Mtengezaji saa aliyekosa kazi kutokana na nyakati za kisasa

GG

Chanzo cha picha, Ifiokabasi Ettang / BBC

    • Author, Mansur Abubakar
    • Nafasi, BBC News, Kaduna
  • Muda wa kusoma: Dakika 5

Katika duka la kutengeza saa la Bala Muhammad, mlio wa saa ulianikiza, ukitoa jazanda ya maisha ya baba huyu aliyejulikana kama Baba Bala.

Duka hili liko katikati ya barabara kuu ya Kaduna, mtaa maarufu uliojaa maduka ya vifaa vya ujenzi, na ndani yake kulikuwa na saa nyingi zilizozunguka kila kona, kila moja ikionyesha muda wake, huku akitulia kwenye kiti kidogo kilichozungushwa na meza yake ya kazi.

Baba Bala, mwenye umri wa miaka 68, alikumbuka enzi zilizopita alipokuwa akitengeneza saa kwa haraka, wakati ambapo alikubaliana na wateja wengi waliokuwa wanamletea saa zao kurekebishwa.

"Kuna wakati nilikuwa napokea zaidi ya agugas 100 kwa siku moja," alielezea, akionyesha jinsi biashara yake ilivyokuwa na umaarufu mkubwa.

Lakini, leo, anakumbwa na wasiwasi mkubwa.

"Teknolojia mpya, hasa simu za mkononi, zinauwa biashara yangu," alisema kwa huzuni.

Alijua kuwa, kazi aliyojivunia kwa miaka mingi ilikuwa ikielekea kumalizika, na hofu kubwa ilikuwa ni kwamba maarifa aliyopata kutoka kwa baba yake na nduguye mdogo yangeanza kupotea.

Baba Bala alieleza jinsi alivyofikia hatua hii baada ya kufundishwa na baba yake, Abdullahi Bala Isa, ambaye alijulikana kama fundi wa saa maarufu katika miji mingi ya Afrika Magharibi.

Pia unaweza kusoma:
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Babake Bala alikuwa akisafiri maeneo kadhaa magharibi mwa Afrika kwa zaidi ya miezi sita kuanzia Senegal hadi Sierra Leone kutengezea watu saa zao zilizoharibika.

Kuna wakati Baba Bala alikuwa akiishi jiji kuu la Nigeria, ambapo mabwenyenye na wanasiasa walikoishi ambapo alibahatika kuwaundia saa zao na kupata riziki ya kuridhisha.

Anakumbuka maafisa wa kuu wa serikali walikuwa wakimletea saa zao za mikononi aina ya Rolex zinazothamani ya dola 10,000.

Anasema saa aina hizo huwa zinapendeza na ndio maana anavutiwa na saa za kutoka Uswizi.

Yeye mwenyewe amevalia saa ya mkononi aina ya Longines, na ni ya kutoka uswizi na jinsi anavyoipenda hulala nayo ikiwa mkononi.

"Nikitoka nyumbani kwangu na nikumbuke sijavaa saa yangu hunibidi nirejee nyumbani. Hakika siwezi kaa bila saa yangu - ina umuhimu kwangu."

Katika duka lake amening'inizia picha kubwa ya babake- Abdullahi Bala Isa, aliyopigwa akiwa afisini mwake kabla ya kifo chake mwaka 1988.

Babake Bala ambaye alifariki 1988,alijulikana kusafiri magharibi mwa Afrika kutengezea watu saa zilizoharibika

Chanzo cha picha, Ifiokabasi Ettang / BBC

Maelezo ya picha, Babake Bala ambaye alifariki 1988,alijulikana kusafiri magharibi mwa Afrika kutengezea watu saa zilizoharibika

Isah anajulikana sana na kurekebisha saa zilizoharibika katika maeneo mengi kama vile Freetown na Dakar, na iwapo kuna mrundiko wa saa zilizoharibika hutegemewa kufanikisha uundaji.

Mara kwa mara huzuru mji wa Ibadan ulioko magharibi kusini mwa Nigeria - mji ambao chuo kikuu cha kwanza kiliasisiwa.

Baba bala anasema hakuna anayejua babake alikotoa ujuzi wa kuunda saa - lakini inaaminika alijifunza wakati wa ukoloni wa Muingereza.

Kwasababu Baba Bala alizaliwa miaka minne kabla ya Nigeria kupata uhuru mwaka 1960.

"Babangu alikuwa mtaalam wa kutengeneza saa na alikuwa akisafiri maeneo mengi kuunda saa. Alijifunza nikiwa mdogo na nikaamua kufuata nyayo zake nilipoinukia ukubwani.

