"Sote watatu ni wapenzi na tunalala kitanda kimoja"

Na Humpo Lakaje, BBC

Mtindo mpya unaoitwa 'Polyamory' unaibuka miongoni mwa vijana wa Afrika Kusini. Polyamory inamaanisha kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na watu wengi kwa wakati mmoja na nyote mnafahamiana na mnakubaliana na mnashiriki ngono pamoja.

Hii ni tofauti na uhusiano ama ndoa ya mitala, ambapo mwanaume anakuwa na wake zaidi ya mmoja wanaofahamiana lakini wanawake hao hawana uhusiano wa kingono.

Lethabo Mojalefa akiwa na nywele fupi, suruali ya rangi inayofanana na nguo aliyovaa juu, alianza mahusiano na Fletcher Mojlefa mnamo Desemba 2018.

Fletcher anajiamini vile vile. Anapenda kuvaa nguo za kifahari.

Wanandoa hao, ambao wana umri wa miaka ishirini na kitu, wanaishi katika eneo la vijijini katika jimbo la Limpopo nchini Afrika Kusini na mtoto wao wa kiume mwenye umri wa miaka miwili.

Walipokutana kwa mara ya kwanza, Fletcher hakujua kwamba Lithabo alikuwa na jinsia mbili.

"Nilimwambia Fletcher kuhusu suala hili baada ya miezi miwili au mitatu ya mahusiano yetu kwa sababu ndipo nilipogundua kuwa ningeweza kumueleza," Lithabo anasema.

Fletcher alikuwa mtu mzuri kwangu pia.

"Alitoka nami hadharani na nilifurahishwa na hilo," anasema Fletcher.

Wanandoa hao walitambua kwamba ikiwa uhusiano wao udumu, mahitaji ya Lithabo ya kingono na kihisia yangepaswa kutimizwa kama mwanamke mwenye jinsia mbili na Fletcher yangetimizwa na mtu wa jinsia tofauti ya yake yaani mwanamke.

Hivyo wakapata wazo la kumleta mtu wa tatu kwenye uhusiano ndipo wawili hao wakaamua kumtafuta mtu huyo kwa pamoja.

Mtu wa tatu katika uhusiano wa wawili hao

Mnamo Agosti mwaka jana, alikutana na Lunia Makua, mwanamke mwenye jinsia mbili. Anafanya kazi kama katika klabu ya usiku katika eneo moja. Yeye pia ni umri wa takribani 20.

"Tulielewana. Mambo mengi tuliyojadili yalikuwa yanatugusa. Alimpenda tangu siku ya kwanza. Nilijua alipenda wanawake wa aina hiyo," Lithabo anasema.

"Ilikuwa sawa na mimi. Kwa sababu ninafanya kitu kimoja. Mimi pia ni mpambanaji. Hiyo ndiyo iliyotukutanisha.

Lunia pia anahisi vivyo hivyo.

"Lithabo alinitongoza. Kisha tukaanza uhusiano naye. Kisha akanitambulisha kwa Fletcher. Kisha tukaingia kwenye uhusiano wote," anasema Lunia.

"Nilikuwa na hisia kwa Lithabo. Niligundua nilikuwa na hisia pia na Fletcher tulipokuwa kwenye shoo. Nilimbusu.

"Muda si mrefu sote tulijikuta pamoja. Sote watatu tulikuwa tukilala kitanda kimoja. Hasa tunapohudhuria hafla za kijamii na kulala kwenye nyumba za wageni."

Lakini, kuelewa uhusiano wa 'polyamory' daima imekuwa vigumu kwa watu katika jimbo la vijijini la Limpopo nchini Afrika Kusini.

Lithabo anakiri kwamba baadhi ya watu wa rika lake bado hawaelewi uhusiano huo. Na hii ni kawaida katika eneo hili.

"Wananiuliza inakuwaje mwenzake anapokuwa na mpenzi wake mwingine," Lithabo anasema. Ninawaeleza kuwa yeye sio tu mpenzi wake, pia nami ni penzi wakengu, ninatoka naye.

“Watu wakishagundua kuwa yeye pia ni mpenzi wangu, wananituhumu na kuniandama.

“Lakini, haijalishi kwangu. Ninajua ninachofanya na ninafahamu maamuzi ninayofanya."

Maoni haya, Fletcher anasema, yanatokana na fikra za kihafidhina za jamii.

"Hawawezi kuamini kuwa mwanamke mmoja angevutiwa na mwanamke mwingine."

Watatu hawa wanaelezea jinsi uhusiano wao unavyofanya kazi.

"Yeye si aina ya mvulana anayeweza kufanya mapenzi na yeyote anayemtaka," Lithabo anasema.

"Wote wanaweza kufanya ngono bila mimi," anasema Fletcher, akimuunga mkono Lithabo.

