Ifahamu meli ya mwisho ya watumwa kutoka Afrika hadi Marekani, safari ilikuwaje?

Perbudakan, amerika serikat, sejarah

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Vifusi vya meli ya Clotilda vinang'inia kwenye upande wa barabara inayotengenisha sehemu mbili za mji wa makazi ya Africatown .

Kugunduliwa kwa mabaki ya meli ya Clotilda iliyozama miaka 160 iliyopita kunaleta maisha mapya katika kijiji kidogo kilichojengwa na manusura wa utumwa.

"Ni vigumu sana kufikiria kuwa wangepitia eneo hili," alisema Darron Patterson.

Akiwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazao wa Clotilda, Patterson anazungumza kwa ufasaha juu ya safari ya Clotilda, msafirisha watumwa wa mwisho anayejulikana kufika Marekani.

Babu yake mkubwa alikuwa Kupollee, ambaye baadaye alibadilisha jina lake kuwa Pollee Allen. Alikuwa mmoja wa wanaume, wanawake na watoto 110 waliotekwa kikatili kutoka Benin huko Afrika Magharibi na kupelekwa Marekani ndani ya meli hiyo yenye sifa mbaya.

Hadithi ya jinsi jamaa za Patterson walifika Marekani kwa meli haramu ya watumwa ilianza kwa mwendo ya chini sana.

Mnamo mwaka wa 1860, au takriban miaka 52 baada ya serikali ya Marekani kupiga marufuku usafirishaji wa watumwa, mfanyabiashara tajiri wa Alabama aitwaye Timothy Meaher aliweka dau kwamba angeweza kupanga usafiri wa Waafrika.

Waafrika aliosema walitekwa nyara ili kusafiri chini ya uangalizi wa serikali ya shirikisho na waliweza kukwepa marufuku.

Hilo lilifanikiwa baadaye. Alisaidiwa na nahodha wa meli aitwaye William Foster ambaye aliongoza meli ya ya hadi urefu wa mita 24.

Meli hiyo ilisafiri ikipitia Bahari ya Atlantiki kwa wiki sita. Meli iliteleza hadi Mobile Bay mnamo Julai 9, 1860 chini ya giza.

Ili kuficha ushahidi wa uhalifu huo, meli hiyo iliyotengenezwa kwa mbao za misonobari ya manjano ilichomwa moto, kisha ikazama kwenye mto.

Katika mto huo wenye kina kirefu, meli kisha ikafichwa chini ya maji, kuwepo kwake kukatoweka.

Ukweli huo ulizama hadi miaka 160 baadaye. Wakati huo mto ulipungua kwa njia isiyo ya kawaida. Mwandishi wa habari wa eneo hilo aitwaye Ben Raines kisha akapata mabaki ya meli kubwa ambayo ilifikiriwa kuwa ilihusiana na Clotilda.

Lakini matokeo yaligeuka kuwa uwongo. Hata hivyo, ugunduzi huo ulifufua shauku na kusababisha utafutaji wa kina, ikiwa ni pamoja na Tume ya Historia ya Alabama, Jumuiya ya Kitaifa ya Kijiografia na Mradi wa Slave Wrecks.

Baada ya juhudi kubwa, mnamo Mei 2019 hatimaye ilitangazwa kuwa mabaki ya Clotilda yalipatikana.

Perbudakan, amerika serikat, sejarah

Chanzo cha picha, Corbis/Getty Images

Maelezo ya picha, Mchoro unaoonyesha shuguli ya kupakia na kushusha pamba ya watumwa kwenye mto Alabama River katika karne ya 19.

Leo hii , au takriban miaka mitatu baadaye, Jiji la Alabama linakaribia kushamiri kwa utalii. Kuvutiwa na hadithi ya Meli ya Clotilda na maisha ya mateka wake inaongezeka polepole.

Patterson alikubali kunionyesha eneo la Africatown, makazi ambapo wengi wa manusura wa utumwa wa meli waliishi. Patterson pia alikulia katika eneo hili.

Tulianza ziara kwenye kipande hiki cha ardhi kwenye kingo za Mto Mobile. Hapa ndipo kikundi cha wazao wa manusura wa meli ya watumwa ya Clotilda hukutana kila mwaka kwa Tamasha lao la Under the Bridge.

Kupitia tukio hilo, walitaka kueleza jinsi mababu zao walivyofika hapa.

Ikiwa kilomita tano kaskazini mwa jiji la Mobile, Africatown ilianzishwa na manusura 32 wa meli ya watumwa ya Clotilda. Walinusurika na kuishi katika enzi ya ukombozi mwishoni mwa Vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo 1865.

Tamaa yao kwa nchi yao iliwafanya waanzishe jumuiya zenye uchangamfu zinazochanganya mila za Kiafrika na njia za maisha za jadi za Wamarekani, kama vile kufuga mifugo na kusimamia mashamba.

Moja ya miji ya kwanza iliyoanzishwa na kudhibitiwa na Waamerika wa Kiafrika nchini Marekani, Africatown ina kanisa lake, kinyozi, na maduka yake, moja ambayo inamilikiwa na Patterson.

Pia kuna Shule shule ya umma ambayo ni uti wa mgongo wa jamii ya eneo hilo.

