Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ni silaha gani zinazotumiwa na Hamas dhidi ya Israel katika vita vya sasa?
Licha ya tofauti kubwa ya nguvu za kijeshi kati ya Israel na vuguvugu la Hamas la Palestina, linalodhibiti Ukanda wa Gaza, shambulio la kushtukiza la "Mafuriko ya Al-Aqsa" lililotekelezwa na harakati hiyo Jumamosi, Oktoba 7, limefichua kiwango kikubwa cha silaha bora zaidi na mafunzo.
Miongoni mwao kulikuwa na ndege zisizo na rubani na ndege za maparachuti zilizowabeba wapiganaji wa Hamas hadi umbali wa kilomita 25 ndani ya miji ya Israel, mabomu yaliyoangamiza magari na vifaru vya Israel. Pamoja na makombora mpya ya ulinzi wa anga ya masafa mafupi ya Metabar 1."
Maswali mengi yaliibuka kuhusu jinsi vuguvugu hilo lilivyopata silaha na kuziboresha licha ya kuzingirwa katika eneo la kilomita za mraba 350 chini ya udhibiti mkali wa Israel upande wa baharini, angani na nchi kavu.
Ali Baraka, mkuu wa uhusiano wa kimataifa wa Hamas, aliiambia BBC kutoka Lebanon: "Tuna viwanda vya ndani kwa kila kitu, kwa makombora ya kilomita 250, kilomita 160, kilomita 80, kilomita 10. Tuna viwanda vya kutengeneza mizinga na makombora.’’
Aliongeza: "Tuna viwanda vya kutengenezea bunduki aina ya Kalashnikovs na risasi zao. Tunatengeneza risasi huko Gaza."
Hamas ilikuwa ikitumia makabiliano ya hapo awali na Israel kutengeneza mifumo ya silaha, hasa makombora na ndege zisizo na rubani.
Picha zilizosambaa za operesheni ya "Mafuriko ya Al-Aqsa" zinaonyesha silaha za zamani na za kisasa za wapiganaji wa Hamas, ikiwa ni pamoja na bunduki ya zamani ya Soviet Dushka, ambayo imeboreshwa.
Mtaalamu wa masuala ya kijeshi Meja Jenerali Safwat Al-Zayat anaielezea silaha hii - imeundwa kupenya magari ya kijeshi na ndege, hasa helikopta.
Hamas ilipata vifaa vya silaha hiyo kutoka vyanzo mbalimbali pamoja na maelfu ya bunduki za kivita za Urusi, China na hata za Korea Kaskazini; kutoka Syria, Iraq, au Libya. Silaha zilimiminika Gaza baada ya kuanguka kwa Gaddafi na kuingizwa kimagendo.
Hamas pia ilitumia makombora ya kushambulia vifaru yaliyotengenezwa na Urusi ya Kornet, na makombora yanayoongozwa na mionzi kushambulia vifaru vya Israel vya Merkava.
Vilevile mfumo wa makombora ya kivita ya BULSAE, ambayo yanafaa katika kukabiliana na magari na silaha za Israel, kulingana na Tovuti ya American Insider.
Tovuti hiyo pia ilionyesha kuwa kuna bunduki za masafa marefu, kama vile Austrian Steyr HS.50, ambazo zilionekana katika mikono ya wapiganaji wa Hamas.
Ripoti za Magharibi pia zilizungumza kuhusu wapiganaji wa Hamas kutumia silaha zilizotengenezwa na Korea Kaskazini - mwanachama wa Hamas akionekana kubeba kile kinachoonekana kuwa kombora lililotengenezwa na Korea Kaskazini .Na kirusha roketi kilichobebwa na mmoja wa wapiganaji kilitambuliwa kama F-7 HE-Frag ya Korea Kaskazini.
Kwa mujibu wa tovuti hiyo, Wapalestina wamekuwa wakitumia silaha za Korea Kaskazini, ambazo huenda zilinunuliwa kwa mara ya kwanza na Iran au Syria, na kisha kuingizwa kinyemela katika Ukanda wa Gaza ili kukwepa mzingiro wa Israel uliowekwa tangu mwaka 2007.
Afisa wa zamani wa ujasusi katika Shirika la Ujasusi la Marekani, Bruce E, anasema, "Wasyria wanashirikiana na Hezbollah, ambayo inashirikiana na Hamas, kuingiza silaha Gaza na kutoa mafunzo kwa wanachama wake.’’
Ndege zisio na rubani
Pia waliwalenga wanajeshi wa Israel kwa bomu yaliyotengenezwa nyumbani, na video nyingine ya inaonyesha wakishambulia minara ya ulinzi kwenye eneo la Israel kando ya mpak.a
Meja Jenerali Safwat Al-Zayat alieleza: "Inaonekana ndege zisizo na rubani kwenye video hii zinalenga vihisi vinavyofuatilia uzio unaotenganisha Gaza na Israel. "
Anasema: "Hamas imeingia katika zama za majukwaa ya mapigano yasiyo na rubani. Ilitengeneza ndege zisizo na rubani zenye teknolojia rahisi na hazigunduliwi. Pamoja na vipuri vya pikipiki na magari.’’
