Nasa: Binadamu wanaweza kuishi mwezini kwa muda mrefu

Na Rob Corp

Sunday with Laura Kuenssberg

.

Chanzo cha picha, NASA

Maelezo ya picha,  Chombo Orion kinaonekana kikielekea Dunia

Wanadamu wanaweza kukaa kwenye Mwezi kwa muda mrefu katika muongo huu, afisa wa Nasa ameambia BBC.

Howard Hu, ambaye anaongoza mpango wa vyombo vya anga vya juu vya Orion kwa shirika hilo, alisema makazi yatahitajika kusaidia misheni ya kisayansi.

"Aliiambia kipindi cha Sunday with Laura Kuenssberg kwamba uzinduzi wa roketi ya Artemis siku ya Jumatano, iliyobeba chombo Orion, ilikuwa "siku ya kihistoria kwa safari ya anga ya juu ya binadamu".

Chombo Orion kwa sasa kiko umbali wa kilomita 134,000 (maili 83,300) kutoka kwa Mwezi.

Roketi ya Artemis yenye urefu wa mita 100 ililipuka kutoka Kituo cha Anga cha Kennedy kama sehemu ya dhamira ya NASA kuwarejesha wanaanga kwenye satelaiti ya Dunia.

Juu ya roketi hiyo ni chombo cha anga za juu cha Orion ambacho, safari hii ya kwanza, hakina watu lakini kimeundwa kwa namna ambayo kitasajili athari za safari hiyo kwenye mwili wa binadamu.

Safari ya ndege ya Jumatano ilifuatia majaribio mawili ya awali ya uzinduzi mnamo mwezi Agosti na Septemba ambayo yalikatizwa dakika za mwisho kwa sababu ya matatizo ya kiufundi.

.

Chanzo cha picha, NASA

Maelezo ya picha, Howard Hu ndiye anayesimamia chombo cha anga za juu cha Orion
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Bw Hu alimwambia Laura Kuenssberg kwamba kutazama Roketi ya Artemis akinyanyuka ni "hisia ya ajabu" na

"ndoto".

" Ni hatua ya kwanza tunayochukua kwa uchunguzi wa muda mrefu wa anga za juu, sio tu kwa Marekani lakini kwa ulimwengu," alisema.

"Na nadhani hii ni siku ya kihistoria kwa NASA, lakini pia ni siku ya kihistoria kwa watu wote wanaopenda safari ya anga ya binadamu na uchunguzi wa kina wa anga.

"Namaanisha, tunarudi kwenye Mwezi, tunafanya kazi kuelekea mpango endelevu na hili ndilo gari litakalobeba watu litakalotua tena Mwezini tena."

Bw Hu alieleza kuwa ikiwa roketi ya sasa ya Artemis ingefaulu basi inayofuata itakuwa na wafanyakazi, ikifuatiwa na ya tatu ambapo wanaanga wangefanikiwa kutua Mwezini tena kwa mara ya kwanza tangu Apollo 17 miaka 50 iliyopita mnamo Desemba 1972.

Ujumbe wa sasa ulikuwa unaendelea vizuri, aliiambia BBC, na mifumo yote ikifanya kazi na timu ya misheni hiyo ikijiandaa kwa kurusha tena chombo Orion ( kinachojulikana kama ‘burn’) wakati wa kurusha roketi siku ya Jumatatu mchana ili kuweka chombo kwenye obiti ya mbali ya Mwezi.

Bwana Hu alikiri kuwa kutazama misheni kutoka duniani hakukuwa tofauti na kuwa mzazi mwenye wasiwasi, lakini alisema kuona picha na video zikirudi kutoka Orion "kweli inatoa hisia ya msisimko, wow, kwamba tunarudi kwenye Mwezi".

Mojawapo ya awamu muhimu zaidi ya misheni ya roketi ya Artemis I ni kurudisha chombo cha Orion Duniani kwa usalama.

Itaingia tena kwenye angahewa ya sayari kwa kasi ya 38,000km/h (24,000mph), au mara 32 ya kasi ya sauti na ngao iliyo upande wake wa chini itakabiliwa na halijoto inayokaribia 3,000C.

.

Mara tu usalama wa vipengele na mifumo ya Artemi imejaribiwa na kuthibitishwa, Bw Hu alisema mpango ulikuwa kuwa na wanadamu wanaoishi kwenye Mwezi "katika muongo huu".

Sehemu kubwa ya sababu ya kurejea Mwezini ni kugundua kama kuna maji kwenye ncha ya kusini ya satelaiti, aliongeza, kwa sababu hiyo inaweza kubadilishwa ili kutoa mafuta ya roketi kwa zinazokwenda zaidi kwenye anga – kwa Mirihi, kwa mfano.

"Tutakuwa tukituma watu na watakuwa wakiishi huko na kufanya sayansi," Bw Hu alisema.

"Kwa kweli itakuwa muhimu sana kwetu kujifunza kidogo zaidi ya mzunguko wa Dunia yetu na kisha kupiga hatua kubwa tunapoenda kwenye sayari ya Mihiri yaani Mars."

"Na misheni ya Artemi inatuwezesha kuwa na jukwaa endelevu na mfumo wa usafiri unaotuwezesha kujifunza jinsi ya kufanya kazi katika mazingira hayo ya anga za mbali."

Chombo cha Orion kinatarajiwa kurudishwa Duniani tarehe 11 Desemba.