Ridhaa ni jambo muhimu sana katika mahusiano ya aina hii ya mpenzi zaidi ya mmoja mnaojuana, anasema Dokta Ian Opperman, ambaye ni mwanasaikolojia pia.

Anasema, "Watu wa mwelekeo tofauti wa kijinsia ni sehemu ya jamii na hujenga mtandao wa mahusiano kwa kupitia wapenzi wao.

"Kuna mambo mengi ambayo yanatofautiana katika 'polyamory' na aina nyingine za mahusiano yasiyo ya mke mmoja."

Kwa mfano, kuna watu wanatoka nje ya ndoa ama uhusiano wao. Lakini, hawatengenezi uhusiano wa kihisia na kingono kati ya mke au mume ama mpenzi wake na huyo 'mchepuko'.

Washauri wa mauhusiano hapa wanasema 'polyamory' ni ya kawaida zaidi sasa na imeenea zaidi Afrika Kusini kuliko ilivyotarajiwa.

Mara nyingi mahusiano ya watu wanaopenda aina hii ya uhusiano mara nyingi huanzia mitandaoni.

Miji mikuu kama vile Johannesburg, Cape Town na Durban imekuwa ikiandaa matukio kwa watu wa 'polyamorous' kukutana na wengine.

Hii sio kwa vijana tu bali...

Wakati kocha wa masuala ya mauhusiano Tracy Jacobs akifutilia watu waliokuja kwake, aligundua kuwa 'polyamory' sio tu inaongezeka kwa vijana.

Anasema, "Ingawa polyamory ni maarufu zaidi miongoni mwa vijana, watu wengine katika kundi la wazee pia wanaifanya.

"Aina ya watu hawa wanaojulikana kama polyamorous ni pana kabisa na hakuna umri wa wazi."

Mtaalamu mwingine wa mauhusiano Elizabeth Retief anasema mahusiano ya watu wengi pia yanavutia zaidi kwa sababu yanatoa uhuru na kutoa changamoto kwa majukumu ya asili.

"Ikiwa unaishi katika nyumba moja na mpenzi wako na mpenzi wake mwingine na mmoja wa watoto wao, majukumu yako ya kijinsia hayafanani kwa yanavyofanya ukilinganisha na monogamous (Uhusiano na mtu mmoja) au mitala ' polygamous' kwa maana ya uhusiano wa wake wengi."

Swali linaloulizwa sana kuhusu polyamory ni jinsi gani huathiri watoto?

Hasa katika mfano wa husiano huu wa Lunia, Lithabo na Fletcher.

"Nadhani mtoto wangu atakua akijua ana mama wawili. Nimeona familia zenye wake wengi ambapo mume ana wake wengi na wanakua katika eneo moja na katika nyumba moja. Kwa hivyo, nadhani kila kitu kitakuwa sawa," Lithabo anasema kuhusu Fletcher na mwanawe.

Lunia pia anakubaliana na maoni haya. Anasema ingawa yeye si mama mzazi wa mtoto wa Lithabo, anahusika katika kumlea mtoto huyo.

“Lithabo huwa ana shughuli nyingi, hivyo asipokuwepo huwa namtunza mtoto, nafikiri ipo siku nitapata mtoto pia, lakini haiwezekani kutokana na aina ya kazi ninayoifanya hivi sasa.

"Ikiwa nitapata mtoto, lazima tukubaliane. Ninahitaji kuzungumza na Lithabo kuhusu hilo. Ikiwa anaona ni sawa, tutapata mtoto."

Dk Opperman anasema kuwa aina hizi za mahusiano zinahitaji mawasiliano makini na watoto.

"Watoto katika familia zenye watu wengi wanaweza kuchanganyikiwa na hii inaweza kutokea wakati wazazi si waaminifu kuhusu asili ya uhusiano wao.

"Ukweli kwamba upendo unaweza kuonyeshwa kwa njia nyingi unaweza kuwachanganya watoto ikiwa haueleweki vizuri."

Wakati haya yakiendelea Lunia, Lithabo na Fletcher wanaweza kumwalika mtu wa nne kwenye uhusiano wao.

"Tuko tayari kuwa na mwanamke mwingine katika uhusiano. Lakini bila shaka ikiwa tu yuko tayari," anasema Lithabo.

Kwa sasa, Fletcher ndiye mwanaume pekee kwenye uhusiano na anawaheshimu wapenzi wake wote wawili, anasema.

"Wanawake wawili wanapokutana, ni wa thamani sana. Kwa hivyo nina bahati. Ninawapenda sana na niko nyuma yao kabisa.

Lakini vipi ikiwa Lithabo, mama wa mtoto wake, ataleta mwanamume mwingine kwenye uhusiano huo?

Kwa swali hili, Fletcher anasema, "Kwa hivyo sitakuwa sehemu ya uhusiano huo kwa sababu mimi ni mtu wa jinsia tofauti. Lakini kama Lithabo anataka kuwa na uhusiano mwingine na mwanamume, sijali."