Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Alexis Mac Allister kuhamia Manchester United?

Alexis Mac Allister

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mchezaji wa Liverpool Alexis Mac Allister
Muda wa kusoma: Dakika 3

Manchester United inafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Argentina Alexis Mac Allister, 27, kutoka Liverpool baada ya duru kuarifu kuwa anatarajiwa kuondoka Anfield msimu huu wa joto. (Star)

Manchester City ingelipendelea kumtoa kipa Muingereza James Trafford,23, kwa mkopobadala ya kumuuza msimu huu wa joto huku vilabu vya Leeds, Aston Villa na Newcastle vikionyesha nia ya kutaka kumsajili. (Teamtalk)

Nicolas Jackson, 24, anatarajiwa kurejea Chelsea msimu huu wa joto baada ya kukosa muda wa kucheza Bayern Munich. Klabu hiyo ya Bundesliga haitaweza kuanzisha kipengele cha wajibu wa kumsajili katika mkataba wa mkopo wa mshambuliaji huyo wa Senegal. (Times - usajili unahitajika)

Arsenal imefahamishwa kwamba winga wa Uhispania Nico Williams, 23, yuko tayari kuondoka Athletic Bilbao msimu wa joto. (Team talk)

Klabu ya Brighton imemfanya Said El Mala, 19, kuwa lengo lao kuu la usajili wa majira ya kiangazi na tayari imewasilisha ofa ya kumsajili winga huyo wa Ujerumani na klabu ya Cologne aliye na umri wa chini ya miaka 21. (Sky Germany)

Manchester United imekanusha kuwasiliana na wakala wa Jurgen Klopp baada ya kusema kuwa klabu hiyo ilifanya uchunguzi kuhusu meneja huyo wa zamani wa Liverpool mwenye umri wa miaka 58 kuchukua mikoba ya Old Trafford. (Sky Sports)

Klopp

Chanzo cha picha, Getty Images

Real Madrid inapigiwa upatu kumsajili beki wa Ujerumani Nico Schlotterbeck, 26, kutoka Borussia Dortmund msimu huu wa joto huku Barcelona pia wakiwania saini yake kwa mkataba wa euro milioni 50. (Fichajes - kwa Kihispania)

Manchester United itaendelea kumfuatilia kiungo wa Middlesbrough Hayden Hackney, 23, kabla ya usajili la majira ya kiangazi, huku Leeds, Tottenham na Everton pia wakimtaka Muingereza huyo. (Team talk)

Galatasaray inataka kumsajili kiungo wa kati wa Inter Milan na Uturuki msimu wa joto Hakan Calhanoglu, 32. (La Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Mkufunzi wa Barcelona Hansi Flick anataka kuimarisha safu yake ya ulinzi kwa kumsajili beki wa pembeni wa Borussia Dortmund na Norway Julian Ryerson, 28. (Fichajes - kwa Kihispania).

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi