Gari linalopaa la Model A: Tunakoelekea dunia haitahitaji kuwa na barabara

Katika hafla ya uzinduzi katika Chuo Kikuu cha Draper huko San Mateo, California, kampuni moja ya utengenezaji magari ulieleza namna gari lake linavyotarajia kupaa.

Kampuni hiyo ya Alef iko kwenye mchakato wa kutengeneza garindege lake la umeme, Model A, kama gari la kwanza la kweli la linalopaa - gari ambalo inatumaini litaonekana kama gari la umeme lakini linaweza kupaa wima, na linaweza kuruka juu kwa umbali wa kilomita 110 ( maili 68).

Kampuni hiyo inatarajia kushindana katika soko linalomilikiwa na wapinzani waliobobea, kama vile AirCar na Pal-V gyrocopter ambayo tayari yana magari yanayoendeshwa na kupaa kama ndege.

Lakini Jim Dukhovny, mtendaji mkuu wa Alef na mwanzilishi mwenza, anasema magari mengi yaliyopo sasa sio magari yanayopa kabisa kwa maoni yake. "Gari linalopaa lazima liwe gari, ambayo ina maana kwamba linaweza kuendeshwa kwenye barabara ya kawaida, kuegesha katika maegesho ya kawaida ya maegesho. Na pia linapaswa kupaa wima," aliiambia BBC.

"Iwapo unahitaji uwanja wa ndege ili kuruka, unatatua tatizo gani? Na kwa nini hili ni gari la kupaa?"

Muundo wa kujigeuza ili kuweza kuruka

Sehemu ya juu ya nje ya gari hili la Model A inayofanana na gari la kawaida inajengwa na wavu ili hewa iweze kupita hadi kwenye propela nane zilizo ndani ambazo husaidia kuinyanyua.

Lakini kuruka umbali wowote kwa kutumia propela peke yake, bila usaidizi wa mabawa, kungehitaji nguvu nyingi sana.

Suluhisho lililopendekezwa la Alef ni kama riwaya - kwa safari ndefu za ndege Model A hubadilika kuwa ndege.

Baada ya kuinuka wima, Model A itageuka na kurudi kawaida, chumba cha marubani cha watu wawili kinazunguka ili dereva abaki akitazama mbele, na gari linakuwa ndege na pande ndefu za gari zikiunda mabawa ya juu na ya chini.

Umbo la kawaida la ndege, lenye mabawa mawili, moja juu ya lingine, ni rahisi kuona katika Mfano A ikiwa unafikiria matundu katikati ya pande dhabiti yakiondolewa. Alef pia imetoa video inayoonyesha mabadiliko hayo.

Forbes inaona kwamba namna ingeruka inafanana na Opener Blackfly, ndege ya umeme inayopaa wima. Ni wazo la busara, lakini ni la vitendo?

Kuifanya gari kuruka na kuendeshwa kwa pamoja huongeza uzito, nguvu ya umeme pia inamaanisha uwe na betri kubwa yenye nguvu kubwa.

"Muundo huo uko kwenye ukingo wa kile ambacho fizikia na teknolojia inaweza kufanya, na ungetarajia iwe," asema mhandisi wa anga Profesa Steve Wright wa Chuo Kikuu cha West of England.

Vikwazo vya kiufundi kimoja wapo ni kuwa na barabara maalumu angani zenye magari mengi yanayoruka. Kama ilivyo kwa ndege kwa sasa.

Udhibiti na uidhinishaji wa magari yanayoruka huenda ukawa mkali, unaotumia muda mwingi na wa gharama kubwa, kama ilivyo kwa ndege yoyote.

Ili kurusha gari hili, hata moja ambalo unaweza kuendesha barabarani, itahitaji leseni ya marubani - ingawa Bw Dukhovny anafikiria kwamba kwa safari fupi za kiwango cha chini juu ya vizuizi kwa kutumia safari ya wima, leseni inayotumiwa kwa waendeshaji wa drone inaweza kutosha.

Na mamlaka ina uwezekano wa kuweka sheria kali juu ya wapi magari yanaweza kusafirishwa.

"Tunakoelekea hatutahitaji barabara"

Kwa sababu hizi na nyinginezo, Prof Wright anadhani mustakabali wa magari yanayoruka hautakuwa gari moja ambalo watumiaji wanamiliki, kuendesha na kupaa nalo.

Katika filamu ya Back to the Future, gari la DeLorean linaloendeshwa na mhusika Doc Brown linaacha njia na kuruka hewani.

"Hivyo sivyo usafiri mkubwa wa anga utakavyokuwa, ambayo ni aibu sana. Kwa kweli nataka kuwa na DeLorean yangu ya kuruka kweli kama mtu mwingine yeyote angetaka," Prof Wright anasema.

Kwa kweli, kusafiri kwa gari linaloruka, Prof Wright anasema, itakuwa kama kukodisha teksi. "Unatooa simu yako, na gari lingesogea na lingekupeleka mahali pa ukubwa wa bustani ndogo na ndege isiyo na rubani inashuka, inatua chini, unaondoka. Kwa hiyo, kwa maneno mengine, unaiita teksi isiyo na rubani."

Makampuni mengi yanatengeneza ndege zisizo na rubani za abiria.

Hivi majuzi, kampuni ya Uchina ya Xpeng ilitoa onyesho lake la kwanza la hadhara la gari lake la X2 huko Dubai.

Lakini Bw Dukhovny anaamini sana kwamba wazo la kuwa na gari lenye uwezo wa kuendeshwa na kuruka kwa wakati mmoja ni la kuvutia.

BBC ilipomuuliza nani atakayeweza kulipa bei ya awali ya kununua Model A ya $300,000 (£266,000), anasema "watu wanaopokea mabadiliko mapema".

Anasema watu wamekuwa wakingojea gari linaloruka au kupaa kwa miaka 100. Lengo kuu la Alef ni kuanza kuuza magari hayo mnamo mwaka 2025.