Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Daniel Khalifa, mwanajeshi wa Uingereza aliyekuwa na ndoto ya umaarufu na kuwa jasusi wa Iran
Ilikuwa majira ya saa moja unusu asubuhi mnamo tarehe 6 Septemba mwaka jana wakati Sky Walkins alipokuwa akiendesha gari kwenye barabara mbili kusini mwa Wansworth Square ya London.
Hakuamini kile alichokuwa akikiona. Mtu mmoja alitoka chini ya lori lililosimama kwenye njia panda na akaondoka.
Bi Wokins anakumbuka siku hiyo: "Nilimuona akianguka chini, na kisha kutoka, akasimama na kutembea kwa utulivu hadi kwenye barabara ya kando. " Nakumbuka alikuwa na koti lake na alikuwa akifanya kazi ya kawaida sana, kana kwamba hakuna kilichotokea."
Mtu huyu alikuwa Daniel Khalifa, mwanajeshi wa zamani katika jeshi la Uingereza ambaye alipaswa kuwa gerezani wakati huo akisubiri kesi kwa mashtaka ya ujasusi kwa Iran.
Alikuwa amefunga suruari mbili na kuzitumia kama kamba ya kujining’iniza chini ya lori la gereza la vansworth na kutoroka kutoka gerezani.
Asubuhi, Khalifa alikuwa akifanya kazi katika jiko la gereza. Wakati lori la kila siku la utoaji wa chakula lilipowasili, aliondoka jikoni na kujifungia chini ya lori
Wakati lori lilipoelekea eneo la ukaguzi, alisikia mmoja wa wafanyakazi wa jikoni akiuliza, "Mtu huyu yuko wapi?" Eneo la ukaguzi liko kati ya lango la nje na mlango wa gereza, ambapo magari yanayoingia na yanayotoka hukaguliwa.
Dereva wa lori hilo anakumbuka kusikia mmoja wa walinzi wa gereza hilo akisema kuwa kuna mtu alikuwa hajulikani alipo, na walinzi wawili walikagua kwa makini gari hilo mara mbili kwa kutumia taa na vioo, na hatimayewakaruhusu gari kuondoka.
"Nilimwambia mlinzi, 'Je, una uhakika ninaweza kwenda?'" anakumbuka. Kwa sababu nilifikiri kwamba ikiwa mtu amepotea, gereza linapaswa kuwekwa karantini."
Licha ya onyo la usalama, kuondoka kwa Khalifa kutoka gerezani hakukuzuiliwa.
Kutoroka kwake na msako wa siku tatu uliofuatia uligonga vichwa vya habari kote Uingereza, lakini wakati huo ni machache yaliyojulikana kuhusu historia ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 au ni kwanini alikuwa gerezani.
Bado hakuna taarifa rasmi kuhusu jinsi alivyotoroka.
Uchunguzi huru ulifanywa baada ya Khalifa kutoroka, lakini licha ya maombi ya mara kwa mara kutoka BBC, wizara ya sheria ya Uingereza haijatoa matokeo yake.
Khalifa sasa amepatikana na hatia ya kufanya ujasusi kwa serikali ya Iran.
Khalifa alizaliwa mwaka 2001 mjini London na mama Muiran na Uingereza na baba wa Muingereza mwenye asili ya Lebanon. Wazazi wake walitengana haraka sana na hakuwa na mawasiliano na baba yake.
Wengi wa marafiki wa Khalifa alipokuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari kusini magharibi mwa London walitoka katika familia za watu wenye hali nzuri, na alihisi aibu kwa umaskini wa jamaa zake.
Haikuwa rahisi kwake kusoma, lakini aliweza kufaulu masomo ya shule ya msingi na kuanza masomo ya sekondari.
Akiwa na umri wa miaka 15, Khalifa alikamatwa akitumia sumaku yenye umeme kuzima kengele ya usalama iliyoambatanishwa na vitu katika duka ili kuviiba.
"Siku zote nimekuwa na kibarua cha kufichua makosa ya usalama," aliwaambia majaji wakati wa kesi yake ya hivi karibuni.
Alisema mama yake alikuwa mkali sana kwahiyo "alipenda kutoroka" ili "kuhisi uhuru".
Mnamo Septemba 2018, alijiunga na jeshi akiwa na umri wa miaka 16.
Hatua inayofuata ya ajira ya Khalifa katika jeshi ilikuwa kozi ya mafunzo kama karani wa mbali, lakini ndoto yake ya kujiunga na kikosi maalum cha jeshi haikutimia kwani aliambiwa kwamba kwasababu alikuwa nusu Muirani, hakuwa na haki ya kujiunga na kitengo hiki nyeti cha kijeshi.
Wiki chache baada ya kuwasili Dorset, Khalifa aliwasiliana na mwanamume wa Iran aitwaye Hamed Qashqawi kwenye Facebook.
Ili kupata imani ya upande wa Iran, Khalifa alitoa nakala bandia za nyaraka za siri na kumpelekea Qashqawi ili kupata imani ya upande wa Iran na hatua kwa hatua akaanzisha uhusiano nao.
