Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Collagen: je ni madhara gani halisi ya tembe mbadala kwa ngozi?
Na Julia Granchi
BBC News Brazil, London
Collagen, za tembe ambazo zimetengenezwa kwa umbo la kidonge cha rangi mbili, zikiwa na mchanganyiko wa poda na au zenye umbo la peremende hupatikana kwa urahisi mitandaoni na katika maduka ya vyakula vya afya kote Brazil, lakini je zina ufanisi kiasi gani?.
Ingawa ni nyongeza mbadala maarufu kwa utunzaji wa ngozi, bado haina ushahidi mzuri wa kisayansi wa kuunga mkono faida kuu inazonadi kuwa nazo: kuboresha mwonekano wa ngozi kwa kuiimarisha na kupunguza mikunjo na alama.
Collagen ni protini muhimu inayopatikana katika mwili wa binadamu, inayohusika na nguvu na kupanuka kwa tishu mbalimbali kama vile ngozi, mifupa na ute unaoonganisha mifupa.
Kadri umri unavyoenda , uzalishaji wa protini hii hupungua, na makunyanzi, alama na kusinyaa huonekana kwenye ngozi ambayo awali ilikuwa na muonekano laini na imara.
"Kutokana na kupungua huku kwa uzalishaji, viwanda hutoa tembe za virutubisho vya kumeza, vikidai kwamba kumeza tembe hizi husaidia kuchochea uzalishaji wa collagen," anaelezea Elisete Croco, mratibu wa Idara ya Vipodozi ya chama cha madaktari wa Ngozi wa Brazil.
Swali la ikiwa kumeza tembe hizi huleta faida au la ni la kawaida katika ofisi za daktari, anasema Croco.
"Jibu linaweza kuwa katika lishe sahihi na ulaji sahihi wa Amino acid kupitia vyakula. Ushahidi wa kisayansi juu ya ufanisi wa bidhaa za collagen, kwa bahati mbaya, ni nadra.
Daktari anaelezea kuwa baadhi ya tafiti zimeweza kuonyesha, kwa kutumia kipimo cha ultrasound, uboreshaji kidogo katika unene wa ngozi ya wanawake ambao walitumia bidhaa hizi.
"Lakini ni muhimu kutambua kwamba tafiti hizi zinafanywa na wenye viwanda yenyewe na mara nyingi huhusisha sampuli za wagonjwa 20 au 30 - idadi ambayo ni ndogo sana kuweza totoa matokeo ya kuaminika’’
Aina tofauti za collagen
Kuna aina tofauti za collagen. Kati ya zile kuu, tunaweza kutaja:
Aina ya 1: Inapatikana katika ngozi, mifupa, na meno, hutoa nguvu na msaada wa muundo. Katika ngozi, ni wajibu wa kudumisha uimara na uwezo wa ngozi wa kupanuka.
Aina ya 2: Inapatikana kwenye mfupa laini unaounganisha mifupa migumu ya mwili (cartilage), ina jukumu muhimu kuwezesha kupinda kwa viungo. Inachangia afya ya viungo na kuzuia uchakavu.
Aina ya 3: Inasaidia viungo vya ndani kama vile ini, wengu na utumbo. Pia hupatikana katika mishipa ya damu, ina jukumu muhimu katika kutanuka na kwa mishipa.
Aina ya 4: Sehemu ya utando (membranę) ambayo husaidia kudumisha tishu zilizo na muundo mzuri. Inafanya kama msaada kwa seli.
"Inayouzwa zaidi kibiashara ni verisol, aina ya collagen 1," anaelezea Mariele Bevilaqua, daktari wa ngozi katika Hospitali ya Moinhos de Vento mjini Porto Alegre.
Verisol imeundwa na peptidi za collagen za bioactive - vipande vidogo vya protini, ambavyo, kwa nadharia, vinaingia kwa ufanisi zaidi katika mwili.
