Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi: Je, Ronaldo kuondoka Al-Nassr?

Ronaldo

Chanzo cha picha, Reuters

Muda wa kusoma: Dakika 3

Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, ambaye leo anatimiza miaka 41, huenda anatarajiwa kususia mechi ya pili kwa Al-Nassr licha ya kuchapisha picha yake akifanya mazoezi, na badala yake akaomba kuondoka katika klabu hiyo ya ya Ligi Kuu ya Saudi Pro mnamo mwezi Juni. (ESPN)

Ikiwa Ronaldo ataondoka Al-Nassr, kuna uwezekano mkubwa wa kurudi katika klabu yake ya kwanza ya Sporting Lisbon. (Fichajes - kwa Kihispania)

Kiungo wa kati wa Ureno Ruben Neves, 28, ambaye alihusishwa na uhamisho wa Januari kwenda Manchester United miongoni mwa vilabu vingine, amesaini mkataba mpya katika klabu ya Saudi Pro League Al-Hilal hadi Juni 2029. (Fabrizio Romano)

Mchezaji wa kimataifa wa England na klabu ya Nottingham Forest, Elliot Anderson, 23, anaongoza orodha ya wachezaji wanaolengwa na Manchester United katika safu ya kiungo wa kati, ambayo pia inajumuisha mchezaji mwenzake wa Three Lions, Adam Wharton, 21, wa Crystal Palace, na mchezaji wa Brighton mwenye umri wa miaka 22, Carlos Baleba, 22. (The Athletic - Usajili unahitajika)

Atletico Madrid iko tayari kumsajili mlinzi wa Tottenham Cristian Romero, 27, kufuatia chapisho la hivi punde la Muargentina huyo kwenye mitandao ya kijamii kuonekana kukosoa klabu hiyo. (Sun)

Mtendaji mkuu wa Newcastle United, David Hopkinson, anasema "hajui ikiwa" wakala wa Sandro Tonali alimpendekeza mchezaji huyo wa miaka 25 kwa Arsenal kufuatia uvumi unaomhusisha kiungo huyo wa kati wa Italia na Gunners siku ya mwisho ya uhamisho. (Talksport)

Elliot Anderson

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mchezaji wa kimataifa wa England na klabu ya Nottingham Forest, Elliot Anderson

Chelsea, Manchester City na Liverpool zina nia ya kumsajili kipa wa Sunderland, Uholanzi, Robin Roefs, huku klabu hiyo ikitarajia ofa zaidi ya pauni milioni 50 kwa mchezaji huyo wa miaka 23. (Football insider)

Klabu ya Ligi Kuu ya Soka LA Galaxy inachunguza njia za kumsajili kiungo wa kati wa Brazil mwenye umri wa miaka 33 Casemiro, ambaye ataondoka Manchester United msimu huu wa joto. (Mail - subscription required)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Beki wa Ufaransa Dayot Upamecano, 27, yuko tayari kusaini mkataba mpya na Bayern Munich ambao utamuweka kwenye kikosi cha mabingwa wa Bundesliga hadi Juni 2030. (Fabrizio Romano)

Wolves wamekubali ofa ya Palmeiras ya pauni milioni 21.6 kwa winga wa Colombia Jhon Arias, na mchezaji huyo wa miaka 28 tayari anajadili masharti binafsi na timu hiyo ya Brazil. (UOL - in Portuguese)

West Ham walikuwa wamekubali mkataba wa pauni milioni 27 kwa mshambuliaji wa Crystal Palace Eddie Nketiah, 26, katika dirisha la uhamisho kabla ya jeraha alilopata mchezaji huyo kusitisha uhamisho huo. (Athletic - subscription required)

Imetafsiriwa na Asha Juma na kuhaririwa na Ambia Hirsi