Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Murillo kuondoka Nottingham Forest?

Chanzo cha picha, Getty Images
Beki wa Nottingham Forest Murillo anajiandaa kukihama klabu hicho msimu huu wa joto huku Chelsea na Liverpool zikionyesha nia ya kitaka kumsajili Mbrazil huyo wa miaka 23. (Teamtalk)
Klabu ya Napoli imeanza mazungumzo na wawakilishi wa kiongo wa Scotland Scott McTominay, 29, kuhusu mpango wa kurefusha mkataba wake Italia hadi 2030. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)
Manchester City italazimika kulipa kati ya pauni mlioni 60-70 kumsajili kiungo wa kati wa England na Nottingham Forest Morgan Gibbs-White, 26, msimu wa joto. (Football Insider)
Chelsea na Tottenham wana nia ya kumsajili beki wa kati wa Bayern Munich kutoka Korea Kusini Kim Min-jae, 29. (CFBayernInsider)
Winga wa RB Leipzig wa Ivory Coast Yan Diomande, 19, ambaye amekuwa akihusishwa na uhamisho wa kwenda Liverpool, anasema klabu hiyo ya Anfield ndiyo klabu babake anaihusudu. (Bild via Goal)
Lakini meneja wa Bayern Munich Vincent Kompany anataka viongozi hao wa Bundesliga kuwashinda wapinzani wao waLigi ya Englandili kumsajili Diomande katika msimu wa joto. (Fabrizio Romano)

Chanzo cha picha, Getty Images
Everton inapanga kumsajili winga wa Wales Harry Wilson, 28, msimu wa joto baada ya Fulham kuwakatalia katika dirisha la uhamisho la Januari. (Football Insider)
Manchester United na Arsenal wana nia ya kumrejesha mshambuliaji wa AC Milan na Marekani Christian Pulisic, 27, kwenye Ligi ya Premia, huku Tottenham pia wakiwa mbiono kusaka saini yake. Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea atapatikana kwa kati ya euro milioni 70-80. (Caught Offside)
Real Madrid wanafikiria kumuuza mshambuliaji wa Brazil Endrick, 19, atakaporejea kutoka Lyon ambako amekuwa akikipiga kwa mkopo huku vilabu kadhaa vya Ligi ya Premia vikionyesha nia ya kutaka kumsajili. (Fichajes - kwa Kihispania)

Chanzo cha picha, Getty Images
Juventus wangependa kiungo wa kati wa Marekani Weston McKennie, 27, atie saini mkataba mpya, lakini mazungumzo yamekwama kwa sababu anataka mshahara wakekuongezwa maradufu, ambao kwa sasa ni kati ya euro 2.5m-3m (£2.18m-£2.6m) kwa msimu. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
Kiungo Sandro Tonali, 25, amethibitisha kujitolea kwake kwa Newcastle United kufuatia uvumi unaomhusisha na Arsenal. Muitaliano huyo alisema alikimbilia kwa meneja Eddie Howe baada ya kufunga bao kwenye Mchuano wa FA dhidi ya Aston Villa Jumamosi kwa sababu alitaka kuonyesha uhusiano wao uko imara. (ChronicleLive)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