Protini hutolewa kutoka kwa tishu zinazojumuisha za wanyama, kama vile ngozi, mifupa na mifupa laini inayounganisha mifupa migumu ya ng'ombe, nguruwe, samaki au kuku.
Ni wakati collagen ya ziada inaweza kuleta tofauti?
Dkt. Elisete Croco wa SBD anaeleza kuwa kuongeza collagen kunaweza kuwa na manufaa katika hali maalum za kimatibabu.
"Kwa kutekeleza tiba za ngozi kama vile kuondoa sehemu ya ngozi, lasers na microneedling, tunaongeza uharibifu wa miundo ya seli, ambao hudhibitiwa na hivyo kusababisha uzalishaji wa kile kinachofahamika kama neocollagenesis (ukarabati wa makovu ya mwili) . Kwa hiyo sio utaratibu yenyewe bali ni mwili, unaohusika na kuunda nyuzi mpya kwa kukabiliana na uharibifu huu.
Kwa njia hii, upatikanaji mkubwa wa protini ya collagen katika mwili ungesaidia kinadharia kuharakisha mchakato huu wa "neocollagenesis", uzalishaji wa ziada wa collagen katika mchakato wa kurejesha nyuzi za ngozi.
"Kwa wagonjwa wangu, ninashauri kuanza kuongezewa angalau mwezi mmoja kabla ya utaratibu. Kwa njia hii, ngozi itakuwa na malighafi zaidi kwa ajili ya kusisimua collagen wakati na baada ya matibabu ya urembo, "anaelezea Bevilaqua.
Daktari anasema kwamba gharama ya nyongeza inaweza kufikia R$150 kwa mwezi.
"Ni uwekezaji mkubwa. Kwa hivyo, nyongeza inapaswa kutathminiwa kwa msingi wa ngozi ya mtu na mtu.
Uwezekano mwingine wa unaofaa wa kuongezewa collagen ni katika matukio ya majeraha ya mifupa.
"Katika hali ya kujeruhiwa , hasa kwenye viungo, uongezaji wa collagen bora unaweza kuchangia ukarabati bora wa tishu ingawa ufanisi pia haujafanyiwa stadi madhubuti’’, anaongeza.
Kinga au nyongeza?
"Ni muhimu kusisitiza kwamba athari kubwa zaidi sio zile za uingiliaji kati wa wakati athari tayari zimekwishajitokeza kwa ngozi yako, la muhimu ni kuzuia athari kabla hajijatokea. Ni jambo la msingi kuanza utunzaji wa ngozi kuanzia umri mdogo, ukiwa bado katika hatua ya ujana, na kuzingatia tabia bora za kiafya za utunzani wa ngozi katika miaka 50 ya kwanza ya maisha," anasisitiza Croco.
Miongoni mwa mambo ya manufaa kwa ngozi, daktari Mariele Bevilaqua anataja kujikinga na jua, kutovuta sigara, kudumisha lishe bora, na vyakula vichache vilivyosindikwa zaidi , kunywa maji ya kutosha , na kuzingatia utaratibu mzuri wa kulala.
Na ikiwa mtu huyo tayari amegundua ishara kama vile mistari laini, mikunjo na madoa kwenye ngozi, bidhaa zenye viungo kama asidi vinaweza kujumuishwa katika utaratibu wa utunzaji wa ngozi, lakini lazima kila mtu kibinafsi afuatiliwe na daktari wa ngozi kulingana na tatizo lake.
"Chaguo ni kutumia njia zisizo za sindano. Njia bora ni kutumia teknolojia zaidi ya asili au taratibu, kwa kuwa ni mwili wenyewe unaozalisha collagen katika suala hili. Kufanya utaratibu kama vile microneedling, kwa mfano, mara mbili kwa mwaka, ikiwa dalili za uzee zinaonekana, inaweza kusaidia katika kuimarisha muonekano wa asili, "anasema Croco.