Tetesi za soka Ulaya: Davies yuko tayari kuhamia Man Utd au Real Madrid

Muda wa kusoma: Dakika 3

Wakala wa Alphonso Davies 'amekasirishwa' na jinsi Bayern Munich walivyofanya katika mazungumzo ya kusaini mkataba mpya wa beki huyo wa Canada mwenye umri wa miaka 24 na sasa anataka kusikiliza ofa kutoka Manchester United na Real Madrid , huku mikutano ikipangwa kufanyika Januari. (Bild)

Mawakala wa Manchester City wamemchagua kiungo wa kati wa Valencia na Uhispania Pepelu, 26, kama mtu anayefaa kuchukua nafasi ya Rodri, mwenye umri wa miaka 28, huku akiuguza jeraha. (Football Transfers)

Tyler Dibling wa Southampton anatazamwa na Manchester United na Aston Villa , na kiungo huyo wa kati wa Uingereza mwenye umri wa miaka 18 pia anaaminika kuwa kwenye rada za vilabu vya Ujerumani na Italia. (Sun)

Crystal Palace hawana uwezekano wa kupokea ofa kutoka kwa Manchester City na Arsenal kumusu kiungo wa kati wa Uingereza Adam Wharton, 20. (Football Insider)

Mkufunzi mpya wa Leicester City Ruud van Nistelrooy anatazamiwa kutoa ofa ya mkopo kwa kiungo wa kati wa zamani wa klabu ya Manchester United Toby Collyer mwenye umri wa miaka 20. (Sun)

Celtic wanaweza kutafuta kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Muingereza Carney Chukwuemeka kwa mkopo mwezi Januari. (Football Insider)

Mchezaji wa Bayern Munich Leroy Sane anaweza kupatikana kwa uhamisho wa bila malipo msimu ujao kwa vile 'kumekuwa na mafanikio kidogo' katika mazungumzo kuhusu kandarasi mpya kwa winga huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 28. (Sky Sport Germany - in German)

Barcelona wamejiweka katika nafasi nzuri katika kinyang'anyiro cha kumsajili Jonathan Tah, ambaye mkataba wake unamalizika Bayer Leverkusen msimu ujao wa kiangazi, baada ya kukutana na mawakala wa beki huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 28 wiki hii. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Barcelona pia inawafuatilia mshambuliaji wa Sporting na Uswidi Viktor Gyokeres, 26, na mshambuliaji wa Lille ya Canada Jonathan David, 24, wakati wakipanga kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 36. (AS - in Spanish)

Manchester City waliwahi kutuma ofa ya pauni milioni 35 kwa Barcelona kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi kimakosa, muda mfupi baada ya klabu hiyo kuchukuliwa na Sheikh Mansour mwaka wa 2008. (Star).

Mkufunzi wa Ipswich Kieran McKenna ndiye chaguo la kwanza la Tottenham ikiwa Spurs itaamua kumfuta kazi meneja wa sasa Ange Postecoglou. (Football Transfers)

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi