Je, Putin atakuwa hatari zaidi pindi atakapokosa nguvu?

GFGF

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Rais Putin

Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya kwa Masuala ya Kigeni na Sera za Usalama alitoa tathmini yake. Kulingana na Josep Borrell, uasi wa Prigozhin ulidhoofisha nguvu ya Kremlin. Kulingana na yeye, kwa kuwa Urusi inayumba, Umoja wa Ulaya unapaswa kujiandaa kwa hatari kubwa.

"Bila shaka, Putin atatoka katika mzozo huu akiwa amedhoofika. Lakini hatari kubwa zaidi ni Putin dhaifu. Ndio maana tunatakiwa kuelewa matokeo ya jambo hili vizuri sana. Putin amepoteza amepoteza nguvu zake kwa vikosi, na bila shaka yoyote, Urusi isiyo na utulivu ni hatari kubwa," alisema.

Maneno haya ya Josep Borrell yalisikika katika mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya nchini Ubelgiji. Kulingana na chapisho la Europeyskaya Pravda, mkuu wa diplomasia wa Umoja wa Ulaya pia aliunga mkono mawazo yake.

Kwa maoni yake, Putin hivi karibuni ataanza kupigana na wale wanaotilia shaka uaminifu wake kwa mfumo. Borrell alitaja matukio ya hivi karibuni nchini Urusi kama moja ya maswala muhimu katika ajenda ya mkutano huo.

Kulingana na yeye, kutokana na matumizi ya nguvu dhidi ya Ukraine, Umoja wa Ulaya uliichukulia Urusi kama tishio. Lakini sasa umoja huo utalazimika kuzingatia kitisho kipya kutokana na kukosekana kwa utulivu wa ndani nchini Urusi.

Kwa hivyo, swali muhimu ni kile Umoja wa Ulaya unakusudia kufanya, Josep Borrell alijibu kwa kusema Umoja huo hitaji la uchambuzi wa kina. Pia, mashirika ya kijasusi ya nchi zote wanachama yanajishughulisha na kazi hiyo.

Kwa mujibu wa mwanadiplomasia mkuu wa Umoja wa Ulaya, maswali mengi yanabaki bila majibu kuhusu matukio yaliyotokea nchini Urusi, kiafuatacho na athari za uasi huo.

"Jibu letu pekee kwa chochote kinachotokea nchini Urusi ni kuendelea kuunga mkono Ukraine," Josep Borrell alisema.

Nadharia nyingine

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Hapo awali, Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, alisisitiza kwamba bado ni mapema sana kufikia hitimisho juu ya uasi wa Wagner nchini Urusi.

Gazeti la The Times la Uingereza linaeleza Putin anaweza kuamuru kulipua kinu cha nyuklia cha Zaporozhye ili kuimarisha msimamo wake dhaifu.

"Huu ni wakati hatari kwa utawala wa Putin, kwa hivyo wakati tishio kwa eneo hilo pia linaongezeka. Ili kuboresha msimamo wake wa kisiasa, Bw. Putin anaweza kushawishika kuzidisha vita kwa matumaini ya ushindi wa haraka ," gazeti hilo linaandika.

Kinu cha nyuklia cha Zaporozhye ndio kikubwa zaidi barani Ulaya na kwa sasa kiko chini ya udhibiti wa Urusi. Kwa muda mrefu, upande wa Ukraine umekuwa ukizungumzia uwezekano wa Urusi kuhujumu kinu cha nyuklia cha Zaporozhye.

Lakini Urusi ilikataa madai hayo. Kwa mujibu wa gazeti la Times, habari kuhusu kuondoka taratibu kwa wanajeshi na wafanyakazi kutoka kwa kinu cha nyuklia katika siku za hivi karibuni zinathibitisha mawazo hayo.