Wanaume wanahitaji pete ya uchumba pia

f
Maelezo ya picha,

Imeandikwa na Brennan Doherty

Pete ya uchumba ambayo ni Ishara iliyovaliwa kwa muda mrefu na wanawake, kwa sasa inazidi kuvutia wanaume.

Mwezi Aprili mwaka jana, kwenye ufuo wa faragha kando ya mji wa Toronto, niliweka pete ya uchumba kwenye kidole cha mpenzi wangu. Kisha akafanya jambo lisilo la kawaida kwa wanandoa ishirini na kitu wa Marekani : alinivisha pete.

Pete yangu ya uchumba ni duara la upana wa milimita 2 za dhahabu nyeupe ili sawa na ya mchumba wangu. Kwenda bila mtu nilihisi ajabu. Kwa watu wengi, pete kwa jadi imekuwa ishara kwamba mwanamke "alichukuliwa" na mwanamume. Lakini nadhani kwa uhusiano wetu kama washirika sawa - mbinu ya jadi haikufaa kabisa.

Pete za uchumba kwa wanaume ni jambo la kawaida katika nchi kadhaa, ikiwa kama vile Chile , Uswidi na Brazili. Lakini katika sehemu kubwa ya ulimwengu wa Magharibi, ni wanawake pekee wanaopokea pete za uchumba. Hilo linabadilika.

Kwa miaka kadhaa iliyopita, kutokana na kukosekana kwa soko la pete za uchumba zinalolenga wanaume, baadhi ya wanaume wana pete za jadi za harusi, anasema Yagmur Telaferli, mkuu wa mawasiliano ya chapa na maudhui katika kampuni ya vito ya Eternate yenye makao yake New York. Hata hivyo, sasa, makampuni makubwa mbali mbali yamepata wazo la mahitaji, na kuanzisha maduka ya pete za uchumba mahsusi kwa wanaume.

Eternate ilizindua maduka yake mnamo Januari. Zaidi ya hayo, bidhaa nyingi kuu zinazohudumia masoko ya kimataifa - ikiwa ni pamoja na Tiffany & Co na Brilliant Earth - zimeanzisha utengenezaji wa miundo ya pete za wanaume, mara nyingi zikiwa ni pete nene na za almasi iliyowekwa kkwa ukubwa zaidi kuliko za wenzao wa kike. Sawa na pete za wanawake, zinaweza kufikia maelfu ya dola .

h

Chanzo cha picha, Kwa Hisani ya Tiffany & Co)

Maelezo ya picha, Kampuni ya kimataifa ya vito vya thamani ya Tiffany & Co ilizindua safu ya pete za uchumba kwa wanaume mnamo 2021, lebo za bei zikipanda hadi nambari sita

Tobias Kormind, mkurugenzi mkuu wa kampuni ya mauzo ya almasi mtandaoni - 77 Diamonds, yenye makao yake London, anasema mahitaji ya pete za uchumba kwa wanaume yalikuwa karibu na sifuri hadi takriban miaka saba iliyopita. Leo, anakadiria wanahesabu kama oda moja kati ya 30 kutoka kwa wanaume wanaotafuta pete za vito zilizo na almasi au vito vya thamani. "Bado sio bidhaa kuu," anasema, "lakini inaonekana kuwa inakua".

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wataalamu kutoka kwa wauzaji wa vito wanasema wanaume wapenzi wa jinsi moja walikuwa baadhi ya wateja wa kwanza kutafuta pete za uchumba kwa wanaume. "Wapenzi wa jinsi moja wamekuwa wakijaribu kufafanua uchumba wao wenyewe na harusi na kutafuta njia za kuelezea ahadi zao kwa kila mmoja," anasema Joshua Sherman, mkurugenzi wa masoko katika Grown Brilliance, ambayo inaangazia almasi zinazokuzwa katika maabara.

Hata hivyo, mwelekeo umepungua. Baadhi ya watu mashuhuri wakiwemo Ed Sheeran, Ryan Reynolds, Brooklyn Beckham na Michael Bublé wameashiria uchumba wao wenyewe na pete, wakati mwingine wakiwavisha na pete ya harusi baada ya ndoa.

Kwa sehemu, pamoja na soko linaloshamiri la mitindo jumuishi na isiyoegemea kijinsia , wanaume zaidi wanakumbatia vito kwa ujumla. Huko Eternate, vito vya wanaume vilijumuisha 7.2% ya mauzo yote mnamo 2021, anasema Telaferli. Leo, takwimu hiyo ni karibu na 15%. Katika Grown Brilliance, Sherman anasema mauzo ya wanaume yameongezeka maradufu ya viwango vya wanawake wanaonunua bidhaa zao.

Baadhi ya watu pia wanatilia shaka ishara za kitamaduni za pete ya uchumba jinsi mitazamo ya kijamii inavyoendelea. Eddie LeVian, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya vito yenye makao yake New York Le Vian Corp, anaelezea pete ya uchumba ya mwanamume kama kielelezo cha mabadiliko ya mienendo ndani ya mahusiano na mapenzi.

Anavaa pete yake ya uchumba.

"Kama mume ambaye anajivunia kumvisha pete ya uchumba ya almasi, niliyozawadiwa na mke wangu Miranda miaka 38 iliyopita, nimejionea wenyewe jinsi tabia hii inavyozidi kukubalika.", anasema

w

Chanzo cha picha, Kwa Hisani ya Brennan Doherty

Maelezo ya picha, Pete ya uchumba ya mwandishi Brennan Doherty iliuzwa kama pete ya harusi

Mtaalam wa uchumba, kutoka California, Talia Koren, ambaye huandaa podikasti ya Kuchumbian , alimpa mchumba wake wa sasa pete ya uchumba takriban wiki moja baada ya kumchumbia. "Sioni kwa nini, katika uhusiano wa jinsia tofauti, mwanamke huvaa pete lakini mwanamume hafanyi hivyo," anasema. "Kwa nini usiwe na ishara ya kujitolea kwa upande wa mwanamume kabla ya ndoa?"

Koren hamjui kibinafsi mtu mwingine yeyote ambaye ametumia mbinu ya pete ya uchumba mke na mume, lakini kulingana na uchunguzi wake mwenyewe, wanandoa wengine wanaonekana kupendezwa kufanya hivyo. Anafikiri wanataka kuoanisha mchakato wao uchumba na maadili yao. Pia anasema tangu ampe pete mchumba wake, baadhi ya wanawake wamemjia wakisema ni hatua nzuri.

Wauzaji wengi wa vito wanaamini kuwa matumizi haya ya pete za wanaume yataongezeka - hata kuwa ya kawaida, hasa kadri watu wengi zaidi, wakiwemo watu mashuhuri, wanavyoukubali mtindo huu. "Imekuwa sehemu muhimu ya vito kwa wanandoa wengi," anasema Alison McGill, mtaalamu wa chapisho la harusi la Canada The Kit.

Muhimu, LeVian anasema mahitaji ya pete yanamaanisha mapato yatokanayo na pete. "Kwa mtazamo wa biashara, kuongezeka kwa pete za uchumba kwa wanaume kunatoa fursa nzuri kwa watengenezji wa vito na wafanyabiashara kwa pamoja. Pamoja na soko linalokua na hamu ya kutafuta njia mpya za kuonyesha mapenzi, kuna uwezekano mkubwa wa kukidhi ladha na mapendeleo mbalimbali."

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi