Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Hamas inapata msaada kiasi gani wa fedha na silaha kutoka Iran?
Shambulio la Hamas kusini mwa Israel, limezua maswali kuhusu uwezo wa silaha za Hamas. Hamas iko katika orodha ya makundi ya kigaidi kwa nchi Magharibi na baadhi ya nchi za Kiarabu.
Hivyo msaada wowote wa kifedha kwa shirika hilo hufanyika kwa siri. Ndio maana si kazi rahisi kujua kiasi halisi cha msaada inachokipata kutoka Iran.
Qatar pia inatajwa kuwa msaidizi wa pili wa kifedha wa Hamas, lakini jicho zaidi liko Iran kwa sababu viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu na Hamas, tofauti na mamlaka ya Qatar, hawafichi taarifa kuhusu uhamishaji wa pesa.
Tarehe 14 mwezi wa Bahman 1390, (kwa kalenda ya Iran) - Ayatullah Khamenei, katika khutba zake za sala ya Ijumaa mjini Tehran, alisema:
“Tuliingilia kati kesi za chuki dhidi ya Israel. Matokeo yalikuwa ushindi wa vita vya siku 33 na ushindi wa vita vya siku 22. Baada ya hayo, popote pale ambapo taifa lolote, kundi lolote linapigana dhidi ya utawala wa Kizayuni, sisi tuko nyuma yake na tutalisaidia, na hatuna wasiwasi wa kusema haya."
Pia alisema tarehe 24 Novemba 2018: "Tuliiunga mkono Palestina, tuliwasaidia Wapalestina, tutawasaidia tena, hatuna muhali wala kujificha juu ya suala hili. Ulimwengu wote wa Kiislamu unapaswa kuisaidia Palestina."
Mwenyekiti wa kamati ya uhusiano wa mambo ya nje ya Baraza la Wawakilishi la Marekani hivi karibuni alisema: ''Iran imekuwa ikitoa msaada wa kifedha kwa Hamas na kuwapa mafunzo ya kijeshi kwa miaka mingi.''
Ingawa kuna habari chache sana kuhusu misaada hii, na taarifa zinazorudiwa katika vyombo vya habari zinatokana na makadirio ya mashirika ya kijasusi ya Magharibi.
Aidha, kiasi cha misaada ya kifedha kilichotolewa na Iran kwa Hamas katika miongo miwili iliyopita hakijabadilika, kuna wakati kimeongezeka na wakati mwingine kupungua.
Uhusiano wa Hamas na Iran
Tangu kuasisiwa kwa Hamas miaka ya 1960 hadi leo, uhusiano na urafiki wa Jamhuri ya Kiislamu na kundi hili umekuwa ukipanda na kushuka, lakini hakuna wakati wowote, misaada ya kifedha ya Iran imesitishwa.
Uhusiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu na Hamas uliongezeka tangu 1367 baada ya Jumuiya ya Ukombozi wa Palestina kuitambua Israel, lakini kwa mujibu wa mwanachama mkuu wa Hamas, msaada wa kifedha wa Iran kwa kundi hili ulianza mwaka 1385.
Mahmoud al-Zahar, mwanachama mwandamizi wa kundi la Palestina Hamas, katika mahojiano na Al-Alam TV, idhaa ya Iran ya Kiarabu 2019, alisema baada ya mkutano wake wa kwanza na Qassem Soleimani 2005, alipokea "karibu dola milioni 22."
Alisema Qassem Soleimani alitakiwa kuwapa fedha nyingi zaidi, lakini kwa sababu walikuwa watu 9 na kila begi lilikuwa na uwezo wa kubeba kilo 40 hawakuweza kubeba zaidi, walipokea dola milioni 22 tu.
2009, wakati msururu wa mawasiliano ya kidiplomasia ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani yalipochapishwa na tovuti ya "Wikileaks," moja ya barua hizo ilitaja madai ya afisa wa Misri kuhusu msaada wa Iran kwa Hamas.
Katika barua hiyo iliyoandikwa 2008, ilielezwa kuwa mkuu wa Shirika la Ujasusi la Misri aliaambia Marekani kwamba Iran ilikuwa inawapa Hamas "dola milioni 25 kwa mwezi" lakini Misri iliweza kuzuia msaada huu kuingia Gaza kutoka katika eneo lake.
Kwa mujibu wa madai ya mkuu wa Shirika la Kijasusi la Misri, "Jamhuri ya Kiislamu ilikuwa imewaajiri wakaazi wa jangwani wa Misri ili iweze kutuma misaada ya kifedha na kijeshi kwa Hamas."
Maelezo ya madai haya hayajawahi kuthibitishwa na vyombo huru.
