Huu ni ugonjwa gani unaomfanya mtu kuwa kama amekunywa pombe

Ingeweza kutokea mara mbili hadi tatu kwa wiki.

Nick Carson angeanza kunung’unika kisha akawa anapunguza taratibu.

Mazungumzo yake yangejirudia mwishowe alipitiwa na usingizi mzito.

Baba wa watoto wawili alikuwa akionyesha dalili zote za ulevi.

Ila Carson hakuwa amekunywa pombe yoyote.

Ulevi wake unaoonekana, hata hivyo, ulifuatana na dalili nyingine - maumivu ya tumbo, kuvimbiwa na uchovu.

Mara nyingi angekuwa mgonjwa na kuzimia.

Ilitokea kwa mara ya kwanza karibu miaka 20 iliyopita wakati familia yake iligundua kuwa alianza kuwa na matukio ya kuchanganyikiwa kiakili.

"Kabla ya hapo sikuwahi kumuona amelewa," asema mke wa Carson, Karen.

Carson mwenyewe angeweza tu kukumbuka matukio ya vipindi hivi kwa umbali siku iliyofuata.

"Sikuwa hat ana kidokezo ya kile kilichotokea," anasema Carson mwenye umri wa miaka 64, anayeishi Lowestoft, Suffolk, nchini Uingereza.

"Saa sita hadi nane baadaye ningeamka kana kwamba hakuna kitu kibaya kwangu, mara chache sana nilihisi uchovu."

Hatimaye Carson na mkewe walipata ulevi na dalili nyingine zilionekana kuchochewa baada ya kula vyakula vilivyokuwa na wanga nyingi kama vile viazi.

Baada ya ziara nyingi kwa madaktari na wataalamu wa lishe, Carson aligunduliwa na ugonjwa adimu unaoitwa Auto-Brewery Syndrome.

Ugonjwa wa Auto-Brewery (ABS), ambao pia hujulikana kama gut fermentation syndrome (GFS), ni hali ya kushangaza ambayo huongeza viwango vya pombe katika damu na hutoa dalili za ulevi wa pombe kwa wagonjwa, hata kama wamekunywa kidogo au kutokunywa pombe.

Inaweza kuwapelekea kushindwa kufanya majaribio ya kidhibiti hewa, na kuleta madhara ya kijamii na kisheria kwa wanaougua.

Lakini jambo hili lisilo la kawaida pia lina utata mkubwa, kwa sababu sababu halisi bado haijulikani vizuri.

Licha ya hayo, hali hiyo pia imekuwa ikitumika kama utetezi wa kisheria katika kesi za kuendesha gari wakiwa walevi.

"Nadhani wataalamu wengi wa sumu katika hatua hii wangekubali kwamba hii ni hali halisi ya matibabu na unaweza kufikia viwango cha juu cha pombe kutokana na uchachushaji wa ndani," anasema Barry Logan, mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Utafiti na Elimu ya Sayansi ya Uchunguzi huko Philadelphia.

"Sote tunazalisha kiasi kidogo cha pombe kutokana na uchachushaji lakini kwa watu wengi, viwango hivyo ni vidogo sana kuweza kupimwa. "

Kwa kawaida uchachushaji wowote unaotokea kwenye utumbo huondolewa kabla ya kuingia kwenye mkondo wa damu - athari inayojulikana kama metaboli ya njia ya kwanza.

"Ikiwa mtu ana ugonjwa huu, itabidi awe anazalisha pombe kwa kiwango ambacho kinazidi kile kinachoweza kuondolewa katika njia ya kwanza," anasema Logan.

Mbinu moja iliyopendekezwa inayosababisha hali hiyo inahusu kukosekana kwa usawa katika vijidudu vya utumbo, ambavyo husababisha kukua kwa vijiumbe fulani ambavyo baadaye, chini ya hali fulani, huchachisha mlo wenye kabohaidreti na kuwa pombe.

Hivi majuzi tofauti mpya ya hali hii - inayoitwa urinary ABS au "bladder fermentation syndrome" yaani "uchachishaji wa njia ya kibofu" - imepatikana kutokea kwa sababu ya kutofautiana kati ya vijidudu wanaoishi kwenye kibofu cha mkojo na kusababisha pombe isiyojulikana katika mkojo.

