Mitindo ya nywele ilivyowasaidia watumwa wa Kiaafrika huko Colombia kutoroka

Chanzo cha picha, AMAFROCOL
Kilomita 50 kutoka katika eneo la maji la Caribbean la Colombia, katika eneo la mraba lililotengwa katikati ya milima, kuna sanamu inayojieleza imewekwa ili kutoa heshima kwa kumbukumbu ya shujaa wa kipekee.
Benkos Biohó anaelezewa kama mtu "wa kiroho, jasiri na mwenye uthubutu" ambaye, mwishoni mwa 1599, aliamuru "mapinduzi na kuwaondoa baadhi ya watu weusi kwa kutoroka", kulingana na mwandishi wa historia wa Uhispania Fray Pedro Simón.
Neno 'cimarrón' tayari linaelezea sehemu ya hadithi hii. "
Cimarron inasemekana kuwa ni kuhusu mtumwa au mnyama wa kufugwa anayekimbilia shambani na kuwa mwitu». Kamusi ya Royal Spanish Academy (1970).
Neno hili linaibua karne nyingi za unyonyaji wa kikatili wa mamilioni ya Waafrika ambao waliondolewa kutoka katika makazi yao na kupelekwa ng'ambo ya dunia ili kuuzwa na kufanywa kama wanyama katika kuwahudumia watawala wao.

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini pia inazungumza juu ya uthubutu wa uasi.
Benkos Biohó pamoja na mke wake Wiwa, watoto wao na wanaume na wanawake wapatao thelathini waliongoza moja ya mapinduzi haya kwa kukimbia kutoka Cartagena de Indias na kuwashinda kundi la walinzi waliotumwa kuwakamata.
Katika kukimbia kwao, hawakusimama hadi walipofika mahali ambapo ni katikati ya Montes de María, ambapo mwaka wa 1714, baada ya mapambano ya zaidi ya karne moja, ilihalalishwa chini ya jina la San Basilio de Palenque, kwa amri ya kifalme, ambapo kanisa hilo ilikuwa katika eneo ambalo kwa sasa kuna mnara.
"Palenque de San Basilio haikuwa ya kwanza wala ya pekee, lakini ndiyo inayojulikana zaidi kwa mkakati wake wa uhuru na kwa sababu iliamriwa na Mfalme Biohó, na hatimaye kwa sababu ulikuwa mji wa kwanza huru nchini Marekani," aliieleze BBC Emilia Eneyda Valencia Murrain, mwanzilishi wa Chama cha Wanawake wa Afro-Colombia (Amafrocol).

Chanzo cha picha, Getty Images
Ingawa baadhi ya maeneo yaliyozungukwa na kuta (palenques) yalififia baada ya muda, San Basilio alihifadhi sehemu muhimu ya urithi wa mababu zake, nyingi kupitia mapokeo ya mdomo, utamaduni unaotukumbusha kuwa Benkos Biohó hakuwa peke yake katika kazi yake.
Na kwamba bila msaada wa mke wake na wanawake wengine ingekuwa vigumu zaidi kupata njia yake ya ushindi.
Akili zao ndizo ziliandika taarifa muhimu na ujanja wao ambao uliunda mfumo wa kuweka kumbukumbu ili kuwaonyesha watumwa njia za uhuru bila watawala wao kutambua.
Kukariri mandhari
Kutekwa nyara na kusafirishwa, Waafrika walikuja Marekani ili kutumika.
Lakini haikujalisha namna walivyojaribu sana kuwavua alama zote za ubinadamu, kuna ile sifa ya ukaidi ambayo ilidumu sana kwenye kumbukumbu ya kile kilichovunjwa kutoka kwao kama vile hamu ya kutoroka kwenye mateso.
Wakati njia mbadala pekee ilikuwa kutoroka, katika eneo geni kama hilo, unajuaje pa kwenda?
Kwenye pwani ya Carribean ile inayoitwa Ufalme Mpya wa Granada, wanawake watumwa walibuni njia nzuri ya busara ya kuunda na kuficha ramani za kuelekea mahali kwenye uhuru wa wazi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wanawake hawakutiliwa shaka kama hiyo.
Aidha, walikuwa na tabia ya kuyaacha mazingira yao kuliko wanaume kutokana na kazi walizopewa.
"Kwa kawaida uwezo, hekima, na ujanja wa wanawake hudharauliwa na ndio maana, kwa upande wa Colombia, wameweza kulinda siri nyingi, ili kuzitumia baadaye kwa faida ya jamii: uponyaji, upishi, kutengeneza siri ...
"Hilo ndilo lililotokea katika mchakato wa uhuru wa San Basilio palenque," alisema Emilia Valencia, ambaye alisikia hadithi kutokahuko alipoenda kuchunguza "miaka mingi, mingi iliyopita.
" "Waliniambia kuwa eneo hilo lilizaliwa kwa sababu, wakati wanawake walivyokuwa wakitoka shamba hadi shamba, iwe ni kufanya shughuli au chochote, walikuwa makini na barabara na hatua muhimu.
"Kisha wakawasilimua hilo wanaume na kwa pamoja wakapanga mkakati".
Chimbuko
Lazima ukumbuke kuwa watumwa walitoka miji tofauti barani Afrika, wakiwa na lugha tofauti, na mwanzoni ilikuwa ngumu kwa kila mtu kuelewana.
" Lakini kulikuwa na lugha ya kawaida ambayo walikuwa wameileta kutoka katika bara lao la nyumbani.
"Tunachokiita chimbuko la kusuka' , ambao umeunganishwa kwenye ngozi ya kichwa, maalum kwa watu wa Kiafrika."