Kulikuwa pia na maendeleo ya maandamano ya kujitoa mhanga, kulingana na Al-Zayat, na klipu ya video ilionyesha kuanzishwa kwa maandamano haya na wapiganaji wa Hamas kulenga shabaha zao nje ya mipaka ya Ukanda wa Gaza.
Meja Jenerali Samir Ragheb, mtaalamu wa wa silaha, anaeleza "Hamas ilipata teknolojia kutoka Iran, na ndege zisizo na rubani za "Zwari" zimeundwa kwa kwa vifaa rahisi na kwa gharama nafuu sana’’.
Ndege za maparachuti
Hamas ilisafirisha wapiganaji wake katika ndege za maparachuti katika miji ya Israel wakiwa na silaha na vilipuzi. Kwa mujibu wa ripoti ya mtandao wa Marekani wa CNN, ni vigumu kwa rada ya Israel kuzigundua kutokana na udogo na kupaa chinichini.
Kuhusiana na kiwango cha ufanisi wake, Meja Jenerali Al-Zayat alisema kuuvuka mpaka wa ukuta na mabomu ya chini ya ardhi.
Afisa wa zamani wa CIA anasema, lilifanyika mwaka 1987 na wapiganaji wa Front Front for the Liberation of Palestine, ambalo lilisababisha mauaji ya wanajeshi wengi wa Israel.
Afisa huyo anadai mafunzo ya matumizi ya ndege hizo za parachuti yalifanyika nje ya Gaza na kisha waliopewa mafunzo wakarudi Gaza kuwafunza wenzako.
Makombora
Makombora hayo yanawakilisha nguvu kubwa ya harakati ya Hamas katika vita hivi, na iliweza kutumia makombora ya hali ya juu ya Ayyash 250, yalipiga shabaha za masafa marefu na kufika Tel Aviv.
Meja Jenerali Al-Zayat anaeleza kwamba Hamas "sasa inamiliki silaha za hali ya juu za makombora, Ayyash 250, kombora jipya zaidi katika mfumo wa silaha wa Hamas. Ni maendeleo ya kombora la Iran Fateh 10."
Kuhusu jinsi Hamas ilivyotengeneza mfumo huu, Al-Zayat anasema: “Tangu mwaka 2005 kuondoka kwa Israel kutoka Gaza, Hamas haikuwa na kitu, kisha ikatengeneza makombora ya Qassam 1 na 2, masafa yake hayakuzidi kilomita 19.
Mnamo 2012, Hamas ilifichua kwa mara ya kwanza kombora la M75 lililolenga Tel Aviv, kisha R-160 (Al-Rantisi) lenye masafa ya kilomita 160, na kombora la A-120 (Al-Attar 120). Yameundwa kwa msaada wa Iran na Hezbollah, lakini wataalamu wa Hamas walipata mafunzo nje ya nchi, kulingana na Meja Jenerali Samir Ragheb.
Ragheb alisisitiza kwamba maendeleo hayajumuisha tu mfumo wa makombora, lakini pia "mbinu za kuutumia kuwachanganya Israel. .”
Aliongeza: "Makombora hayo hurushwa kutoka chini ya ardhi, kupitia milango ambayo hufunguliwa kwa ajili ya kurushwa na kisha hufunga tena. Na maeneo hayo ni vigumu kuyagundua."
Meja Jenerali Al-Zayat alifichua "mradi ambao Hamas inafanyia kazi kwa sasa, kwa mifumo ya kuvuruga mawasiliano na mifumo ya ugunduzi. Hilo likitokea, litageuza wimbi la vita. Upatikanaji wa mifumo ya vita vya kielektroniki itakuwa tishio la moja kwa moja kwa Israeli na uwezo wake wa kugundua na kutungua makombora.’’
Ulinzi wa anga
Hamas ilichapisha video ya mfumo wa makombora ya ulinzi wa anga wa "Metabar 1" unaolenga ndege za Israel, pamoja na kundi la wanachama wake wakiwa wamebeba makombora ya ulinzi wa anga mabegani.
Wataalamu wanasema mfumo wa Metbar 1 ni nakala ya mfumo wa Iran wa “Shahab Thaqib” uliotengenezwa kwa msingi wa mfumo wa Kichina wa “HQ-7”.
Lakini makombora ya Hamas hayana uwezo wa kupaa na kugeuka kufuatilia, jambo ambalo linadhoofisha uwezo wa kulenga shabaha. Na yamekusudiwa zaidi kwa helikopta na ndege zisizo na rubani na hazishughulikii na shabaha za juu.