(Hali hii imeonekana kwa wagonjwa wa kisukari, ambayo isipodhibitiwa husababisha sukari kwenye mkojo ambayo vijiumbe maradhi vinaweza kula), Lakini ni nini kinachoweza kuchochea mabadiliko haya ya ghafla na makubwa katika vijidudu wanaoishi ndani ya miili yetu na kusababisha ugonjwa waABS?

Ingawa ABS imepatikana kwa watu wenye afya njema, kiwango kikubwa cha maambukizi kinaripotiwa kwa watu wanaougua magonjwa yanayoambatana na ugonjwa wa kisukari, ugonjwa wa ini unaohusiana na unene kupita kiasi, ugonjwa wa Crohn, (ugonjwa wa kufura kwa utumbo kunako sababisha kuvimba kwa muda mrefu kwa njia ya mfumo wa utumbo, ambayo hutoka kwenye tumbo lako hadi kwenye sehemu ya kutoa haja kubwa), upasuaji wa awali wa matumbo, (uwezo wa kuharibika wa njia ya kupitisha chakula au gesi kupitia utumbo lakini bila dalili yoyote ya kizuizi), au ukuaji wa bakteria wa utumbo mdogo.

Kesi za kwanza zilizoripotiwa za ugonjwa huu zilionekana nchini Japani mapema miaka ya 1950, na kumekuwa na maoni kwamba idadi ya watu wa Japani huathirika sana.

Watafiti wengine wamependekeza kuwa tofauti fulani ya maumbile ambayo hupunguza uwezo wa ini kuvunja ethanol, inaweza kuchangia kuenea kwa hali hiyo katika baadhi ya watu, kama vile Wajapani.

Kimsingi inamaanisha kuwa watu walio na lahaja hii hawawezi kusafisha miili yao ya pombe, kwa hivyo uchachushaji wowote kwenye utumbo unaweza kusababisha viwango vya ethanoli kukusanyika.

Lakini ripoti ya matibabu ya kesi mbili kutoka 1984 ilionyesha mwathirika mwingine - chachu inayoishi katika njia ya utumbo ya wagonjwa.

Madaktari katika Shule ya Tiba ya Chuo Kikuu cha Hokkaido waliripoti jinsi muuguzi mwenye umri wa miaka 24 ambaye hapo awali alikuwa na afya njema, kwa muda wa miezi mitano, alipata dalili za kizunguzunguna kujisikia mchovu kwa ujumla, kichefuchefu na kutapika saa moja hadi mbili baada ya kula chakula cha wanga.

Siku moja, saa mbili baada ya kifungua kinywa chake, alilalamika kizunguzungu, kupoteza fahamu na akahitaji kulazwa hospitalini.

Mkusanyiko wa ethanoli katika pumzi na damu yake ulionekana kuwa juu sana, ingawa hakuwa ametumia pombe yoyote.

Uchunguzi wa kimaabara ulibaini alikuwa ameongeza idadi ya chachu ya Candida albican kwenye utumbo wake.

Ingawa chachu hii hupatikana kati ya vijidudu kwenye utumbo wa mwanadamu, ilikuwa imetoka kudhibitiwa.

Uchunguzi kama huo kwenye kisa cha pili cha utafiti huo, mpishi mwenye umri wa miaka 35 ambaye alilalamika juu ya harufu ya pombe kwenye pumzi, pamoja na uoni hafifu na mwendo wa kusuka wakati anatembea, pia aligunduliwa kuwa na viwango vya juu vya Candida albican kwenye utumbo wake.

Uchunguzi wa kimaabara juu ya chachu kutoka kwa wagonjwa wote wawili ulionyesha walikuwa wakichachusha wanga hadi inakuwa pombe.

Watafiti wakati huo walipendekeza kwamba Candida ya kawaida katika matumbo ya wagonjwa wao ilikuwa imetoka nje ya udhibiti na kuanza kunyunyiza wanga kutoka kwa milo yao.

Wakati wagonjwa walikula wanga nyingi, viwango vya pombe katika miili yao viliongezeka ipasavyo.

Muuguzi na mpishi walipopewa dawa ya kuzuia fangasi na wanga katika lishe yao ikakatazwa, dalili za ulevi zilitoweka kabisa.

Hivi majuzi, tafiti zingine zimefunua kuwa mara nyingi huchukua mchanganyiko wa sababu kadhaa ili kuongeza hatari ya ABS.