Chanzo cha picha, AMAFROCOL
Na hiyo misuko ilizungumza: walisimulia hadithi, walitangaza hali ya kijamii ya yeyote aliyesuka, waliweka wazi hali zao za ndoa, ni dini gani wanayoabudu, iliwatambulisha kuwa watu wa jamii fulani au makabila.
Katika Ulimwengu Mpya, walianza kuzungumza juu ya uhuru.
"Baada ya kupanga na wanaume hao, walikubaliana kwamba wangetumia kusuka, mitindo ya nywele, kama mafumbo na siri za kuonesha njia wanazopaswa kutorokea.
" Watumwa hao wakawa wachora ramani bila penseli wala karatasi, wakiunda na kuvaa ramani zilizochorwa na nywele vichwani mwao.
"Hivyo ndivyo walivyobuni kile kinachojulikana kama ramani maarufu za kutoroka au njia za uhuru au njia za kutoroka," anasema Valencia.
Na si hivyo tu.
Katika mitindo hii ya nywele, wanawake pia waliweka vitu vya thamani ambavyo vingetumika mara walipofika kwenye palenques, kama vile kiberiti, vipande vidogo vya dhahabu au mbegu za thamani kwa ajili ya kulima.

Chanzo cha picha, AMAFROCOL
Kusukwa misokoto
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
"Wanaume 'walisoma' kanuni katika mitindo yao ya nywele, kuanzia kwenye paji la uso, ambazo ziliweka mipaka ya mahali walipokuwa, hadi nyuma ya shingo, ambayo iliwakilisha mlima uliofungwa, mahali ambapo walipaswa kuelekea katika kukimbia kwao", alisema katika utafiti "Poetics of the Afro-Colombian hairstyle" (2003) mwanasosholojia Lina María Vargas.
Alikuwa ameambiwa na Leocadia Mosquera, mwalimu kutoka idara ya Chocó ambaye alifundishwa siri ya mitindo ya nywele na bibi yake.
Alimuelezea kwamba haikuwa tu suala la kuwakilisha vipengele vya kijiografia au onyo kuhusu kuwepo kwa vituo vya ufuatiliaji: kwa vichwa vyao vilivyojazwa siri walipaswa kuwasiliana na kila mtu mkakati ulikuwa nini.
Misuko pia ilionyesha sehemu za kukutana, zilizowekwa alama na safu kadhaa za misuko zinazoungana mahali pamoja, kila moja ikiwakilisha njia inayowezekana.
Katika hatua hizo walikutana wakati wa kutoroka ili kujua wanaendeleaje na kufanya maamuzi.
Msuko wa mwisho ulikuwa upande wa nyuma ya shingo.
Kama Leocadia alivyoeleza, kwa mfano, wangekutana chini ya mti, wangemaliza msuko wima na kwenda juu, ili usimame; ikiwa ni ukingo wa mto, waliuweka pembeni mwa masikio.
Kwa kuongezea, wakati mwingine kulikuwa na misuko ya urefu tofauti kwenye njia zile zile, vikiambia vikundi tofauti umbali wa kwenda, wenye nguvu zaidi walipaswa kuja nyuma.
Taarifa hizi zote na zaidi zilipitishwa katika miji na mashamba ya Colombia ya kikoloni kwa kila mtu kuona lakini uelewa wa wachache tu.
Toleo lingine
Kwa bahati mbaya, mitindo hii ya nywele za ukombozi baada ya muda ikawa silaha ya unyanyapaa.
"Kitu fulani kilitokea," anasema Valencia

Chanzo cha picha, AMAFROCOL
"Watumwa huru ’Maroon’ walisaidia kuunda miji kwa sanaa.
Lakini basi mitindo ya nywele ilipumzika haikuendelea.
"Kwa nini? Kwa sababu walivyoonekana kuwa huru na kuanza kuunganishwa katika jamii, wanawake walilazimika kuacha mitindo ya nywele zao, ambayo ilikuwa mila zao, utamaduni wao.
" Ingawa vizazi vingine vilipokea kwa shukrani urithi huo kwa hadithi zilizopitishwa kutoka kizazi hadi kizazi, wengi walilazimika kuiweka katika nyanja binafsi na wengi zaidi hawakujua.
"Kulikuwa na mahitaji ya waajiri na jamii kwa ujumla kuunganisha mfumo wa aina moja, hivyo wanawake weusi walilazimika kunyoosha nywele zao.
Tangu wakati huo, anasema Valencia, "kila kitu kinapitia katika nywele zao... vurugu zilinza kuanzia shule ya chekechea.
"Imekuwa mbaya, lakini tunapiga hatua, shukrani kwa mazungumzo, vikao, mafunzo na michakato yote ya kitamaduni.
"Tumeweza kuondoa ukoloni akilini na mwilini na sasa unaweza kuona tunakuwa na makamu wa rais mweusi (Francia Elena Márquez Mina) na waziri (wa Elimu, Aurora Vergara Figueroa).
"Kwa wanawake weusi, kupitia taratibu hizo za kunyoosha nyweli kwa kutumia kemikali na kadhalika ili kujaribu kwenda sawa, niamini, ni mateso na inaumiza sana," Valencia anahitimisha.















