Fahamu ugunduzi bora zaidi wa mambo ya kale uliofanyika mwaka 2021

Chanzo cha picha, AFP
Athari za Covid 19 zitaendelea kuathiri akiolojia ya dunia haswa kwenye viuo vikuu maarufu vya kusomea akiolojia nchini Uingereza, vinavyokumbwa na uhaba wa fedha na watuma maombi ya kujiunga hadi kuchangia idara zingine kufutwa.
Hata hivyo jitihada za kufufua utalii wa utamaduni wa Misri zimeufanya mwaka huu kuwa wenye mafanikio makubwa kwa kugunduliwa miili ya watu wa zamani.
Miili hiyo ya mafarao wa zamani na malkia ilisherehekewa kwa njia yake katika sherehe zilizoandaliwa mwezi Aprili mwaka huu.

Chanzo cha picha, EGYPTIAN MINISTRY OF ANTIQUITIES
Miili ya ajabu iliyogunduliwa kutoka sehemu tofauti duniani
Kuongezea miili kadhaa ya makuhani wa Misri iliyofukuliwa kutoka kaburi la Saqqara kwenye bonde maarufu la Wafalme.
Mwaka huu pia kuna utafiti mpya wa miili maarufu ya zamani kutoka sehemu tofauti duniani. Inatusaidia kuelewa historia ya vipindi walivyoishi.
Ilianza kwa kufukuliwa kwa miili ya miaka 2000 kutoka utawala wa Ptolemy ambao sio wa kawaida kwa sababu una hirizi ya tawi la dhahabu mdomoni mwake.
Inaaminika kuwa hirizi hii inawakilisha sehemu ya mwili, ulimi, ambao uligunduliwa kwa mara ya kwanza katika historia ya Misri.
Wana akilojia bado hawajaelewa ni kwa nini wamisri wa zamani walibuni ulimi huo.

Chanzo cha picha, WARSAW MUMMY PROJECT
Mwili mingine kutoka nchini Misiri mwa huu ulikisiwa kuwa kwa mwanamume kuhani ambaye alifariki miaka 2,100 iliyopita, lakini wakati wana akiolojia walichunguza tena kwa kutumia teknolojia waligundua kuwa mwili huo ulikuwa umefungwa nguo ya kike inayovaliwa na wanawake wajawazito jambo ambalo liliwasisimua watafiti.
Hii ni kwa sababu ulikuwa kama ugunduzi wa kwanza duniani wa mwili ulio na kijusi.
Inabaki kuwa fumbo la ni kwa nini kijusi huyo hakutolewa kama viungo vingine. Huenda upasuaji ulikuwa mgumu au ilikuwa ni imani fulani ya kiroho iliyosema kuwa mama na mtota ambaye hakuwa amezaliwa ni kitu kimoja na hivyo hawangetenganishwa.

Chanzo cha picha, MINISTRY OF ANTIQUITIES / REUTERS
Teknolojia ya hali juu imetuwezesha kufahamu hatma ya "mpiganaji jasiri" Seqenenre Taa II, aliyefariki kwenye vita dhidi ya wavamizi miaka 3,600 iliyopita. Uchungua wa hivi majuzi ulibaini majera mengi mabaya kwenye mwili wake.
Inakisiwa mpiganaji huyo alikuwa amepiga magoti huku mikono yake ikiwa iimefungwa nyuma kabla ya kifo chake ishara kuwa maadui zake walimuu baada ya kushndwa na kushikwa mateka.

Chanzo cha picha, NIELSEN ET AL. / ANTIQUITY 2021
Wacha tuangaliwa miili mingine magharibi mwa Ulaya. Watu wengine huenda wameskia kuwa miili ya watu wa kale iligunduliwa kwa wingi maeneo tofauti. Kwa mfano "Tollund Man", mwanamume wa umri aa makamo aliyeishi zaidi ya miaka 2,400 iliyopita nchini Denmark.
Matokeo ya hivi majuzi kutokana na utifiti wa viungo vya ndani iligunduliwa kuwa Tollundman alikuwa amekula saa 12 hadi 24 kabla ya kifo chake. Kuna kiwango kikubwa cha mimia na vitu vingine. Watu wa kale waliamini kuwa vitu hivi vilikuwa na uhusiano na vitu takatifu.

Chanzo cha picha, WENYING LI / XICRA
Fumbo la mwili kutoka enzi za shaba. Hakuna anayefahamu jinsi ya kupotea katika jangwa la Taklamakan magharibi mwa China. Hivi majuzi wana akiolojia wamegundua kitu kuhusu suala hilo.
Utafiri wa DNA umeonyesha kuwa watu hawa hawakuwa wahamiaji, waliwasili Asia miaka 4,000 iliyopita lakini watoto wa watu walioishi katika bonde la Tarim nchini China karibu miaka 10,000 iliyopita.

Chanzo cha picha, UNMSM
Pia mwaka huu kuna ugnduzi wa hivi punde zaidi ambapo wana akiolojia nchini Peru mwishoni mwa mwezi Novemba walipata mwili unaokisiwa kuwa wa manamume wa umri kati ya miaka 25 hadi 30, katikati mwa mji mkuu Lima.
Mwili huo unaaminiwa kuwa wa miaka 800 hadi 1200 ambacho ni kipindi cha kabla ya kuwasili kwa bar la Ulaya.
Wataalamu wanasema mwili huo huenda ulikuwa wa mtu wa cheo cha juu aliyeheshimika kwa sababu ulikuwa umezikwa eneo muhimu na sadaka kutoka miaka ya nyuma zilikuwa huko.

Chanzo cha picha, Reuters
Maajabu ya bonde la Nile
Ugunduzi mwingine mkubwa wa akiolojia ulifanywa nchini Misri mwaka huu ni mabaki ya mji wa "Aten" au mji wa Dhahabu wa zaidi ya miaka 3,000.

Chanzo cha picha, DR. ZAHI HAWASS ON FACEBOOK
Mji huo wa kali unaaminiwa kuwa mkubwa zaidi kuwai kugunduliwa nchini Misri. Unaaminiwa kuwa ndio ulikuwa mji mkuu wa kibiashara wakati wa kipindi cha Farao Amenhotep III, aliyetawala Misri karibu 1400 BC.

Chanzo cha picha, EPA
Miaka mingi iliyopita wakati Misri ilaanza kama ufalme, watu wanaweza kushangaa kujua kuwa nyakati hizo, tayari kulikuwa na kiwanda kikubwa cha pombeo ambacho kingeweza kuitwa kiwanda kamili.
Mwaka huu mabaki ya kiwanda hicho, cha karibu miaka 5,000 yaligunduliwa katika mji wa kale wa Abydos ulio mwanzo ya mto Nile.
Wana akiolojia waligundua kuwa kiwanda hicho kilikuwa na maeneo 8 ya kupikia pombe kila moja likiwa na majiko 40 yaliyotumika kuchemsha nafaka na maji kabla ya kuchachushwa kuwa pombe.
Utamaduni wa thamani wa ustaarabu wa Wachina
Ugunduzi wa wana akiolojia Mashariki mwa Asia nao sio mdogo. China imegundua mabaki ya kiwanda cha miaka 2,600 katika mkoa wa Henan, kinachoaminiwa kuwa kiwanda cha zamani zaidi ya pesa duniani ambacho hakikuwa kimegunduliwa.
Kinyume na cha pesa zilizotengenezwa kulikuwa na pesa na kijiko kilichotengenezwa kutoka kwa shaba na kutengnezwa kama muudo wa kijiko kikiwa na urefu sentimita 10.
Inaaminiwa kuwa kilikuwa ni kipindi cha utawala wa Zhou kabla ya kuibuka kwa tawala zingine zenye nguvu.

Chanzo cha picha, SANXINGDUI MU
Sehemu za mkoa wa Sichuon kitu kingine kimeguduliwa kutoka kwa utawala wa Shang.
Katika kaburi la mji wa kale wa Sanxingdui, maiaka michache iliyopita, Maelfu ya vitu vya thamani vimegunduliwa huko.
Ukuaji wa akili ya mwanadamu

Chanzo cha picha, DENIS GLICKS
Kuieleza hadithi kwa kutumia picha ilikuwa mwanzo wa ustaarabu wa mwanadamu.
Mapema mwaka huu mchoro wa zamani zaidi wa picha ya mnyama uligunduliwa katika kisiwa cha Sulawezi nchini Indondea na wanaakialojia walitumia kemikali ya uranium.
Mchoro wa picha za kundi la watu wakiwinda inaashira fikra za ndani na ni ishara kuwa ukuaji wa akili ya mwanadamu ulifanyika wakati mmoja kote duniani.

Chanzo cha picha, MAXIME AUBERT