Mwanajeshi wa jeshi la walinzi wa mapinduzi ya Kiislamu aliteuliwa kama mshirika wake, ambaye alitumia jina la msimbo "David Smith" katika mawasiliano yake na Khalifa.
Mnamo mweszi Agosti 2019, mwaka mmoja tangu tangu Khalifa aingie jeshini, alipokea kiasi cha pauni 1,500 kutoka upande wa Irani. Kiasi hicho kiliwekwa katika mfuko wa ukusanyaji wa mbwa katika Mill Hill Park, kaskazini mwa London.
Kile ambacho Khalifa alifanya mara baada ya kupokelewa kutoka upande wa Iran kilikuwa cha ajabu sana. Alijaza fomu ya kuwasilisha habari kwenye tovuti ya huduma ya upelelezi wa ndani ya Uingereza - MI6.
Aliliambia shirika hili kwamba kwa kutoa taarifa za uongo kwa upande wa Iran, alichukua pesa kutoka kwao na kujitolea kuwa "mpelelezi mara pande mbili [wa Iran na Uingereza]".
Khalifa hakufichua kwamba alikuwa mwanajeshi, na idara ya upelelezi wa ndani ya Uingereza haikupanga kazi hiyo kutokana na pendekezo lake.
Akisikitishwa na majibu ya shirika hilo, Khalifa aliendelea na maisha yake kama mwanajeshi kijana, lakini pia aliendelea kuwasiliana na upande wa Iran.
Mwaka mmoja baadaye, mnamo Agosti 2020, Khalifa alisafiri kwenda Istanbul, Uturuki.
Kilichotokea katika safari hii hakijulikani. Inaonekana kwamba safari hii ilifanywa kwa lengo maalum angalau kutoka upande wa Iran.
Nia ya Iran ilikuwa ni kwa Khalifa kusafiri kwenda Tehran, lakini mara chache aliondoka katika hoteli ya Istanbul Hilton - makazi yake.
Khalifa baadaye alimwambia Qashqawi kwamba mawasiliano ya IRGC yalivuruga mipango hiyo lakini akasema kuwa amewasilisha "kitu" kwao.
"Niliwakabidhi kifurushi, lakini nadhani hawajanijibu kwa siku nane," Khalifa alisema katika ujumbe wa sauti kwa Qashqawi.
David Smith, mshirika wa Khalifa nchini Iran, alimuomba awe muangalifu na kuandika katika telegram: "Tunaweza kufanya kazi pamoja kwa miaka mingi."
"Kwahakika," Khalifa akajibu, "Sitaondoka jeshini mpaka utakaponiambia." zaidi ya miaka 25 tangu sasa."
Wakati akiwa jeshini, ikiwa ni pamoja na wakati akiwa katika mazoezi ya kijeshi nchini Marekani, Khalifa alikusanya picha nyingi za vifaa vya mawasiliano vya siri kwenye simu yake ya mkononi ya iPhone - ikiwa ni pamoja na skrini ya kompyuta inayoonyesha anwani ya IP. Haijulikani ni picha ngapi alizotuma kwa Iran kwa jumla.
Wakati wa mazungumzo na mawasiliano yake, ambayo yalirekodiwa kwenye iPad yake, Khalifa alisema alitaka wamfunze kuwa jasusi.
Alisema: "Nataka kupata mafunzo kutoka kwenu na nadhani mahali pazuri pa kufanya mazoezi ni ndani ya Iran."
"Mimi ni mwerevu kuliko kila mtu hapa na nimeshinda tuzo," aliongeza. Mimi ni bora kuliko kila mtu. Mimi ni mjuzi wa yote."
Tuzo ambayo Khalif alikuwa akizungumzia ilikuwa ni tuzo ya mwanajeshi bora kijana katika kitengo chake kidogo, ambapo alipokea kombe la bei nafuu.
Lakini mafunzo na mazoezi yaliyohitajika hakuyapata nchini Iran.
Mwishoni mwa mwaka huo huo, Khalifa alianza kuandaa orodha ya majina ya vikosi maalum tofauti kutoka kitengo maalum cha anga na kitengo maalum cha baharini.
Mwanzoni, alipata tu majina ya mwisho na ya kwanza, lakini alipata likizo ambayo ilimruhusu kupata majina ya kwanza ya watu na kupiga picha za orodha. Picha hizi baadaye zilipatikana kwenye iPhone yake.
Simu zake zilirekodiwa Novemba 9 na Novemba 22, 2021.
Khalifa hakutaja jina lake, lakini alifichua kwamba alikuwa mwanajeshi anayehudumu. Hata hivyo, MI5 haikumuajiri kama "wakala mara mbili" na badala yake, Khalifa alikamatwa katika kambi yake mnamo Januari 6, 2022.
Taasisi za Uingereza hazitajua ni taarifa gani nyeti zaidi ambazo Khalifa alituma kwa Iran.
Ujumbe mwingi aliobadilishana na hadhira yake kupitia programu ya Telegram iliyosimbwa kwa njia fiche umefutwa.
Baada ya kukamatwa kwake, Khalifa aliruhusiwa kuendelea kuhudumu katika jeshi, lakini alipewa majukumu ya kiwango cha chini.
