzi wa sayari," anasema Rozek. "Mabadiliko haya yalipimwa hasa kwa kutumia uchunguzi wa ardhini. Tutaendelea kufuatilia mabadiliko haya kabla ya kuwasili kwa chombo kingine 'misheni ya Hera' mwaka ujao kuchunguza athari zake," aliongeza.

4. Psyche

Imefafanuliwa na NASA kama "moja ya vitu vya kuvutia zaidi kwenye ukanda mkuu wa miamba," Psyche iligunduliwa mwaka 1852. Imepewa jina la mungu wa roho wa kike wa Kigiriki.

Psyche iko mbali sana na dunia, ikizunguka Jua kati ya sayari za Jupita na Mars na inadhaniwa kuwa na chuma na mwamba mzito. Wanasayansi wanaamini kwamba sehemu kubwa ya chuma inatoka kwenye kiini cha sayari ndogo, kiambato cha sayari, na kuichunguza kunaweza kufichua jinsi kiini cha dunia na viini vya sayari zingine jinsi vilivyoundwa.

Mwaka 2023, NASA ilizindua misheni ya kuifuatilia kwa kupata ramani na kuichunguza zadi.

Ugunduzi mpya

Mapema mwezi huu, Kituo cha Uchunguzi cha Vera Rubin kilifichua kuwa darubini yake mpya iligundua zaidi ya miamba mipya 2,000 na vitu vingine saba karibu na dunia ndani ya masaa 10 tu.

Takriban miamba 20,000 hugunduliwa kila mwaka, na vituo vingine vyote vya uchunguzi duniani na angani vikijumlishwa.

"Ikiwa unataka kutazama anga la usiku, unahitaji uwanja mpana sana wa kuona," anasema Profesa Grady. "Hicho ndicho inachofanya darubini hii katika Kituo cha Uchunguzi cha Vera Rubin."

Kituo hicho kinasema kinatarajia kugundua mamilioni ya miamba mipya katika miaka michache ya kwanza ya maisha ya mradi, na kuwapa wanasayansi miamba zaidi ya kuchunguza na kufichua vidokezo zaidi kuhusu mfumo wa jua.