Uhusiano kati ya Hamas na Jamhuri ya Kiislamu ulipungua wakati wa kilele cha mzozo nchini Syria. Na mwanzo wa maandamano dhidi ya Bashar al-Assad, Hamas ilikataa kumuunga mkono Assad.
Baadhi ya vyombo vya habari vya ndani, ikiwa ni pamoja na Tabnak (Desemba 2013), viliripoti kwamba vikosi vya Hamas vimeingia kwenye vita dhidi ya Bashar al-Assad nchini Syria.
Hata hivyo, misaada ya kifedha ya Iran kwa Hamas haikukoma.
Khalid Meshaal, mkuu wa wakati huo wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, katika mazungumzo ya kina na gazeti la Qatar "Al-Sharq" mwezi Disemba 2014, alisisitiza uungaji mkono wa Iran haujakoma katika miaka hii, bali umeathirika.
Al-Monitor iliandika juu ya athari za kupunguzwa misaada ya Iran kwa Hamas: "Kupunguzwa kwa uungaji mkono wa kifedha wa Iran kwa Hamas katika miaka ya hivi karibuni kumeathiri harakati hii na kusababisha shida kubwa ya kifedha.
Hamas ililazimika kufunga taasisi zake kadhaa za vyombo vya habari, kama vile Quds Satellite TV na Kituo cha Habari cha Palestina. Hamas pia ilianza kuwalipa wafanyikazi wake nusu ya mishahara yao au chini ya hapo.’’
Urafiki wenye nguvu na wa kudumu
Baada ya mzozo wa Syria kupungua, uhusiano kati ya Hamas na Jamhuri ya Kiislamu ulizidi kuimarika. Hata hivyo, vyanzo tofauti vilichapisha takwimu tofauti kuhusu kiasi cha misaada ya kifedha iliyotolewa na Iran kwa Hamas.
Mwaka 2020, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitangaza kwamba, kulingana na makadirio yake, kiasi cha msaada huu ni dola milioni 100 kila mwaka.
Lakini vyombo vya habari vya Israel vinadai idadi hiyo ni kubwa. Agosti 2018, Televisheni ya Israel iliripoti: "Wakati wa mkutano uliofanyika kati ya Hamas na Ayatollah Khamenei, Tehran ilionyesha nia yake ya kuongeza msaada wa kifedha wa kila mwezi kwa Hamas hadi kiwango cha dola milioni 30 kwa mwezi."
Idhaa hiyo iliripoti mwaka 2017 kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatoa msaada wa kifedha kwa kundi hili takriban dola milioni 6 kwa mwezi, ambayo ina maana ya dola milioni 72 kwa mwaka.
Ismail Haniyeh, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas alisema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliipa dola milioni 70 harakati hii ya Palestina ili kujenga vikosi vyake dhidi ya Israel na kusambaza roketi zinazozalishwa na vikosi vya Hamas katika Ukanda wa Gaza."
Kulingana na shirika la habari la Reuters, misaada imeongezeka katika miaka michache iliyopita. Katika ripoti iliyonukuu chanzo cha usalama cha Israel, chombo hiki cha habari kiliandika Jamhuri ya Kiislamu iliongeza misaada ya kifedha kwa tawi la kijeshi la Hamas kutoka dola milioni 100 hadi dola milioni 350 kwa mwaka.
Ina maana kwamba anatoa takriban dola milioni 29 kwa kundi hili kila mwezi. Takwimu hii inaendelea mwaka huu pia.
Msaada wa kijeshi
Katika miaka ya hivi karibuni, pamoja na misaada ya kifedha, Jamhuri ya Kiislamu pia ilitoa silaha kwa Hamas.
Oktoba mwaka huu, NBC News iliandika: "Kwa mujibu wa ripoti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya mwaka 2019, Iran inatoa dola milioni 100 kwa Hamas kila mwaka, pamoja na hayo, imetoa teknolojia na maarifa ambayo yanaiwezesha Hamas kujenga ghala lake la kombora huko Gaza kwa kuzingatia miundo ya Iran."
Mwezi Disemba 2013, gazeti la Khorasan lilimnukuu Javad Karimi Qudousi, mjumbe wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na mjumbe wa Bunge wakati huo, na kuandika: "Tulituma makombora 50,000 na maelfu ya makombora ya vifaru huko Gaza."
Katika mwaka huo huo, Mohammad Ali Jafari, kamanda wa zamani wa IRGC alisema: "Iran ilihamisha teknolojia ya kutengeneza makombora ya Fajr 5 hadi Ukanda wa Gaza."
Julai 2018, Ali Khamenei alisema katika mkutano na viongozi wa Hamas huko Tehran: "Si muda mrefu uliopita, Wapalestina walipigana kwa mawe, lakini leo, badala ya mawe wana roketi. Haya ni maendeleo.’’