"Mimi nilianza kuwa fundi wa saa nilipokuwa na umri wa miaka kumi," alikumbuka Baba Bala, akieleza jinsi alivyovutiwa na saa tangu utotoni.

Aliweza kutengeneza saa na kupata fedha wakati wenzake shuleni walikuwa wanakosa pesa.

"Wakati wenzangu walikuwa wanalia kwa kutokuwa na pesa, mimi nilikuwa na pesa kwa sababu nilikuwa nikifanya kazi."

Anasimulia jinsi ufundi wake wa kuunda saa ulivyovutia mwalimu wake akiwa shuleni: 'Mwalimu alikuwa na saa ambazo zimeharibika na alikuwa amejaribu kuzipeleka kwa fundi zitengenezwe lakini haikuwezekana. Aliponijulisha hayo alinipatia saa zake na nikamtengenezea siku hiyo hiyo.''

Wakati huo, saa zilikuwa zikitambulika kama mavazi ya kila siku- ilikuwa ni vigumu kuona mwanamume ambaye hajavaa saa ya mkononi.

Watu wengi walikuwa wakileta saa zao zitengenezwe na baadhi yao hawarudi kuzichukua

Chanzo cha picha, Ifiokabasi Ettang / BBC

Maelezo ya picha, Watu wengi walikuwa wakileta saa zao zitengenezwe na baadhi yao hawarudi kuzichukua

Lakini maisha ya Baba Bala yalianza kubadilika, kama ilivyokuwa kwa wateja wengi wa zamani.

"Leo, vijana wanatumia simu kutafuta majibu badala ya saa," alisema.

Wakati ambapo biashara yake ilijulikana na watu wa matajiri na viongozi wa serikali, sasa ni vigumu kupata wateja wapya. "Saa za kisasa zinageuza kila kitu," alisema kwa huzuni.

Katika mtaa wa zamani wa maduka ya saa eneo la Kaduna, Baba Bala aliona kuwa maduka mengi yamefungwa, na baadhi ya marafiki zake wameshajiuzulu au wamefariki.

Lakini Isa Sani bado anaendelea na biashara ya kurekebisha saa zilizoharibika .

'Nikienda dukani kwangu kila siku, hukaa bila kupata mteja yoyte siku nzima lakini bado sijakata tamaa tangu mwaka 2019,'' anasema mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 65.

''Nina shamba ambalo watoto wangu hunisaidia kulima na tunajikimu kimaisha kupitia mavuno ya shambani.''

Kwa unyonge anasema:'' hafikirii kuwa kurekebisha saa zilizoharibika itakuwa biashara ya kunoga kama awali.''

Vijana wa eneo hilo, kama Faisal Abdulkarim na Yusuf Yusha'u walio na umri wa miaka 18, walikubali kwamba siku hizi, simu za mkononi zimechukua nafasi ya saa.

"Nikiangalia simu yangu, naweza kujua muda kwa urahisi," alisema mmoja wao.

Dkt. Umar Abdulmajid, mhadhiri wa chuo cha mawasiliano cha Yusuf Maitama anaamini mambo yatabadilika.

''Saa za zamani hazipo tena kwahivyo hakuna shughuli ya kuzirekebisha, lakini kuna saa zinazotumia intaneti zimeanza kuingia kwahivyo zitahitaji fundi wa kuzitengeza zikiharibika.''

Baba Bala alikubali mabadiliko hayo, lakini alijua kuwa anapitia changamoto kubwa.

"Simu na teknolojia ya kisasa vinafifisha biashara yangu, lakini mimi bado nipo hapa na nitaendelea kutoa huduma," alisema, akieleza kuwa biashara yake inahitaji kubadilika ili kuendana na wakati.

Baba Bala hutumia muda mwingi katika duka lake akisikiliza habari kwa njia ya redio

Chanzo cha picha, Ifiokabasi Ettang / BBC

Maelezo ya picha, Baba Bala hutumia muda mwingi katika duka lake akisikiliza habari kwa njia ya redio

"Watu wengi wamekuwa wakileta saa zao zitengenezwe na baadhi yao hawarudi kuzichukua zimejaa hapa,'' anasema Baba.

Lakini Baba Bala amekataa kufunga duka lake - mtoto wake wa kike ambaye huuza nguo na humnunulia kadi za simu ili auze angalau apate kipato cha siku.

Hata hivyo anajivunia kuona mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 12 akitaka kuwa rubani, na alifurahi kuona familia yake inavyoendelea kuona dunia kwa mtazamo tofauti.

Mada zinazofanana:

Imetafasiriwa na Mariam Mjahid na kuhaririwa na Asha Juma