Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Man City itafanikiwa kumsajili Guehi msimu ujao?

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City inapanga kumsajili beki wa Crystal Palace Muingereza Marc Guehi, 25, kwa lengo kuimarisha safu yao ya ulinzi msimu ujao. (Times - usajili unahitajika)
Klabu za Manchester City, Manchester United na Chelsea zinamfuatilia winga wa Colombia Daniel Munoz lakini Crystal Palace haina nia ya kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (Caught Offside)
Manchester United itajaribu kumsajili kiungo wa kati wa Atletico Madrid na Muingereza Conor Gallagher, 25, wakati wa uhamisho wa wachezaji wa Januari. (Team talk)
Kiungo wa kati wa Bournemouth na Marekani Tyler Adams, 26, ametajwa kuwindwa na Manchester United mwezi Januari au msimu ujao wa joto. (Mail)
Napoli na vilabu 10 vya Ligi Kuu ya England vina nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 20 lakini Manchester United haina wasiwasi kuhusu kuondoka kwake. (Telegraph - usajili unahitajika)
Babake mlinzi wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 16 Mjerumani Cassiano Kiala alisafiri hadi London wiki iliyopita kwa mazungumzo na Chelsea na Manchester City. (Mirror)
Klabu ya Arsenal inavutiwa na mlinda lango wa AC Milan wa Italia Lorenzo Torriani mwenye umri wa miaka 20. (Gazzetta - kwa Kiitaliano)

Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle huenda ikamrejesha mlinzi Muingereza Matt Targett mwenye umri wa miaka 30 kutoka Middlesbrough ambako alikuwa anakipiga kwa mkopo baada ya beki wa Uingereza Dan Burn, 33 kupata jeraha. (The I)
AC Milan imefikia makubaliano ya kimsingi na Niclas Fullkrug, 32, na inatarajia kukamilisha makubaliano na West Ham kwa mshambuliaji huyo wa Ujerumani haraka iwezekanavyo. (Calcio Mercato - kwa Kiitaliano)
Mauricio Pochettino, Oliver Glasner na Marco Silva wako kwenye orodha ya Tottenham kuchukua nafasi ya meneja Thomas Frank ikiwa klabu hiyo itaamua kuachana na meneja huyo wa Denmark. (Caught Offside)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City haina mpangi wa kumuachia kipa Muingereza James Trafford, 23, mwezi Januari ingawa klabu ya Wolves imeonyesha nia ya kutaka kumsajili (Football Insider)
Liverpool inajadiliana na mlinzi wa Ufaransa Ibrahima Konate kuhusu kandarasi mpya na haitamuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 mwezi Januari japo yuko huru kuzungumza na vilabu mwezi ujao. (Team talk)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