Idadi ya fangasi na bakteria wanaozalisha pombe katika njia ya utumbo, lakini pia njia ya mkojo kwa baadhi ya wagonjwa wa kisukari, wanaweza kusababisha uzalishwaji wa pombe kupita kiasi.

Wengi wa spishi zinazohusika ni chachu ya Candida, ikiwa ni pamoja na Candida albican, Candida kefyr, na Candida galbrata, lakini pia Saccharomyces cerevisiae, chachu inayotumika katika kutengeneza mvinyo na kutengeneza pombe, na bakteria ya utumbo inayoitwa Klebsiella pneumoniae.

Peke yake, viwango visivyo vya kawaida vya vijidudu hivi kwenye matumbo ya wagonjwa vinaweza kusababisha ugonjwa wa ABS.

Kula vyakula vyenye wanga nyingi huchangia dhahiri, kwani huwapa vijidudu malighafi nyingi kugeuza kuwa pombe.

Watu wenye matatizo ya utumbo ambao husababisha chakula kudumaa katika njia yao ya usagaji chakula pia huathirika hasa na ugonjwa wa ABS kwani inaweza kubadilisha mazingira ya tumbo kwa njia zinazopendelea vijidudu vinavyozalisha pombe.

Kuwa na uvumilivu mdogo wa pombe kunaweza pia kuwa na jukumu, kwani pombe inayozalishwa na vijidudu ina athari kubwa kwa mwanadamu anayezihifadhi.

"Matibabu na utambuzi wa ugonjwa wa ABS umepata maendeleo makubwa katika muongo uliopita," anasema Barbara Cordell, mtafiti katika Chuo cha Panola, Carthage, Texas, ambaye anasoma kuhusu ugonjwa wa ABS na pia ni rais wa shirika lisilo la faida la Taarifa na Utafiti wa Auto-Brewery.

Lakini ni nini hasa kinachoweza kusababisha ukosefu wa usawa wa vijidudu na kusababisha spishi nyingi zenye uwezo wa kuchachusha pombe imekuwa ngumu zaidi kubaini.

"Tunazungumza kuhusu maambukizo makubwa hapa na ABS - mara nyingi kiasi cha chachu inayochachusha na bakteria kuliko kwa mtu mwenye afya," anasema Cordell.

"Inazidi mfumo kama vile maambukizo mengine ya nje ya udhibiti."

Matumizi ya mara kwa mara au ya muda mrefu ya viuavijasumu yamependekezwa kuwa sababu ya hatari, kwani mara nyingi huripotiwa na wagonjwa wanaougua hali hiyo, au kwamba wanaweza kuugua tena baada ya kupata matibabu.

Hii inaweza kuwa na maana fulani kwani matumizi mengi ya viuavijasumu kwa ujumla yanajulikana kukasirisha vijidudu vya utumbo, lakini utafiti zaidi unahitajika ili kudhibitisha ikiwa hii ndiyo husababisha moja kwa moja ugonjwa wa ABS.

Kula sana aina mbaya za vyakula kunaweza pia kuwa na sababu.

Matumizi ya kupita kiasi ya vyakula vilivyosindikwa zaidi pia yamehusishwa na kukasirisha vijidudu vya utumbo.

Pia tunajua kuwa sehemu kubwa ya matibabu lazima iwe chakula cha chini cha kabohaidreti iwe mtoa huduma na mgonjwa wataamua kutumia dawa au la," anasema Cordell.

Kwa upande wa Saccharomyces cerevisiae na Candida albican, vijidudu hivi vya utumbo vinajulikana kukua vyema na kutoa ethanoli zaidi katika hali ya asidi kidogo, kwa pH ya karibu 5-6.

Kwa kawaida, pH ya tumbo ni [asidi kali] kati ya 1.5-3.5," anasema Ricardo Dinis-Oliveira, mtaalamu wa sumu katika Chuo Kikuu cha Cooperativa de Ensino Superior Politécnico e Universitário nchini Ureno.

"Wakati wowote chakula kinapoingia ndani, hata hivyo, pH yake hupanda zaidi na [kupunguza tindikali].

Katika hali ya watu wanaosumbuliwa na hali ambayo husababisha kudumaa kwa chakula hii ina maana kwamba pH ya tumbo itakaa katika viwango hivyo vya juu kwa muda mrefu, ambayo inaweza kusaidia pH kwa vijidudu vinavyohusika na kutengeneza ethanol.