Zifahamu pikipiki za umeme zinazokabiliana na uchafuzi wa mazingira kwa njia ya kelele na hewa
Kutana na Tuktuk ama pikipiki za magurudumu matatu zinazotumia umeme zikikabiliana na uchafuzi wa mazingira kwa njia ya kelele na hewa huko Mombasa.
Mtangazaji kinara wa BBC Roncliffe Odit amepata wasaha wa kuzungumza na Mkurugenzi wa Ana Green Tech Africa Bi. Amina Ibrahim ambao ni wazalishaji wa pikipiki hizi anayeelezea namna zinavyofanya kazi na jinsi wanavyokabiliana na changamoto zilizopo za miundombinu, masoko mapya na utofauti utakaoletwa na usafiri huu.










