Qassem Basir: Fahamu Kombora jipya la Iran, Je ni kuitisha Marekani?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 4

Waziri wa ulinzi nchini Iran alizindua kombora la masafa marefu lililoboreshwa.

Uzinduzi huo unajiri huku kukiwa na vitisho kutoka kwa Marekani kuhusu mpango wake wa kinyuklia huku taifa hilo likifanya majadiliano ya makubaliano ili kutatua mzozo huo.

Kombora hilo linashirikisha uboreshaji katika mwongozo na uwezo wake wa kukwepa rada pamoja na mifumo ya ulinzi ya angani.

Kombora hilo lilifanyiwa majaribio April 17 2025.

Pia unaweza kusoma

Je, Qassem Basir ni kombora la aina gani?

Televisheni ya Iran ilielezea kombora hilo kuwa na uwezo wa kusafiri umbali wa angalau kilomita 1,200 (maili 745).

Pia ilisema kuwa kombora hilo linaweza kutambua na kupiga shabaha kati ya nyingi bila mwongozo wa GPS na kwa usahihi na kwa uhakika.

Wakati wa majaribio, uingiliaji mkubwa wa kielektroniki ulitumiwa dhidi ya kombora hilo, lakini liliendelea kuruka bila kuathiriwa.

Iran inasema kombora hilo linaweza kufika Israel na kupenya baadhi ya mifumo ya hali ya juu zaidi ya ulinzi wa makombora duniani.

Wataalamu wanasema kombora hilo la Qassem Basir ni la kwanza kutumiwa na Tehran .

Mtaalamu wa masuala ya silaha mwenye makao yake nchini Urusi Yuri Lyamin anasema kuwa kombora hilo la masafa ya kati sasa ndilo "kombora la masafa marefu zaidi" la Iran na la kielektroniki, likichukua nafasi ya kombora la masafa mafupi la Zolfaghar Basir.

Tehran ilianzisha mpango wake wa makombora ya masafa marefu baada ya kuteseka na mashambulizi ya makombora ya Scud ya Iraq katika vita vya Iran na Iraq - na kama ua dhidi ya majirani zake wenye silaha za Magharibi kwani vikwazo vimeizuia kufikia ndege za kisasa za mashambulizi.

Kuhusu uwezo wa kiulinzi wa Iran, Waziri wa Ulinzi alisema: "Tunapopata ujuzi wa kisayansi na kiufundi wa kutengeneza zana za kijeshi, yakiwemo makombora, tunazizalisha kwa wingi na kwa haraka. Vikosi vya wanajeshi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vimefikia ukomavu kamili wa kutengeneza makombora madhubuti."

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe

Iran yakanusha kuwasaidia Wahouthi kushambulia Israel

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wakati huohuo Iran imekana kutoa msaada kwa waasi wa Houthi nchini Yemen na kuahidi kujibu mashambulizi yoyote katika ardhi yake.

Haya yanajiri baada ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kutishia kushambulia Iran kujibu shambulio la kombora la Wahouthi kwenye Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion mjini Tel Aviv siku ya Jumapili.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ilisema katika taarifa yake siku ya Jumatatu kwamba "hatua ya Wayemen ya kuwaunga mkono watu wa Palestina ni uamuzi huru unaotokana na hisia zao za mshikamano" na Wapalestina.

Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Nasirzadeh alionya wakati wa kuzindua kombora jipya la masafa marefu la Iran Jumapili usiku: "Ikiwa tutashambuliwa, tutajibu kwa nguvu na kulenga maslahi na kambi zote za Marekani."

Iran inawaunga mkono Wahouthi, ambao wanadhibiti maeneo mengi ya Yemen, ukiwemo mji mkuu, Sanaa.

Kufuatia shambulio hilo, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliapa siku ya Jumapili kuanzisha "mashambulio" mapya dhidi ya Wahouthi na kuilenga Iran.

Netanyahu alisema, "Israel itajibu shambulio la Houthi kwenye uwanja wetu wa ndege mkuu kwa wakati na mahali tunapochagua (kwa kuwalenga) magaidi wakuu wa Iran,"

Kujibu vitisho hivyo, Tehran ilithibitisha Jumatatu kwamba itajibu shambulio lolote katika ardhi yake.

"Tunathibitisha azimio thabiti la watu wa Iran kujilinda," Wizara ya Mambo ya Nje ilisema katika taarifa yake, ikionya Israel na Marekani juu ya "matokeo" ya vitisho hivi.

Rais wa Marekani Donald Trump na utawala wake wamezidisha vitisho vyao dhidi ya Iran katika miezi ya hivi karibuni, wakitaja uungaji mkono wake kwa Wahouthi.

Shambulizi ambalo halijawahi kutokea katika uwanja wa ndege wa Ben Gurion siku ya Jumapili lilisimamisha kwa muda usafiri wa anga na kuwaacha watu sita kujeruhiwa kidogo, kulingana na mamlaka ya Israel.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Seif Abdalla