'Hatuondoki kamwe' - familia zasalia kaskazini mwa Gaza wakati Israeli ikijiandaa kwa operesheni ya ardhini

Palestinians next to a demolished building in Gaza City

Chanzo cha picha, EPA-EFE

Maelezo ya picha, Hali kwa watu wa Gaza inazidi kuwa mbaya, huku maji, chakula, umeme na dawa vikiwa haba
    • Author, Feras Kilani
    • Nafasi, BBC Arabic, Sderot, Israel

Muda wa mwisho wa Israel kwa raia kuondoka kaskazini mwa Ukanda wa Gaza umepita lakini baadhi ya watu wanasema watasalia huko.

Makataa ya Israel ya watu kuondoka kaskazini mwa Ukanda wa Gaza yamepita, lakini Mohamed Ibrahim, hatahama.

"Sitaondoka katika nchi yangu, sitaondoka kamwe," mwanamume huyo wa miaka 42 alisema, aliketi sebuleni iliyojaa akizungukwa na jamaa ambao wamejazana ndani ya nyumba kutoka maeneo mengine. Wengine walizungumza huku wengine wakiangalia simu zao kwa habari za hivi punde kuhusu msiba huo.

"Siwezi kukimbilia mahali pengine, hata kama wataharibu nyumba zetu juu ya vichwa vyetu," aliongeza. "Nitabaki hapa".

Akiwa na familia yake tayari mara kwa mara amezunguka eneo linalozunguka Mji wa Gaza, kitovu cha mijini katikati mwa kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

"Jumapili iliyopita saa 02:00 asubuhi, kulitokea mashambulizi na makombora," alisema. "Nilikimbia na mke wangu na watoto wanne."

Waliondoka nyumbani kwao Jabalia kuelekea eneo la Sheikh Radwan, lakini walisikia eneo hilo pia lingelengwa na wakaenda kwenye kitongoji cha Jiji la Gaza.

Lakini hakuona kama ni kweli kwao kuondoka kaskazini mwa Gaza, ambayo Israel imewaonya watu kuhama.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

"Tulitakiwa kukimbilia kusini, mimi na familia yangu tuende wapi?" Mohamed aliuliza.

Watoto wake wanakosa bustani yao, wakiwa wamejazana katika orofa pamoja na familia yao kubwa. Mwanawe Ahmad alipenda baiskeli kuzunguka mtaa wao na rafiki yake. Anaendelea kumuuliza baba yake ikiwa rafiki yake wa dhati yungali hai, lakini hakuna njia ya kumfikia.

Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza

'Hakuna maisha'

Abo Jamee trying to tease out the last drops of water
Maelezo ya picha, Abo Jamee akijaribu kufyonza matone ya mwisho ya maji

Katika barabara iliyo karibu, Abo Jameel, mjenzi mwenye umri wa miaka 38, alijiinamia chini kwenye bomba lililounganishwa na mfumo wa maji, akijaribu kuteka matone ya mwisho ya maji

"Kwa siku nane kumekuwa hakuna chakula wala maji," alisema. Israel imekata umeme na maji ya Gaza, na kuzuia mafuta na vifaa vingine kuingia.

"Hakuna maji, hakuna umeme, hakuna maisha, taabu," aliongeza. Lakini pamoja na watoto wake watano ameamua kubaki. Ana wavulana wawili na wasichana watatu, mdogo ana umri wa miaka minne .

"Hatuna pa kwenda, hatutoki hata wakitaka kupiga nyumba zetu."

"Tunaweza kwenda wapi kama familia ya watu watano au sita?" alisema.

Wanajeshi wamejiandaa

TH

Hamas wanasema watu 400,000 kati ya milioni 1.1 wanaoita kaskazini mwa Gaza nyumbani walielekea kusini kwenye Barabara ya Salah al-Din katika muda wa saa 48 zilizopita, kufuatia amri ya Israel kuondoka.

Ukitazama ukanda wa Gaza kutoka kilima zaidi ya kilomita moja kutoka mpaka na Israel, ukubwa wa mashambulizi ya ardhini ambayo yanaweza kuanzishwa hivi karibuni ni wazi.

Kando ya barabara kuu inayopita karibu nayo kundi la magari ya majeshi wenye silaha walipiga kelele, huku ndege isiyo na rubani ya kijeshi ikizunguka angani juu.

Karibu naua la mpaka mlio wa risasi kutoka kwa silaha ndogo .Kwa kujibu, kifaru cha Israeli kilifyatua safu ya makombora.

Taarifa za habari za ndani zilisema kuwa mshambuliaji wa Hamas ambaye alikuwa amefichwa katika eneo hilo aliuawa.

Mji wa karibu wa Sderot wa Israeli ulikuwa tayari umeachwa, na amri rasmi ya kuhama ilitolewa na mamlaka dakika chache baada ya sisi kuondoka.

Huko nyuma zaidi kutoka mpakani, milio ya risasi nzito yaweza kusikika kutoka kwa bunduki zilizochimbwa mashambani kando ya barabara kuu. Hatukuweza kuendesha gari kwa zaidi ya dakika chache bila kupita msafara wa kijeshi wa magari au mizinga iliyokuwa ikisafirishwa .

Onyesho hili kubwa la nguvu za kijeshi litakuwa kiini cha mpango wa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu "kubomoa Hamas" baada ya wanamgambo hao kushambulia Israel Jumamosi tarehe 7 Oktoba.

Zaidi ya watu 1,300 waliuawa nchini Israel katika shambulio hilo la kuvuka mpaka, na mateka 126 walikamatwa.

Idadi ya vifo katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi ilifikia Wapalestina 2,383 waliokufa na 10,814 kujeruhiwa Jumapili asubuhi, kulingana na vyanzo vya wizara ya afya ya Palestina.

Kuzungukwa na vita

Children are still out in the streets in Gaza City
Maelezo ya picha, Watoto bado wako nje mitaani katika Jiji la Gaza

Katika mji wa Gaza watoto bado wamekuwa wakicheza mitaani.

Wanachukua fursa ya muda mfupi wa utulivu kwenda nje kwenye vichochoro na barabara za kukimbia.

Ndio njia yao pekee katika maisha ambayo sasa yamezungukwa na vita.

Takriban nusu ya wakazi wa Gaza wako chini ya umri wa miaka 18. Na zaidi ya watoto 700 wameuawa huko katika mzozo huu tayari, kulingana na wizara ya afya ya Mamlaka ya Palestina.

Mamlaka ya Hamas huko Gaza imewaambia watu wasiondoke kaskazini huku Israel ikisema Hamas inawazuia watu kuondoka ili kuwatumia kama ngao za binadamu, jambo ambalo kundi la wanamgambo linakanusha.

Iwapo Israel itaamua kufanya shambulio la ardhini kaskazini mwa Gaza, na wapiganaji wa Hamas wafanye vita vya kuvizia dhidi yao kutoka kwa majengo na mahandaki waliyokalia katika eneo hilo, kunaweza kuwa na mapigano ya miezi kadhaa ambayo yanaweza kusababisha uharibifu wa eneo lote.

Makumi ya maelfu ya raia watanaswa katikati.