Hata hivyo, mji huu ambao wakati mmoja ulikuwa mzuri ulipitia nyakati ngumu wakati barabara kuu ilipojengwa katikati mwa eneo hilo mwaka wa 1991. Uchafuzi wa viwanda pia ulimaanisha kwamba wakazi wengi waliosalia hatimaye walipakia na kuondoka.

"Hatukuweza hata kukausha nguo kwa sababu ingefunikwa na majivu ya bidhaa kutoka kwa matangi ya kuhifadhia mafuta na viwandani nje kidogo ya Africatown," alisema Patterson.

Jamii ya Africatown, ambayo iliongezeka hadi watu 12,000 mwaka 1960, sasa imepungua hadi takriban watu 2,000 pekee.

Perbudakan, amerika serikat, sejarah

Chanzo cha picha, Buyenlarge/Getty Images

Maelezo ya picha, Watumwa wenye asili ya Afrika katika shamba Alabama, mwaka 1900.

Kuhama, umaskini, na athari za uharibifu wa mazingira zinaonekana wakati Patterson anaposonga mbele zaidi katika Africatown. Eneo hilo limejaa viwanda vilivyotelekezwa.

Ardhi tupu na nyumba zilionekana kando ya barabara tulivu za makazi, ambazo zingine ziliharibiwa vibaya.

Lakini Africatown inabadilika, kwa mara nyingine tena. Baada ya kugunduliwa meli hiyo, kulikuwa na hamu ya kujenga upya na kuhifadhi mahali hapa pa kihistoria.

Takriban miaka mitatu tangu kugunduliwa kwa meli ya Clotilda, mabaki ya meli hiyo yamefanyiwa uchunguzi wa kina wa kiakiolojia. Moja ya malengo ilikuwa kuamua jinsi ya kuinua kwa usalama kutoka chini ya maji.

Kuripoti kwa vyombo vya habari ilileta fedha nyingi kutoka kwa serikali, vikundi vya jamii, na taasisi za kibinafsi hadi Africatown.

Mmoja wao ni kutoka The Africatown Redevelopment Corporation ambayo hutoa ruzuku maalum kwa ajili ya kurejesha nyumba zilizoharibiwa na kujenga upya kwenye ardhi iliyoachwa.

Perbudakan, amerika serikat, sejarah

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Makumbusho ya kukumbuka masaibu ya watumwa iliyofunguliwa katika Alabama.

Tangazo la kugunduliwa kwa meli hiyo mnamo 2019 liliamsha udadisi wa Patterson. Alianza kukusanya mabaki ya mababu zake hadi "maisha yake yote yalibadilika".

Tangu wakati huo amekuwa akijishughulisha katika kuhakikisha kuwa hadithi ya mababu zake inasimuliwa kwa usahihi, ikijumuisha jukumu lake katika filamu ya Descendant ambayo itaonyeshwa mara ya kwanza katika Tamasha la Filamu la 2022 la Sundance.

Pia aliwahi kuwa mtayarishaji wa filamu itakayotolewa hivi karibuni, The 110: The Last Enslaved Africans Brought to America. Filamu hii inawahusu manusura wa meli ya Clotilda.

Kwa Patterson, ugunduzi wa meli ulileta matumaini mapya kwamba Africatown ingepanda.

"Baada ya miaka mingi ya kukanusha, hatimaye imethibitishwa mahali ilipo.

"Ni muhimu kwa sura ya Africatown kama ufufuaji wa makazi ambao unafanyika kwa sasa," alisema.

Mahali pengine pa ziara ya kuongozwa ya Patterson ni Africatown Heritage House. Jengo hilo liko katikati ya kitongoji, likiangalia nyumba zilizotunzwa vizuri kwenye barabara iliyo na mitende.

Jumba la makumbusho linalojengwa litafunguliwa mwanzoni mwa msimu wa joto wa 2022. Mkusanyiko huo unajumuisha vitu vya kale vya Afrika Magharibi na sehemu ya ajali ya meli ya Clotilda, ambayo inaonekana katika sehemu za uhifadhi.

Perbudakan, amerika serikat, sejarah

Chanzo cha picha, Print Collector/Getty Images

Maelezo ya picha, Wamiliki wa shamba la pamba ambao walitumia huduma za watumwa walikuwa miongoni mwa watu tajiri zaidi nchini marekani wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka ya 1850.

Mradi wa ukarabati pia unajumuisha daraja la waenda kwa miguu linalounganisha maeneo mawili ya Africatown. Maeneo hayo kwa sasa yametenganishwa na barabara kuu.

Ziara ya kando ya maji ambayo huchukua wageni karibu na eneo la ajali ya meli imeratibiwa kuanza majira ya masika ya 2022. Baadhi ya wenyeji pia hutoa ziara za kutembea za Africatown.

Wakati idadi ya watalii bado si kubwa, Africatown inakabiliwa na msururu wa changamoto zinazofanana na makazi mengine nchini Marekani, hasa yale yanayopitia ufufuaji wa haraka.

Masuala haya ni pamoja na kuhakikisha kuwa wananchi wote wanaunga mkono mabadiliko. Lakini Patterson anasema jamii ya Africatown imeungana katika dhamira moja.

Unaweza pia kusoma :