Lakini wakati wapelelezi walipokamilisha kesi yake hatua kwa hatua, alihisi kwamba angekamatwa karibuni.
Khalifa alikuwa hayupo kazini mnamo Januari 2, 2023. Mahakama iliambiwa kuwa aliweka bomu bandia kwenye dawati lake na kuondoka.
Ingawa kifaa hicho hakikuonekana kama bomu halisi, bado kilisababisha kitengo cha utupaji mabomu kuitwa kwenye eneo hilo ili kuhakikisha kuwa ni salama.
Lakini hakuenda mbali na alikamatwa tena Januari 26, 2023, takriban kilomita 11 kutoka kwenye kambi alikotumikia.
Wachunguzi waligundua kuwa alikuwa akiishi katika gari lenye kitanda, na choo kinachobebeka. Pia walipata £ 18,000 pesa taslimu katika gari lake, baadhi yake bandia.
Kwa mujibu wa sheria ya kupambana na ugaidi, Khalifa alituhumiwa kwa kuandaa majina ya watu maalum na kutengeneza na kutega bomu bandia.
Baada ya kutoroka kutoka gerezani, Khalifa aliweza kutoroka kutoka kwa polisi kwa siku chache, lakini hatimaye alikamatwa kilomita 23 kutoka gerezani katika eneo la Northolt.
Kabla ya kesi ya Khalifa, alikuwa amefungwa katika sehemu iliyo hatarini ya gereza la Wansworth kwasababu kulikuwa na hofu kwamba angeshambuliwa na wafungwa wengine.
Mfungwa Chris Jones ambaye aliondolewa mashtaka baada ya kukaa kwa miezi saba huko Wansworth - alimuelezea Khalifa kama "kiumbe wa masafa" ambaye alimwambia "kulikuwa na sifa ya upendo".
Wakati wa kifungo chake, Khalifa alifanikiwa kupata kazi kama msaidizi katika jiko la gereza. Huko, alipata suruali ya jikoni na baadhi ya vipande vya chuma vilivyotumika kulinda kabati za chakula dhidi ya panya, ambazo alizitumia kutoroka.
Baada ya kutoka chini ya lori, Khalifa alienda katika kitongoji cha Richmond moja ya vitongoji vya London na kuiba kofia ya kutoka dukani na kuivaa ili kuepuka kugundulika.
Haionekani kama ana pesa yoyote wakati huu. Lakini usiku huo alimpigia simu mtu kutoka kwa simu ya baa na kumtumia £ 400 pesa taslimu.
Hakuna mtu aliyeshtakiwa kwa kutoa msaada wa kifedha kwa Khalifa, mfungwa aliyetoroka, lakini wachunguzi hawaamini kuwa mawakala wa Iran walimpa pesa hizo.
Aliacha ujumbe kwa mawasiliano yake ya Iran akisema alikuwa "anasubiri" lakini hakupata jibu.
Khalifa alitumia usiku wa kwanza wa kutoroka kwake katika Hifadhi ya Richmond. Labda alitumia usiku wa pili huko Chizik, kilomita chache kutoka kwenye bustani hii, na polisi walipokuja kumkamata, alikaa siku tatu kwenye mitaa ya London Magharibi.
Khalifa alikamatwa siku tatu baada ya kutoroka kutoka gereza la Wansworth mnamo Septemba 2023 kwenye njia ya mfereji kaskazini magharibi mwa London.
Wakati huu, umma ulifahamishwa habari za kutoroka kwa Khalifa kutoka gerezani, na mamia ya watu waliripoti kumuona - baadhi ya wakiwa ni wakweli , na wengi walitoa taarifa zisizo za kweli.
Saa 04:35 asubuhi Jumamosi, Septemba 9, Khalifa alikamatwa wakati akiendesha baiskeli kwenye njia ya mfereji huko Northolt, Kaskazini Magharibi mwa London, na mpelelezi wa nguo za wazi kutoka Idara ya polisi ya kupambana na ugaidi ya London.
Katika sehemu ya kesi yake, Khalifa pia alikiri kutoroka kutoka gerezani.
Baada ya masaa 23 ya majadiliano, jopo la majaji lilimkuta na hatia ya kukiuka sheria ya kuhusu Uyahudi na Sheria ya kupambana na ugaidi. Aliondolewa mashtaka ya kutengeneza bomu katika kambi za jeshi.
Lakini katika kesi hii, kuna swali kwamba ndoto hii - ambaye alitoa zaidi ya miaka 25 ya kazi kwa ajili ya walinzi wa mapinduzi hatimaye ametoa siri kutoka jeshi la Uingereza kwa shirika la usalama wa Iran?
Jopo la majaji katika kesi hiyo lilihitimisha kuwa lilifanya hivyo.
Chanzo cha habari cha wizara ya sheria kimeiambia BBC kuwa ripoti ya Khalifa ya kutoroka jela ilikuwa na taarifa nyeti na uamuzi juu ya kile kinachoweza kuwekwa hadharani utafanywa "katika wiki zijazo".
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi