Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Marubani wa Japan hawakujua ndege inawaka moto hadi walipoambiwa na mhudumu
Marubani wa ndege ya Japan iliyogongana na ndege ya walinzi wa pwani ya Japan katika uwanja wa ndege wa Tokyo Haneda hawakujua kuwa ndege yao ilikuwa inawaka moto.
Ni mhudumu wa ndege aliwafahamisha kuhusu moto huo, msemaji wa shirika la ndege la Japan aliambia BBC.
Baada ya hapo, shughuli ya kuwaokoa abiria 379 waliokuwa kwenye ndege ya Shirika la ndege la Japan nambari 516 ilifanywa kwa haraka sana.
Watu watano kati ya sita waliokuwa kwenye ndege ndogo ya walinzi wa pwani, Bombardier Dash-8, walikufa.
"Mara tu baada ya ndege kutua, rubani alihisi mshtuko wa ghafla, na kujipata akashindwa kuzuia ndege kwenye njia ya kutua. Ndege iliwaka moto wakati huo lakini marubani hawakuwa na habari hadi walipofahamishwa kuhusu tukio hilo [kupitia] mhudumu wa ndege, " msemaji wa JAL alisema.
Kulikuwa na marubani watatu na wahudumu 12 kwenye ndege hiyo wakati kisa hicho kilipotokea. Mfumo wa utangazaji wa ndege hiyo uliharibika, na kuwalazimu wahudumu kutumia sauti zao kutoa maagizo.
"Kitu cha kwanza wahudumu walifanya [baada ya kugundua kuna] baadhi ya abiria ambao waligundua kuwa ndege yao ilikuwa inawaka moto, ni kuwafanya watulie na wasisimame, jambo ambalo lingeweza kufanya kutoka kwenye kuwa ngumu sana. Mfumo wa matangazo haukuweza kutumika kwa hiyo. maagizo haya yalifanywa bila mfumo huo."
Vyombo vya habari vya Japan vimeelezea kuwa shughuli ya kuwatoa abiria kwenye ndege hiyo kuwa "dakika 18 za muujiza". Abiria waliacha mizigo yao, na kukimbilia kwenye njia za dharura ya kuteleza na kutoka kwenye ndege kabla ya kuteketezwa na moto.
"[Wakati] moshi ulipoanza kuingia ndani ya ndege hiyo na kuenea... wahudumu wa waliaanza kuwafokea abiria, [wakisema]: 'Acha vitu vyako!', 'Vua viatu vyako virefu', na kuelekeza 'Kichwa chini' ,” alisema msemaji huyo.
"Ushirikiano wao... ulikuwa [muhimu] kwa abiria wote [kuweza] kukimbilia usalama kwa haraka", waliongeza.
Mamlaka ya Japan baaadaye Jumatano kwamba ndege ya walinzi wa pwani haikuruhusiwa kupaa kwenye barabara ya Haneda. Ndege hiyo iliratibiwa kupeleka misaada katika maeneo yaliyokumbwa na tetemeko la ardhi.
Kulingana na maafisa, ndege ya JAL iliruhusiwa kutua kwenye njia ya 34R huko Haneda huku ndege ya walinzi wa pwani ikiambiwa "isubiri kwenye eneo la C5" - mahali ambapo ndege zinangojea kibali cha kuingia kwenye njia ya ndege kuruka na ilikuwa- imezimwa.
Nakala za mawasiliano zinaonyesha ndege ya walinzi wa pwani iliitikia wito kutoka kwa waongoza usafiri wa anga - maelekezo yake wa mwisho inaonesha kabla ya mgongano.
Nakala hizo zinaonekana kukinzana na usemi wa rubani wa walinzi ya pwani - aliyenusurika kati ya wafanyakazi sita waliokuwa ndani ya ndege hiyo - ambaye aliwaambia wachunguzi kwamba alikuwa amepewa ruhusa ya kuingia kwenye njia ya ndege kuruka wakati ndege ya JAL ilikuwa inakaribia.
BBC pia imepata habari zinazodokeza kwamba mfumo wa taa kwenye sehemu husika huenda haukuwa ukifanya kazi. Lakini wataalam wanadokeza kuwa kuna viashiria vingine kama vile alama zilizopakwa rangi ambazo zingeonyesha ni wapi ndege zinahitajika kusimama kando ya njia ya kurukia.
Mnamo 2016, ndege ya Emirates Boeing 777 ilitua kwa dharura mjini Dubai na kanda za video zilionyesha matukio ya vurugu huku abiria wakijaribu kuchukua mizigo yao walipokuwa wakikimbilia slaidi za dharura. Wafanyakazi hao walisifiwa kwa jitihada zao za kuwaokoa abiria, na kwa bahati nzuri wote 300 waliokuwa kwenye ndege hiyo walinusurika.
Tukio la Jumanne ni ajali ya kwanza kubwa iliyohusisha Airbus A350, mojawapo ya aina mpya ya ndege iliyoundwa kwa nyenzo za hali ya juu kama vile plastiki iliyoimarishwa na nyuzi za kaboni.
Watengenezaji wa ndege hiyo wanapeleka timu ya wataalamu kusaidia katika uchunguzi wa Bodi ya Usalama ya Usafiri wa anga ya Japan.
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi