Kwa nini wanaume hawa wa Israel walijitolea kupigana, lakini sasa wanakataa kurudi Gaza?

Mwanajeshi
Muda wa kusoma: Dakika 6

Kila mtu katika kikosi chake alijua mtu aliyeuawa. Yuval Green, 26, alijua takribani watu watatu. Alikuwa askari wa akiba, daktari katika askari wa miavuli wa Jeshi la Ulinzi la Israeli, aliposikia habari za kwanza za shambulio la tarehe 7 Oktoba la Hamas.

"Israel ni nchi ndogo. Kila mtu anamjua mwenzake,” anasema. Katika siku kadhaa za ghasia, watu 1,200 waliuawa, na wengine 251 kutekwa nyara huko Gaza. Mateka 97 wamesalia huko Gaza, na karibu nusu yao wanaaminika kuwa hai.

Yuval alijibu mara moja wito wa nchi yake kwa kubeba silaha. Ilikuwa ni misheni ya kuwatetea Waisraeli. Anakumbuka hofu ya kuingia katika jumuiya za Wayahudi zilizoharibiwa karibu na mpaka wa Gaza. "Unaona ... maiti mitaani, kuona magari yamechomwa na risasi."

Wakati huo, hakukuwa na shaka juu ya kuripoti kazini. Nchi ilishambuliwa. Ilibidi mateka waletwe nyumbani.

Kisha yakaja mapigano katika Gaza yenyewe. Vitu vilivyoonekana ambavyo haviwezi kuonekana. Usiku aliona paka wakila mabaki ya binadamu katika barabara.

"Anza kufikiria, kama apocalypse. Unatazama kulia kwako, unatazama kushoto kwako, unachoona ni majengo yaliyoharibiwa, majengo ambayo yameharibiwa na mashambulizi ya makombora, kila kitu. Hiyo ndiyo Gaza sasa hivi.”

Baadaye, kijana aliyeripoti kazini tarehe 7 Oktoba anakataa kupigana.

Yuval Green ni miongoni mwa wale wanaokataa kuendelea na mapigano huko Gaza

Yuval ndiye mratibu mwenza wa barua ya umma iliyotiwa saini na zaidi ya 165 , katika hesabu ya hivi karibuni, askari wa akiba wa Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF), na idadi ndogo ya wanajeshi wa kudumu, wanaokataa kuhudumu, au kutishia kukataa, isipokuwa mateka kurudishwa, jambo ambalo linahitaji mpango wa kusitisha mapigano na Hamas.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Katika nchi ambayo bado imeumizwa na ghasia mbaya zaidi katika historia yake, wale wanaokataa kwa sababu za dhamiri ni wachache katika jeshi ambalo linajumuisha askari wa akiba wapatao 465,000.

Kuna sababu nyingine ya kuchoka kwa wanajeshi wengine wa akiba wa IDF.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya Israel, idadi inayoongezeka wanashindwa kuripoti kazini.

Gazeti la The Times of Israel na vyombo vingine kadhaa vilinukuu vyanzo vya kijeshi vikisema kwamba kulikuwa na shauku kwa kati ya 15% hadi 25% ya wanajeshi waliojitokeza, haswa kutokana na uchovu na muda mrefu wa huduma wanayohitajika kutoa.

Hata ikiwa hakuna uungwaji mkono mkubwa wa umma kwa wale wanaokataa kutumikia, kuna uthibitisho kwamba baadhi ya matakwa muhimu ya wale waliotia sahihi barua ya kukataa zinaungwa mkono na idadi inayoongezeka ya Waisraeli.

Kura ya maoni ya hivi karibuni ya Taasisi ya Demokrasia ya Israel (IDI) ilionesha kuwa kati ya Wayahudi wa Israel 45% walitaka vita viishe, kwa kusitishwa kwa mapigano kuwarudisha mateka nyumbani, dhidi ya 43% ambao walitaka IDF ipigane ili kuisambaratisha Hamas.

Jambo muhimu ni kwamba, kura ya maoni ya IDI pia inapendekeza kwamba hisia ya mshikamano ambayo iliashiria siku za mwanzo za vita wakati nchi hiyo ikirudi kutoka kwenye kiwewe cha Oktoba 7 imeondolewa na migawanyiko ya kisiasa: 26% tu ya Waisraeli wanaamini kuwa sasa kuna hisia ya umoja, wakati 44% wanasema hakuna.

Ripoti zinaonesha kupungua kwa wanajeshi wa Israel wanaoripoti kazini

Chanzo cha picha, Getty Images

Hata Waziri wa zamani wa Ulinzi, Yoav Gallant, mwanachama wa Chama cha Likud cha Netanhayu, aliyefukuzwa kazi na waziri mkuu mwezi uliopita, alitaja kushindwa kuwarudisha mateka hao ikiwa moja ya sababu ya kutoelewana na mkuu wake.

"Kuna na hakutakuwa na upatanisho wowote kwa kuwaacha wafungwa," alisema. "Itakuwa alama ya Kaini kwenye paji la uso la jamii ya Israeli na wale wanaoongoza njia hii potofu."

Netanyahu, ambaye pamoja na Gallant wanakabiliwa na hati ya kukamatwa kutoka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa tuhuma za uhalifu wa kivita, amekanusha mara kwa mara na kusisitiza dhamira yake ya kuwaachilia mateka.

The seeds of refusal

Kukataa kwa Yuval kulianza katika siku chache baada ya vita kuanza. Kisha naibu spika wa Knesset (bunge la Israeli), Nissim Vaturi, alitoa wito kwa Ukanda wa Gaza "kufutwa kutoka kwenye uso wa Dunia". Rabi mashuhuri Eliyahu Mali, akimaanisha kwa ujumla Wapalestina katika Gaza, alisema: “Usipowaua, watakuua.” Rabi huyo alisisitiza kwamba askari wanapaswa kufanya tu kile ambacho jeshi liliwaamuru, na kwamba sheria ya serikali haikuruhusu mauaji ya raia.

"Watu walikuwa wakizungumza juu ya kuua wakazi wote wa Gaza, kana kwamba ni aina fulani ya wazo la kitaaluma ambalo lina maana ... . Na askari hufanya mambo mengi."

Kumekuwa na machapisho kwenye mitandao ya kijamii kutoka kwa wanajeshi huko Gaza wakiwadhulumu wafungwa, kuharibu mali, na kuwakejeli Wapalestina, ikiwa ni pamoja na mifano mingi ya askari waliopiga picha na mali za watu, ikiwa ni pamoja na nguo za wanawake na nguo za ndani.

"Nilikuwa nikijaribu kupambana na hilo wakati huo kadiri niwezavyo," asema Yuval. "Kulikuwa na hali nyingi za udhalilishaji, hali ya kulipiza kisasi."

Maelfu ya Wapalestina wamekimbia makazi yao

Chanzo cha picha, Getty Images

Mabadiliko yake binafsi yalikuja na agizo ambalo hangeweza kutii.

“Walituambia tuchome nyumba, nami nikaenda kwa kamanda wangu na kumuuliza: ‘Kwa nini tunafanya hivyo?’ Na majibu aliyonipa hayakuwa mazuri. Sikuwa tayari kuchoma nyumba bila sababu za maana, bila kujua kwamba hii inatumika kwa madhumuni fulani ya kijeshi, hivyo nikakataa na kuondoka.”

Hiyo ilikuwa siku yake ya mwisho huko Gaza.

Kwa kujibu, IDF iliniambia kwamba hatua zake "zilitokana na hitaji la kijeshi, na kwa mujibu wa sheria za kimataifa" na kusema Hamas "ilificha mali zao za kijeshi katika maeneo ya kiraia kinyume cha sheria".

Watatu kati ya waliokataa wamezungumza na BBC. Wawili walikubali kutaja majina yao, huku wa tatu akiomba kutotajwa kwa sababu aliogopa madhara.

'Watu walizungumza kuhusu unyanyasaji au mauaji'

Mwanajeshi mmoja, ambaye aliomba kutotajwa jina, alikuwa katika uwanja wa ndege wa Ben Gurion wa Tel Aviv wakati habari zilipoanza kuja kuhusu mashambulizi ya Hamas.

Anakumbuka alihisi mshtuko mwanzoni. "Nakumbuka nikirudi nyumbani ... redio inawaka na watu [wanapiga], wakisema: 'Baba yangu alitekwa nyara, nisaidie. Hakuna anayenisaidia.’ Kwa kweli ilikuwa ndoto mbaya sana.”

Huu ndio wakati ambapo IDF ilitengenezwa, alihisi. Haikuwa kama kufanya uvamizi wa nyumba katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa au kuwakimbiza vijana wanaorusha mawe. "Labda kwa mara ya kwanza nilihisi kama nilijiandikisha katika ulinzi wa kweli."

Lakini msimamo wake ulibadilika kadiri vita vikiendelea. "Nadhani sikuhisi tena ningeweza kusema kwa uaminifu kwamba kampeni hii ilijikita katika kuokoa maisha ya Waisraeli."

Heshima kwenye eneo la tamasha la Nova

Chanzo cha picha, Reuters

Anasema hii ilitokana na alichokiona na kusikia miongoni mwa makomredi. “Ninajaribu kuwa na huruma na kusema, ‘Hivi ndivyo inavyowapata watu waliosambaratishwa na vita…’ lakini ilikuwa vigumu kupuuza jinsi hotuba hii ilivyokuwa pana.”

Anakumbuka jinsi makomredi walivyokuwa wakijisifu, hata kwa makamanda wao, kuhusu kuwapiga "Wapalestina wasio na msaada". Na alisikia mazungumzo zaidi ya kusisimua. "Watu walizungumza kwa utulivu kuhusu kesi za unyanyasaji au hata mauaji, kana kwamba ni ufundi, au kwa utulivu wa kweli. Bila shaka hilo lilinishangaza sana.”

Askari huyo pia anasema alishuhudia wafungwa wakifumbwa macho na kutoruhusiwa kuhama “kwa muda wote wa kukaa… na kupewa kiasi cha chakula ambacho kilikuwa cha kushangaza”.

Wakati ziara yake ya kwanza ya kazi ilipomalizika aliapa kutorejea.

IDF ilinielekeza kwa taarifa ya Mei mwaka jana ambayo ilisema unyanyasaji wowote wa wafungwa ulipigwa marufuku kabisa.

Pia ilisema milo mitatu kwa siku ilitolewa, "ya wingi na aina iliyoidhinishwa na mtaalamu wa lishe". Ilisema kufungwa pingu kwa wafungwa kutafanywa tu "ambapo kuna hatari ya usalama" na "kila siku uchunguzi unafanywa ... ili kuhakikisha kuwa pingu hazijakazwa sana".

Umoja wa Mataifa umesema ripoti za madai ya kuteswa na unyanyasaji wa kingono na wanajeshi wa Israel "zilikuwa kinyume cha sheria na za uasi" na zimewezeshwa na "kutokuadhibiwa kabisa".

Imateafsiriwa na Lizzy Masinga na kuhaririwa na Seif Abdalla